Inna Lillah Waina Illayhi Raajiun

Tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za msiba wa kufariki dunia Sheikh Shamim bin Khamis wa Zanzibar. Msiba huo ulitokea jana usiku Zanzibar baada ya sheikh kuwa mgonjwa kwa muda mrefu.

Maziko ya Sheikh yatafanyika leo Ijumaa baada ya Swalatu Jumaa kijijini kwao Donge, Panga Maua (Zanzibar) na jeneza litaswaliwa hapo hapo.

Sheikh Shamim amewacha pengo kubwa katika safu ya masheikh mahodari, na atakumbukwa daima kwa jitihada yake kubwa ya kuutumikia Uislamu, akiwa mstari wa mbele katika vyombo vya habari mbalimbali Zanzibar katika kutoa ufafanuzi na kueneza elimu ya Uislamu hususan katika masuala ya fiqhi ya miamalati.

Aidha, Sheikh amekuwa na mahusiano mazuri na Hizb ut Tahrir upande wa Zanzibar, ambapo amekuwa karibu sana na wanaharakati wake kwa wakati wote.

Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania tunatoa mkono wa taa’zia kwa familia, ndugu, Waislamu na wanazuoni hususan wa Zanzibar kwa msiba huu mkubwa na pengo kubwa lisilozibika kiurahisi.

Tunamuomba Allah Taala Awape wafiwa ujira mkubwa, Amthibitishe marehemu kwa kaul thabit, Amsamehe, Amjazie penye mapungufu, na Amuingize katika pepo ya Firdaus –
Amiin

04/01/ 2019
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!