Makaburi Yana Utukufu Wake Haijuzu Kuyafukua au Kukaa Juu Yao

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Assalamu Alaykum Warahamatullah Wabarakatuh, Allah Akuhifadhi, Akusaidie na Akunusuru Amir wetu na sheikh wetu,

Sheikh wetu mkarimu, kuna swali muhimu sana kama utaniruhusu, linahitaji jibu ili tujue namna ya kuifanyia kazi maudhui ambayo tumeshajulishwa tayari kuwa itatokea…

Maudhui yenyewe ni kuwa, kuna mradi tayari wa kujenga paneli za umeme wa jua juu ya sehemu za juu za makaburi zilizoinuliwa, na hili ni natija ya tatizo la umeme unalolikabili mji wa Yata huko Alkhalil. Wanataka kuutekeleza mradi huu. Lakini hasa kadhia ambayo nataka kuiuliza ni kwamba wanataka kujenga paneli hizi juu ya ardhi kipimo cha donma 15 za masafa ya mraba kwenye makaburi ya zamani na ya sasa. Je inafaa kuweka paneli hizi kwenye makaburi haya, na pembezoni mwa makaburi na juu ya sehemu za juu zilizoinuliwa(wekwa alama) zinazofunika makaburi? Allah Akulipe kheri.

Jawabu:

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh,

Hakika Mtume (SAW) amebainisha kuwa makaburi yana utukufu, basi haifai kuyafukua au kukaa juu yake au amali yoyote katika amali zinazogusa makaburi kwa jambo linalo ondoa utukufu wa makaburi. Na miongoni mwa dalili za hayo ni:

– أخرج أبو داود من طريق عائشة رضي الله عنها «أَنَّ رَسُولَ اللهِ ﷺ قَالَ: كَسْرُ عَظْمِ الْمَيِّتِ كَكَسْرِهِ حَيّاً». وجاء في عون المعبود شرح سنن أبي داود: قال السيوطي في بيان سبب الحديث، عن جابر رضي الله عنه قال: خرجنا مع رسول الله ﷺ في جنازة فجلس النبي ﷺ على شفير القبر وجلسنا معه، فأخرج الحفار عظماً ساقاً أو عضداً فذهب ليكسره، فقال النبي ﷺ: «لَا تَكْسِرْهَا فَإِنَّ كَسْرَكَ إِيَّاهُ مَيِّتاً كَكَسْرِكَ إِيَّاهُ حَيّاً وَلَكِنْ دُسَّهُ فِي جَانِبِ الْقَبْرِ» أي أن العظم إذا كان موجوداً فيجب المحافظة عليه وإبقاؤه في التراب.

 1.Ametoa AbuDaud kwa njia ya Aisha (RA) “Kwamba Mtume (SAW) amesema: Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja wakati yupo hai”. Na imeelezwa katika kitabu Aun Al-ma’buud sherehe ya Sunan Abu Daud: Suyut amesema katika kubainisha sababu ya hadithi, kutoka kwa Jabir (RA) amesema: Tulitoka pamoja na Mtume (SAW) kwa ajili ya janaza, Mtume (SAW) akakaa juu ya pembe ya kaburi nasi tukakaa pamoja nae. Mchimbaji akatoa mfupa wa muundi au mfupa wa sehemu ya juu ya mkono(humerus) akawa anataka kuuvunja. Mtume (SAW) akasema: “Usiuvunje kwani ukiuvunja akiwa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai lakini uzike pembezoni mwa kaburi”. Yaani ikiwa mfupa utapatikana ni wajibu kuuhifadhi na kuufukia chini.

Kwa hivyo, kuyafukua makaburi ya waislamu haifai isipokuwa mifupa itakapooza na kupotea na kuwa kama mchanga hapo tena inafaa kulima na kujenga juu yake na mengineyo katika amali za halali. Ama itakapokuwa mifupa ipo basi haifai kuyafukua makaburi na kujenga juu yake au kufanya amali nyenginezo, isipokuwa katika hali maalum zinazohusiana na maiti au mfano wake (kama zilivyobainisha hayo nusuus). Ama kiasi cha muda gani unaolazimu kueleweka kwamba maiti ameshaoza na kupotea ardhini, jambo linarudiwa kwa wataalamu uchunguzi hasa wa jambo.

