Vipi Khilafah Itakavyo Waondolea Watu Mzigo wa Ushuru

بسم الله الرحمن الرحيم

  • Ili Kuendesha Mambo Ya Dola Na Watu, Kila Dola Inahitaji Pesa. Chini Ya Urasilimali Pesa Hizi Kimsingi Hukusanywa Kupitia Riba Na Ushuru Wa Moja Kwa Moja Na Usio Wa Moja Kwa Moja. Vile Vile Katika Uislamu, Dola Inapaswa Kufadhili Mambo Na Majukumu Yake Kutoka Kwa Hazina Ya Dola, (Bait Ul-Mal). Ili Dola Itekeleze Jukumu Lililo Wekwa Mabegani Mwake Na Shari’ah, Shari’ah Imeipa Dola Mamlaka Ya Kukusanya Mapato Fulani. Sheikh Ata’ Bin Khalil Abu Rashtah Anaeleza Katika Kitabu Chake, Migogoro Ya Kiuchumi, Yafuatayo: “Mapato Ya Kudumu Ya Bait Ul-Mal “Ngawira Zote Za Kivita, Jizya (Kodi Ya Raia Wasiokuwa Waislamu), Kodi Za Ardhi (Ushr, Kharaj), Khumus Ya Rikaz (Mali Iliyofichwa Chini Ya Ardhi), Mali Za Dola, Pamoja Na Ushuru Wa Forodha Unaochukuliwa Kutoka Kwa Wanaovuka Mipakani Na Tulio Na Vita Nao, Fedha Zinazotokana Na Mali Ya Ummah, Fedha Za Urathi Wa Wale Wasiokuwa Na Warathi, Fedha Za Ghushi Zilizo Nyang’anywa Magavana Na Maafisa Wa Dola, Fedha Zilizo Chumwa Kwa Haramu, Fedha Za Faini, Fedha Za Walioritadi, Na Kodi…”

 

  • * Fedha Za Bait Ul-Mal Kimsingi Zinatosha Zaidi Ya Sana Kukidhi Majukumu Yote Haya. Dalili Za Kiislamu Zinaashiria Waziwazi, Kuwa Utozaji Ushuru Kwa Mujibu Wa Maana Ya Kimagharibi Ya Neno “Ushuru” Ni Haramu. Kwani Rasulullah (Saw) Amesema,

« إِنَّ صَاحِبَ الْمَكْسِ فِي النَّارِ »

“Hakika Mtoza Ushuru Yuko Motoni.”

Na Yeye (Saw) Amesema:

« إِنّ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُم وَأَعْرَاضَكُمْ عَلَيْكُمْ حَرَامٌ كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا فِي بَلَدِكُمْ هَذَاشَهْرِكُمْ هَذَا … »

“Hakika Damu Zenu, Na Mali Zenu Na Heshima Zenu Ni Tukufu Kama Ulivyo Utukufu Wa Siku Yenu Hii Katika Mji Wenu Huu Katika Mwezi Wenu Huu…”

Dalili Hizi Na Nyingi Zaidi Zaeleza Waziwazi Kuwa Shari’ah Imeharamisha Utawala Kutoza Ushuru Juu Ya Waislamu. Uharamu Huu Unakusanya Kila Ushuru, Uwe Ushuru Wa Moja Kwa Moja Au Usio Wa Moja Kwa Moja, Ada Za Mahakama, Au Vitengo, Au Mihuri Ya Uagizaji Bidhaa, Au Ushuru Wa Forodha, Au Ada Za Leseni, Au Chochote Mfano Wake. Dalili Hizi Juu Ya Kadhia Hii Zimeelezewa Kwa Ufafanuzi Katika Kielelezo Cha Katiba Au Dalili Zake Muhimu.

 

* Ni Haramu Kwa Dola Ya Kiislamu Kuchukua Chochote Kutoka Kwa Ummah Ambacho Sio Wajib Juu Yao, Hata Kutoka Katika Utajiri Wao Wa Ziada! Hata Kama Hakuna Chochote Kilicho Bakia Katika Hazina, Dola Inaruhusiwa Pekee Kuomba Kutoka Katika Utajiri Wa Ziada Wa Matajiri Miongoni Mwa Ummah, Na Kisha Kwa Jukumu Lililo Faradhishwa Na Shari’ah Juu Ya Ummah Na Bait Ul-Mal. Na Wakati Huo Pekee, Ambapo Hakuna Chochote Kilicho Bakia Katika Hazina Ya Dola, Dola Inaruhusiwa Kuchukua Kiwango Kinacho Hitajika Na Bait Ul-Mal Na Wala Si Zaidi Ya Hicho. Hivyo Kabla Ya Kuwaomba Matajiri Miongoni Mwa Ummah Usaidizi Wao, Dola Ni Lazima Itumie Kila Dirham Katika Bait Ul-Mal…

Ali (Ra) Alipendekeza Kwa Umar Bin Al-Khattab (Ra) Kusibakie Chochote Katika Bait Ul-Mal Akimwambia: “Ugawanye Utajiri Unaoupata Kila Mwaka, Na Usizuie Chochote Kutokana Nao” (Imeripotiwa Na Ibn Sa’ad Kutoka Kwa Al-Waqidi). Na Imeripotiwa: “Kuwa Ali Alikuwa Akitumia Kila Kitu Katika Bait Ul- Mal Kufikia Hadi Angeifagia Na Kukaa Ndani Yake” (Imeripotiwa Na Ibn Abd Al-Barrin Al-Istidhkar Kutoka Kwa Anas B. Sirin). (Muqaddimat).

