Lini Itakua Hijra Kwa Sura Yake Hasa?

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Swali hili nalilinganisha na zama Mtume (SAW) alipoipata nusra na kuanza kuhama (hijra) kwa maswahaba zake, na yanayotokea sasa huko Al-Sham.

Hizb Tahrir ni chama cha kisiasa kinakwenda kwa mujibu wa njia ya Mtume ili kusimamisha Dola ya Kiislamu, na sasa Hizb inaanza kuifikia nusra huko Syria, na tumeshuhudia hilo kwenye Afisi Kuu ya Habari ya Hizb.

Swali: Kwanini Hizb haiwataki wanachama wake kuhama (hijra) kuelekea Syria kama Mtume (SWA) alivyowataka wanachama wake? Au mazingira/ hali (waqia) inatofautiana? Nataraji utanifafanulia hilo.

 

Jawabu

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh.

Ndio, hakika Mtume (SAW) aliwaamrisha maswahaba kuhama (hijra) kuelekea Madina, lakini hili lilikuwa baada ya Mtume (SAW) kuipata nusra ya watu wa Madina, yaani baada ya Bai’atul Aqaba ya pili, ambayo ndiyo Bai’a kwa ajili ya utawala, yaani Madina imekuwa ni Daar Al-Islam kihukumu kwasababu nguvu zilikuwa zimehakikishwa kwa ajili ya Uislamu na Waislamu, na ilikuwa (nguvu) inasubiri kufika kwa Mtume (SAW) ili iwe (Madina) Daar Islam kivitendo hasa (fi’ilan), zisimamishwe humo ahkaam…

Na itakapo hakikika kwetu kama ile Bai’atul Aqaba ya pili, hapo tena hijra itakuwa kwa sura yake kwa mujibu wa hukmu za sharia.

Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashtah

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!