2.Hakuna tofauti kati ya wanavyuoni kwa kauli moja kwamba kukaa juu ya makaburi ikiwa kwa kufanya haja ndogo au haja kubwa kuwa haifai. Na wakatofautiana ikiwa si kwaajili ya hayo… Imeelezwa katika kitabu Al-Mausu’a Al-Fiqhiyyah cha Kuwait:

Wakasema Manahafi nayo ndio madhehebu yao, na Mashafi na Mahanafi ya kwamba inachukiza kukaa juu ya makaburi, kwa yale aliyoyapokea Abu Marthad Al-Ghanawi: Kwamba Mtume (SAW) alisema:

لاَ تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ وَلاَ تُصَلُّوا إِلَيْهَا

Musikae juu ya makaburi na wala musiswali kwa kuyaelekea”.

وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال النّبيّ ﷺ: «لأَنْ يَجْلِسَ أَحَدُكُمْ عَلَى جَمْرَةٍ فَتُحْرِقَ ثِيَابَهُ فَتَخْلُصَ إِلَى جِلْدِهِ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَنْ يَجْلِسَ عَلَى قَبْرٍ». قال الحنفيّة والشّافعيّة: وإن أراد الجلوس أثناء زيارة القبور يجلس بعيداً أو قريباً بحسب مرتبته في حال حياته. وعبارة الشّافعيّة: ينبغي للزّائر أن يدنو من القبر بقدر ما كان يدنو من صاحبه في الحياة لو زاره.

Na kutoka kwa Abu  Huraira (RA) amesema: Kasema Mtume (SAW): “Hakika mmoja wenu kukaa juu ya kaa la moto likateketeza nguo yake  na likapenya kwenye hadi kwenye ngozi yake ni bora kwake kuliko kukaa juu ya kaburi”. Wakasema Mahanafi na Mashafi: Na akitaka kukaa wakati anapozuru makaburi akae mbali au karibu kwa mujibu wa nafasi yake (hadhi yake) katika hali ya uhai wake. Na maelezo ya Mashafi: Inatakikana kwa mwenye kuzuru kulikurubia kaburi kwa kadri alivyokuwa anamkurubia huyo rafiki yake katika uhai pindi anapomzuri.

Na Tahawi katika Mahanafi yeye anaona kuwa inafaa kukaa juu ya makabri, na akainasibisha hii kauli kwa Abu Hanifa, Abu Yusuf na Muhammad, na vilevile ndivyo walivyokwenda maMaliki, kutokana na yale yaliyopokelewa kwamba Ali (RA) alikuwa akiweka kichwa chake kwenye kaburi na akikaa juu yake. Na Tahawi akasema:  Na karaha inaporomoka moja kwa moja ikiwa kukaa ni kwa ajili ya kisomo.) Mwisho.

  1. Basi pakihitajika kuanzisha mradi wa kujenga mapaneli za kuzalisha umeme wa jua juu ya sehemu zilizoinuliwa juu ya makaburi kwenye ardhi ya kipimo cha donma 15 za masafa ya mraba kwenye makaburi ya zamani na ya sasa … itaangaliwa:

Je inawezekana kuachwa sehemu hizi za makaburi zilizoinuliwa juu na kutekelezwa (kujengwa) yale mapaneli  bila ya kudhalilishwa makaburi, au kuudhiwa makaburi, au kufukuliwa au kudhihiri mifupa yake hasa makaburi ya zamani? Mimi nasema hilo liko mbali (yaani haiwezekani)… Ama mukisema kwamba sisi tutafanya pupa tusidhalilishe kaburi lolote na wala haianguki nguzo yoyote katika sehemu hizi zilizoinuka juu ya kaburi lolote katika makaburi mapya, inawezekana kuwa na ukweli katika kauli hii kwa yale makaburi mapya, kwa sababu yanaonekanwa waziwazi inawezekana kuyakwepa… Ama makaburi ya zamani, ikiwa makaburi hayaonekani, vipi itaaminika kukosa kupita juu yake na mfano wa hili?

Kwa hiyo, kwa kuogopa uharamu au kwa uchache ukaraha, jiepusheni na makaburi na tafuteni sehemu nyengine… Allah Ndie Mjuzi zaidi na Mbora zaidi wa hekima.

Ndugu yenu Atta Ibn Khalil Abu Rashta

11, Rabiul Awal, 1440H – 19, November 2018

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!