* Hizb Ut Tahrir Inaeleza Katika Kielelezo Chake Cha Katiba Ya Dola Ya Khilafah:

Kifungu Cha 147: “Dola Ina Haki Ya Kutoza Ushuru Ili Kutekeleza Lolote Ambalo Shari’ah Imewajibisha Juu Ya Ummah Endapo Fedha Katika Bait Ul-Mal Zitakuwa Hazitoshi Kwani Uwajibu Wa Kulifadhili Utagura Kwa Ummah. Dola Haina Haki Ya Kutoza Ushuru Kwa Ajili Ya Lolote Ambalo Si Wajib Juu Ya Ummah Kulitekeleza, Na Hivyo Hairuhusiwi Kukusanya Ada Za Mahakama Au Vitengo Au Kutimiza Huduma Yoyote.” Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Anafafanua Waziwazi Na Kwa Mkazo Katika Kitabu Chake Pamoja Na Jibu La Swali (Tarehe: 19/05/2016 M) “Wakati Ambapo” Dola Inaruhusiwa Kutoza Ushuru Juu Ya Ummah:

“Hivyo Basi, Utozaji Ushuru Katika Uislamu Unahitaji Kutimiza Masharti Mawili Ili Kuruhusu Utozaji Wake Kwa Ajili Ya Kutekeleza Miradi, Na Kwa Kiwango Kilicho Na Umuhimu Pekee:

1 – Mradi Ni Sharti Uwe Umewajibishwa Juu Ya Bait Ul-Mal, Yaani Juu Ya Dola Na Waislamu, Na Uwajibu Wake Ni Lazima Uwe Umepatikana Kupitia Nasi Ya Kisheria. Hii Ni Mithili Ya Barabara Muhimu, Ambayo Hakuna Badala Yake, Au Hospitali, Wakati Ambapo Hakuna Badala Yake Katika Eneo, Au Viwanda Vizito Vya Mashini Au Mifano Yake Ambayo Kukosekana Wake Husababisha Madhara Kwa Taifa, Kutokana Na Hadith Ya Mtume (Saw): رارض الو ررض ال » » “Hakuna Kujidhuru Wala Kudhuru Wengine.”

2 – Ni Sharti Kuwe Hakuna Fedha Za Kutosha Katika Bait Ul-Mal. Ikiwa Masharti Yote Haya Hayatapatikana, Hairuhusiwi Kutoza Ushuru, Ikiwa Mradi Umewajibishwa Juu Ya Dola Pekee Kama Njia Ya Utekelezaji Mambo Ya Kawaida Ya Watu, Kama Vile Ujenzi Wa Barabara Isiyo Muhimu, Au Ujenzi Wa Hospitali Ya Pili Mahali Ambako Tayari Kuna Hospitali; Katika Hali Hii Fedha Hutumiwa Juu Yake Kutoka Kwa Bait Ul-Mal Endapo Zitapatikana. Vilevile, Ikiwa Mradi Umewajibishwa Juu Ya Waislamu, Lakini Kuna Fedha Za Kutosha, Hapo Mradi Huo Hutekelezwa Kutokana Na Fedha Hizo Pasi Na Kutoza Ushuru.

Lakini, Kama Ilivyo Tajwa Mwanzoni Kabisa Mwa Makala Haya, Kuna Baadhi Ya Aina Za Ushuru Zilizowekwa Na Shari’ah, Kama Jizyah, Ushr Na Kharaj, Ambazo Zitakusanywa Na Khilafah Kwa Mujibu Wa Dalili Katika Uislamu. Hizb Ut Tahrir Pia Imedhibiti Kadhia Hizi Katika Kielelezo Cha Katiba Ya Dola Ya Khilafah:

Kifungu Cha 144: “Jizya Hukusanywa Kutoka Kwa Raia Wasiokuwa Waislamu (Watu Wa Dhimma). Inatakiwa Kuchukuliwa Kutoka Kwa Wanaume Walio Baleghe Ikiwa Wana Uwezo Wa Kulipa, Na Haichukuliwa Kutoka Kwa Wanawake Au Watoto.”

Kifungu Cha 145: “Kodi Ya Ardhi Hulipwa Juu Ya Ardhi Ya Kharaji Kwa Mujibu Wa Kiwango Chake. Zakah Hukusanywa Kutoka Kwa Ardhi Ya Ushri Kwa Mujibu Wa Uzalishaji Halisi.”

