Takliif Jumla (‘Aam) na Takliif Maalum (Khaas)

بسم الله الرحمن الرحيم

Imeandikwa katika kitabu cha Takatul uk 50: (e-Katika vizingiti vinavyosimama mbele ya dawa ni uzito wa kujitolea mambo ya uhai wa dunia katika mali, biashara na mfano wake kwa ajili ya njia ya Uislamu na kubeba ulinganizi wake. Na ili kuushinda uzito huu akumbushwe muumini kwamba Allah amenunua kutoka kwa waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata pepo. Na utamtosha ukumbo huu na anaachwa mwenyewe achague kuyatoa muhanga mambo haya wala halazimishwi kwa chochote. Mtume (SAW) aliandika barua kwa Abdallah bin Jahsh wakati alipomtuma kuongoza kikosi ili wakawachunguze makureshi huko Nakhla baina ya Makka na Taif, na katika barua hiyo kuliandikwa: “Usimlazimishe yeyote katika wenzio kwenda pamoja nawe, nenda kwa amri yangu pamoja na atakae kufuata”) Mwisho.

Swali:

Zipo Hadithi za Mtume (SAW) zenye kuonyesha kwamba ni wajibu  kwa Muislamu  kumtii mas-ul (kiongozi) wake, na hivi ndivyo tunavyoona katika Hizb yaani kuwalazimisha mashababu kutekeleza majukumu yanayotakikana hata yakiwa mazito kwa shababu bila ya kuachiwa yeye fursa na wala halazimishwi juu ya amali (kuitenda) kama ilivyokuja katika Hadithi… Basi vipi tutafanya muwafaka kile kilichoelezwa katika Takatul kifungu “e” ya kwamba shababu halazimishwi juu ya amali na zile Hadithi ambazo zinamaanisha kwamba ni juu ya shababu kumtii mas-ul wake? Na naomba samahani kwa swali kuwa refu. Jazakallahu Khayra.

Jawabu:

Wa alaykum salaam Warahmatullah Wabarakatuh,

1-Yadhirika umepata mkanganyiko kuhusiana na Takliif. Basi zipo takaaliif jumla (amaa) ambapo mas-ul humtaka kila shababu na ni juu yao kuzitekeleza hali ya kumtii mas-ul muda wa kwamba hizo (takliif) ni katika uwezo wake na zimefungamana na ahkaam za kisheria, anahudhuria halaka kila ya wiki au ya kila mwezi na anafanya mawasiliano yanayohitajika (anakutana na kujadiliana na macontact wake), na anaingiliana na watu kwa mujibu wa mipaka ya takaaliif (majukumu) yaliyoelezwa kwenye faili la idara na maelekezo mengine ya kiidara… Na kuna takaaliif (majukumu) maalumu ambayo hukalifishwa shababu au kundi la mashababu kutenda amali maalumu kama kufikisha barua kwa rais wa nchi fulani, au waende kiujumbe  kwa mtu mwenye nguvu, au waende kutafuta habari maalumu iliyozingirwa na hatari, au kwenda kuzungumza mbele ya makazi ya twaghuti katika matwaghuti au kumkabidhi barua kutoka kwa Hizb…Na mfano wa hayo katika majukumu maalumu, basi amali kama hizi hakalifishwi nazo ila yule mwenye kuzikubali, na akizikubali hukalifishwa kuzitenda na huhisabiwa akizembea baada ya kuzikubali. Na kama hakukubali, basi hafanywi chochote dhidi yake na hatenzwi nguvu, yaani halazimishwi utendaji wake.

Na imeelezwa katika faili la kiidara katika mada “Ta’amiim/Jukumu maalum”: (Hakika kila anaekubali jukumu maalumu basi huwa kafungika nalo, wala hatokubaliwa kutotenda lile alilolikubali kulibeba. Na huzingatiwa kutotenda lile alilolikubali kutenda ni ajizi na ataadhibiwa kwalo)

Na kama unavyoona, pametajwa mwanzo (Hakika kila anaekubali…) yaani kama hajakubali halazimishwi wala haadhibiwi.

  1. Hii ndio hasa maudui. Na ili sura ikae wazi, nakunukulia msafara wa uvamizi wa Abdallah bin Jahsh ili ufahamu kwamba huo msafara wa uvamizi haukuwa ni jukumu jumla (takliif amm) yaani kuwataka waislamu watoke waende kupigana vita kama mfano wa vita vya Tabuk, katika hili Mtume (SAW) aliwataka waislamu watoke waende Tabuk kupigana, na kwa hivyo aliwaadhibu waliokaa nyuma wasiende katika waislamu kwa sababu jukumu hili lilikuwa ni la wote/jumla (amm). Na kumtii mas-ul katika jukumu jumla ni wajibu…

Ama msafara wa uvamizi wa Abdallah bin Jahsh haukuwa wa kuwataka waislamu watoke wakapigane kiujumla, bali lilikuwa jukumu maalum kwa idadi ya watu maalum kwenda kutafuta habari katika mazingira mazito, kwa hivyo mazungumzo ya Mtume (SAW) kwa amiri wao Abdallah yalikuwa kwamba asimlazimeshe yeyote:

