Salamu Za Hizb Ut-Tahrir Tanzania Kwa Kuingia Eid Ul-Fitr

ﺑﺴﻢ ﷲ ﺍﻟﺮﺣﻤﻦ ﺍﻟﺮﺣﻴﻢ

Allahu Akbar Allahu Akbar Allahu Akbar
Hizb ut-Tahrir Tanzania inawapongeza Waislamu kwa kuingia siku tukufu ya Idd ul Fitri na kumalizika Ramadhani. Wakati tukimshukuru Allah SWT kwa siku hii tukufu, tunawaomba Waislamu wasiwakebehi wala kuwadharau wale ambao bado wanaendelea na Swaumu.

Tunamuomba Allah SW atukubalie ibada zetu za funga, visomo vyetu vya Qur-ani, qiyamul-layli, swadaqa na amali nyengine, pamoja na kuturuzuku fadhila zote za mwezi mtukufu na pia kutulipa lililo bora zaidi nalo ni radhi Zake.

Hizb ut-Tahrir Tanzania inawakumbusha Waislamu kutekeleza faradhi ya Zakatul-fitri na sunna zote za idd-ul-fitri kuanzia kutanguliza iftar kabla ya swala, Swala ya idd, kujipamba kwa mapambo halali, kutembelea ndugu, jamaa na kuisherehekea Iddi kwa namna zote halali.
Pamoja na kuwa Idd kuwa ni furaha, Hizb ut-Tahrir Tanzania inawakumbusha Waislamu kuwa wao ni sehemu ya Ummah mmoja kote duniani, na hivyo tuna wajibu wa kuwafikiria Waislamu wenzetu ambao wanaingia katika Idd hii hali ya kuwa wanadhulumiwa kama vile dhulma za wayahudi huko Palestina, mauaji ya Syria, Yemen, Somali, Afrika ya Kati, Myanmar, Turkistan ya Mashariki, Afghanistan nk. Bila ya kusahau ndugu zetu waliowekwa vizuizini katika magereza kwa kisingizio cha sheria ya kibaguzi ya ugaidi hapa Tanzania na duniani kote.

Aidha, tunaukumbusha Ummah wa Kiislamu kuwa idhlali hii na unyonge kama huu hautoondoka ila kwa kuwepo serikali ya Kiislamu ya Khilafah na kuilingania kwake ni faradhi kama zilivyo faradhi nyengine kama Swala, Funga, Zakatul-fitri nk.

Tunawalingania Waislamu katika ardhi kubwa za Waislamu kusimamisha serikali ya Kiislamu (Khilafah) ili tuweze kusheherekea Idd kwa furaha kwa Ummah wote na pia kuzitekeleza hukmu zote zilizobakia kwa ukamilifu wake.
WA KULLU ‘AAMUN WA ANTUM BIKHAIR.

01 Shawal 1440 Hijri
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!