Mambo Ya Lazima Kwa Harakati Ambayo Inalenga Kuleta Muamko Katika Ummah

بسم الله الرحمن الرحيم

Chama Ambacho Kimejitwika jukumu hili kubwa, nalo ni jukumu la kuamsha ummah kwa kurudisha maisha ya kiislamu. Na hilo ni kwa kusimamisha Khilafah, harakati kama hii haina budi iwe na mambo haya yafuatayo:

Kwanza: Fungamano la kimfumo:

Lazima kupatikane fungamano la kimfumo ili iwezekane kuunda harakati, Na fungamano lenyewe ni Aqidah ya kiislamu, Na thaqafah ya kichama/kiharakati, Ambayo yalazimu iingie katika kiwiliwili cha wanachama, ili iwe ndio fungamano, Na wala isiwe ni kwa ajili ya kanuni za kiidara!!

Pili: Njia ya wazi:

Kadhalika hapana budi kwa harakati iwe Na twariqah/Njia maalum, yenye khatua za wazi, inadhamini njia ambayo harakati inatumia, Kuanzia mwanzo wa Daa’wah mpaka katika kuchukua Uongozi, Na kuutekeleza mfumo, na kuubeba Kama Risala kwa ulimwengu wote!!

Tatu: Kujilazimisha na njia/ twariqa na hapo kuna mazingatio:

Harakati isimame juu ya kufichua Njama za makafiri Na tamaa zao katika biladi za waislamu ili harakati iweze kumakinika kwa kusimama na matendo yake kwa sura kamili katika Mavutano ya kifkra na mapambano ya kisiasa, Na imakinike katika kuileta rai Aam, inayotokana na Waayi Aam Juu ya mfumo na walinganizi wake, ili uwe mfumo ni mfumo wa ummah, Na lengo la harakati ama chama ndio lengo la ummah; ili harakati iweze kumakinika katika kuchukua uongozi wa kivitendo kama ilivyochukua uongozi wa kifikra!!

Nne: Kujua vidhibiti vya chama/harakati navyo ni :

Amiri
Tabanniy
Twaa

Mambo matatu yanayotengeneza harakati:
Fikra
Twariqah na
Mwanadamu

Yanahitaji vidhibiti vitatu kwa ajili ya utekelezaji wa kivitendo katika fikra yaHarakati/chama Nazo:
Amiri
Tabanniy
Twaa

Pasi na haya matatu ya mwisho hakuwezi kupatikana kazi ya kiharakati/chama inayotofautisha na harakati zengine.

Amiri wa harakati/chama Anatabanniy fikra hukmu na Rai, Na katika mbinu ambazo zinapelekea harakati kufikia lengo lake Ambalo imepatikana harakati kwa ajili hio Nayo ni kuamsha ummah juu ya misingi ya mfumo inayobeba, na inabidi wanachama wajilazimishe na hii Tabanniy, watabanniy Aliotabanniy amiri katika fikra na twariqah na katika tabaniy za kanuni ya idara ya chama, wakimtii amiri katika mipaka ya mfumo, kwa sababu mfumo Ambao Wameungana juu yake umempa uweza wa kufanya Tabanniy katika kubeba Da’awah ya kusimamisha Dola.

Na ukampa Amiri haki ya kutiiwa katika hilo, Ndipo Wanafanyakazi wanachama wote kama umbo moja, chini ya uongozi wa Amiri, na kwa fikra alizotabanniy ili kuhakikisha undugu.

Hakika kuwepo na amiri katika harakati, Amiri ambae ana haki ya kutiiwa ni Suala la wajib, kwani hakuna jamaa’h bila amiri, Na hakuna amiri bila twaa’h na twaa’h ya amiri ni wajib katika mipaka alioamrisha Allah, na katika jambo la kushirikiana ambalo amiri ameamrisha.

Amepokea bukhari katika sahih yake kua mtume s.a.w Asema:

“Atakae mtii Amir basi amenitii mimi,Na atakae muasi Amiri basi ameniasi mimi”

Tano: Kudiriki waqiah wa kimaeneo na wakimataifa:

Hapana budi kwa harakati kudiriki kihakika waqiah ambao inafanya kazi ndani yake
Na kudiriki ukweli wa fikra na hisia zilizotanda katika jamii.
Na kudiriki waqia wa kimataifa Na kuhusu wanasiasa na viongozi

Kufahamu mambo yanayoujenga Mujtamah:

Mujtama’h haupatikani kwa mkusanyiko wa watu binafsi kama wanavyodhania wengi, bali wengi wanaojivurumiza katika kubeba daa’wah, Na walinganizi wa kuleta islaah ambao wanasema:
“Anapotengea mtu binafsi jamii nayo hutengea”

Hakika jamii kama tulivyotanguliza maelezo hupatikana kwa vifungu vinne navyo ni :
Watu
Fikra
Hisia
Nidhamu

Saba: Lengo kua maalumu na kufanya bidii katika kazi:

Kwa kupitia haya chama/Harakati itakua imepanga vizuri Lengo lake na kuona Njia yake, na kujilazimisha kwayo, Na matendo yakawa katika mustawa unaotakikana, Kwa namna ambayo lau mambo yatakua marefu kwetu inamkinika kwetu kurudia jambo ambalo linampango maalumu.
Tumelitizama na kulichambua, tukipata upungufu katika matendo ama makosa Tunaliacha, Na tukipata mahala labda tumepaacha katika ijtihad yetu tunapaweka sawa…!!!

Kudiriki Sunnah Ya Allah Katika Kuleta Mabadiliko:

Na hilo ni kwa kupitia Kauli ya Allah taa’la:

لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ ۗ وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُ ۚ وَمَا لَهُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَالٍ

“Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake”.
《 TMQ 13:11》

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!