Ramadhani ituhamasishe kuunusuru Uislam

Wakati tukiwa ndani ya Ramadhani na kujifunga na ibada mbali mbali, tukumbuke kwamba ndani ya mwezi kama huu, Mtume SAAW pamoja na maswahaba zake 313 waliingia katika mapambano makali dhidi ya Makafiri wa Kiqureish katika vita vya Badri vilivyopiganwa mwaka wa 2AH sawa tarehe 17 Ramadhani. Hii ni tofauti kabisa na tunavyouchukua leo mwezi huu wa Ramadhani kuwa ni mwezi wa uvivu na kubweteka kwa kujiachia na kulala mchana kutwa misikitini au kuwa huu ni mwezi wa kusitisha shughuli na kula futari za kila aina tu. La hasha! Huu sio ufahamu wa Mtume SAAW na maswahaba  r.a  Katika vita hivi vya Badri maswahaba wachache waliokuwa na silaha hafifu na duni walikabiliana na jeshi la makafiri 1000 waliojizatiti kwa farasi wa kivita, warusha mishale na wapiganaji mahiri wakiwemo wakuu takriban wote wa Kiqureishi.

Waislamu chini ya Uongozi wa Mtume SAAW walionyesha ushujaa mkubwa katika medani ya vita huku Mtume SAAW akinyanyua mikono yake mitukufu kumuomba Mola Wake Awajaalie ushindi.  Na Allah Taala Akateremsha nusra yake kwa Waumini . Allah Taala anatukumbusha:

إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلاَئِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ

“Kumbuka  Mola wako alipowafunulia Malaika (Akawaambia) “Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu wale walioamini; Nitatia woga katika nyoyo za makafiri. Basi wapigeni juu ya shingo zao na kateni kila ncha ya vidole vyao” (TMQ 8: 12)

Aidha, Allah Taala anazidi kueleza jinsi Alivyowapa Waumini ushindi:

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُمْ بِأَلْفٍ مِن الْمَلاَئِكَةِ مُرْدِفِينَ

“(kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni kuwa: “Kwa yakini Mimi Nitakusaidieni kwa malaika elfu moja watakaofuatana kwa mfululizo (wanaongezeka tu)” (TMQ 8: 9)

Hapa tunapata ithibati na fundisho tosha kwamba dua pekee bila amali  ya kivitendo haitatufikisha kwenye Ushindi. Bali tunahitajika kujiandaa  kwa maandalizi huku tukiomba msaada wa Allah Taala. Maswahaba katika vita hivi walijiandaa upeo wa maandalizi yao na wakajitahidi kwa mbinu mbali mbali za kivita. Kwa mfano, Al-Hubab bin Mundhir alimshauri Mtume SAAW iwekwe kambi ya Waislamu karibu na visima vya maji ambapo wangejenga hodhi la maji, na kuvifukia visima vyengine ili kuwanyima maji maadui watakapofika kwenye uwanja wa Badri. Nae Sa’ad bin Muadh r.a alishauri kujengwe hema litakalokuwa kituo cha Waislamu kupokea maelekezo ya kivita kutoka kwa Mtume SAAW. Mbinu hizi zote zilitekelezwa kwa haraka sana kwa amri ya Mtume SAAW. Na rai ya Al-Hubab ilitekelezwa usiku wa manane. Mbinu hizi  zilichangia kwa kiasi kikubwa kabisa kuwadhoofisha makafiri.

Namna hii ndio ilivyokuwa juhudi ya  Mtume SAAW na maswahaba  katika kujitolea kwao kuuhami Uislamu ndani ya mwezi kama huu wa Ramadhani. Tofauti na leo ambapo Uislamu tumeufanya ni suala la pili, baada ya shughuli zetu za kimaisha.

Mwisho, sisi ndani ya Hizb ut-Tahrir tunawalingania Waislamu kutumia fursa hii adhimu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuungana nasi ili tuongeze kasi ya ulinganizi katika  kurejesha maisha ya kiislamu na watu kuishi chini ya mfumo wa  Kiislamu  utakao andaa jeshi kikweli chini ya bendera ya tawhiid ili kukombowa kila ardhi  yetu iliyoporwa na makafiri  na kufunguwa miji  mingine  kwenda na  kuwakomboa wasio kuwa waislamu kama  wakristo  majusi  baniani   budha  nk  kuwakomboa kutoka kwenye minyororo ya  mabepari wana democrassia   na  kuwaweka  chini ya uislamu  , ni marufuku kuwalazimisha  kusilimu lakini kwa neema uadilifu amani na utulivu  watakao uona  wao wenyewe  wataomba kusilimu bila kulazimishwa  na yeyote ,

 

 

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!