Imeelezwa katika kitabu cha Dalaail Al-Nubuwwah cha Baihaqy: Kutoka kwa Ibn Is-haq amesema: Amenieleza Yazid bin Ruman kutoka kwa Urwa bin Zubeir amesema: Mtume (SAW) alimpeleka Abdallah Bin Jahsh huko Nakhla, akamwambia: (Kuwa hapo mpaka utuletee habari yoyote katika habari za makureshi) na wala hakumuamrisha kupigana, hilo lilikuwa katika mwezi mtukufu, akamuandikia barua kabla hajamueleza wapi apite akasema: (Toka wewe na wenzio mpaka mukienda mwendo wa siku mbili hapo fungua barua yako uone kilichomo, nilichokuamrisha kitekeleze na katu usimlazimishe yeyote katika wenzio kwenda pamoja nawe). Zilipopita siku mbili akafungua ile barua, tahamaki mna haya: (Nenda mpaka ufike Nakhla baina ya Makkah na Taif ili utuletee habari za makureshi kwa kile watakacho wasiliana nawe miongoni mwao). Akawaambia wenziwe wakati aliposoma ile barua akasema: Nimesikia na nimetii mwenye kupenda kufa shahid kati yenu basi aende pamoja nami, hakika mimi naitekeleza amri ya Mtume (SAW) na mwenye kuchukia hilo kati yenu basi na arudi, hakika ya Mjumbe wa Allah (SAW) amenikataza kutaka kumlazimisha yeyote kati yenu, watu wakaenda pamoja nae…)

Na katika sira ya Ibn Hisham  (Wakati alipokwenda Abdallah Ibn Jahash kwa siku mbili akaifungua barua na akaiangalia tahamaki kilichomo ni (Utakapoangalia barua yangu hii, nenda mpaka ufike Nakhla baina ya Makkah na Taif hapo kaa uchunguze makureshi na utujuze habari zao) Andallah ibn Jahsh alipoangalia ile barua akasema nimesikia na nimetii, kisha akawaambia wenziwe hakika ameniamrisha Mjumbe wa Allah (SAW) niende mpaka Nakhla nibaki hapo nichunguze makureshi ili nimpelekee habari zao na amenikataza mimi kutaka kumlazimisha yeyote kati yenu basi mwenye kutaka kufa shahidi kati yenu na anaependa hilo  basi aende, na mwenye kuchukia hilo basi arudi, lakini mimi naitekeleza amri ya Mjumbe wa Allah (SAW). Basi akenda na wenzake wakaenda pamoja nae hakuna yeyote aliyeachwa nyuma asiende).

Kama unavyoona, jukumu lile lilikuwa jukumu maalum (khaas) kwa hiyo hakumlazimisha yeyote juu ya jukumu hili, nalo ni jukumu la kupata shahada. Na katika maneno ya hadithi kiongozi wao Abdallah aliwaambia (hakika ameniamrisha Mjumbe wa Allah (SAW) niende mpaka Nakhla nibaki hapo nichunguze makureshi ili nimpelekee habari zao na amenikataza mimi kutaka kumlazimisha yeyote kati yenu basi mwenye kutaka kufa shahidi kati yenu na anapenda hilo  basi aende, na mwenye kuchukia hilo basi arudi, lakini mimi naitekeleza amri ya Mjumbe wa Allah (SAW). Basi akaenda na wenzake wakaenda pamoja nae hakuna yeyote aliyeachwa nyuma asiende). Pamoja na hayo kama unavyoona hakuna yeyote kati yao aliyeachwa nyuma asiende. Yaani pamoja ya kuwa hawakulazimishwa juu ya jukumu hili maalum lakini hakuna yeyote kati yao aliyeachwa nyuma asiende. Allah Awape Baraka.

  1. Sasa turudi katika paragrafu “e” iliyotajwa hapo juu katika kitabu cha Takatul, nayo ipo katika mlango wa maingiliano na ummah na vikwazo ambavyo vipo mbele ya maingiliano haya wakati shababu anapotekeleza amali hii, basi paragrafu hii inahusiana na kujitolea katika mambo ya maisha ya dunia wakati wa kufanya amali hizi za maingiliano. Na amali za maingiliano zinapelekea kufanya amali maalumu zilizozingirwa na hatari, na kuzitenda amali hizo kunapingana na mambo ya maisha ya dunia ambayo ni mali, biashara … n.k. Basi ambae hakubali kutenda majukumu maalumu ambayo yanapatikana katika hatua ya maingiliano halazimishwi kwayo bali huachwa kwa (kutekeleza) amali jumla pamoja na kuendeleza kumkumbusha mambo yanayopelekea uchamungu na kwamba Allah Amenunua kutoka kwa waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata pepo …Na hutosha kumkumbusha hivi na huachiwa yeye uchaguzi katika kujitolea

Na kama unavyoona hakika pametiwa mkazo katika maandishi ya hapo juu kuhusu kujitolea kwa sababu ya uzito wa jukumu maalumu…

  1. Kwa ufupi lile jambo ambalo shababu halazimishwi ni jukumu maalumu (takliif khaas) na lile analolazimishwa ni jukumu jumla (takliif amm), na kumtii mas-ul kwa hili wakati limo katika mamlaka yake na linawafikiana na hukmu za kisharia.

Nataraji picha itakuwa imekaa wazi. Na Allah Ndie Mwenye kuwafikisha

Ndugu yenu Atta Ibn Khalil Abu Rashta

20 Safar 1440H – 29 October 2018

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!