Kifungu Cha 149: Mapato Ya Kudumu Ya Bait Ul-Mal Ni: Ngawira (Fei’), Jizyah, Kharaaj, Khumus Ya Hazina Iliyofichwa Ardhini (Rikaz) Na Zakah. Mali Zote Hizi Hukusanywa, Ima Ziwe Zahitajika Au La, Kwa Msingi Wa Kuendelea.”

Dalili Ya Hizi Zimefafanuliwa Katika Kielelezo Cha Katiba Au Dalili Zake Muhimu – Sehemu Ya 2:

*Kharaj Huchukuliwa Kama Badala Ya Matumizi, Kwa Mujibu Wa Uwezo Ardhi Iliyo Nao, Na Hiki Si Kiwango Maalum. Kuna Mambo Kadhaa Ambayo Yanapaswa Kuzingatiwa Wakati Wa Kuamua Kiwango Cha Kharaj Juu Ya Ardhi, Au Juu Ya Mimea Au Matunda Yatokayo Katika Ardhi Hiyo. Hivyo Basi; Rutba Ya Ardhi, Ubora Na Idadi Ya Mavuno/Mazao, Mbinu Za Unyunyiziaji Maji (Mvua, Visima, Mikondo, Mito, Vinyunyizio, Mashini Nk), Eneo La Miundombinu Na Viunganishi, Nk. Yote Ni Mambo Yanayo Paswa Kuzingatiwa Ili Kulinda Ardhi Pamoja Na Wakulima Wake Kutokana Na Madhara Au Utumizi Wa Kupita Kiasi. Pia Rasulullah (Saw) Aliamrisha Kuzingatia Uzito Wowote Kwa Wamiliki Wa Ardhi Kupitia Majanga Ya Kimaumbile Na Uharibifu Wa Mimea: “Punguzeni Tathmini Kwani Katika Mali Kuna Urathi, Anaye Athiriwa Na Hali Ya Baridi Ya Anga (Ariyyah), Kukauka Kwa Mimea Na Majanga Ya Kimaumbile.”

Khalifah Umar B. Al-Khattab Alimuuliza Uthman B. Haneef Na Hudhayfah B. Al-Yaman Baada Ya Kurudi Kutoka Katika Kuitafiti Ardhi Na Kuweka Kiwango Cha Kharaj Nchini Iraq (As-Sawad), Kuhusu Vipi Wameweka Kiwango Cha Kharaj Juu Ya Ardhi Hiyo? Na Kuongeza: “Huenda Mumewabebesha Mzigo Watu Mulio Fanya Kazi Nao Kwa Lile Ambalo Hawawezi Kulihimili?” Hudhayfah Alisema: “Nimewacha Baadhi Ya Ziada.” Na Uthman Akasema: “Nimewaacha Walio Madhaifu, Lau Ningetaka Ningechukua Kutoka Kwao.” (Mali Katika Dola Ya Khilafah Na Sheikh Abdul Qadeem Zalloum). Kuna Ufafanuzi Mpana Uliofafanuliwa Katika Vitabu Vya Hizb Ut Tahrir. Waweza Kuvifikia Katika Linki Niliyoiweka Mwisho Wa Makala Haya …

*Khilafah Haitatoza Chochote Juu Ya Raia Wake, Wawe Waislamu Au Dhimmi Ambacho Hawawezi Kukimudu. Khalifah Umar (Ra) Aliharamisha Unyanyasaji Wa Dhimmi, Ambao Hawana Uwezo Wa Kulipa Jizya. Alisema: “Waacheni Na Wala Msiwatoze Juu Yao Kile Wasicho Kimudu, Kwani Hakika Nimemsikia Mtume Wa Mwenyezi Mungu (Saw) Akisema:

  • « لَ تُعَذِّبُوا النَّاسَ، فَإِنَّ الَّذِينَ يُعَذِّبُونَ النَّاسَ فِي الدُّنْيَا يُعَذِّبهُمُ اللهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ »

“Msiwaadhibu Watu Kwani Hakika Ya Wale Wanaowaadhibu Watu Duniani Mwenyezi Mungu Atawaadhibu Siku Ya Kiyama.’’

Mtume Wa Mwenyezi Mungu (Saw) Alimteua Abdullah Bin. Arqam Juu Ya Jizya Ya Watu Wa Dhimma Na Akasema:

«، أَلَ مَنْ ظَلَمَ مُعَاهِداًأَوْ كَلَّفَهُ فَوْقَ طَاقَتِهِ، أَوِ انْتَقَصَهُ، أَوْ أَخَذَ مِنْهُ شَيْئاً بِغَيْرِ طِيبِ نَفْسِهِ، فَأَنَا حَجِيجُهُ يَوْمَالْقِيَامَةِ » “

“Hakika, Yeyote Mwenye Kumdhulumu Mtu Aliye Chini Ya Mkataba (Mu’ahad), Au Akamkalifisha Juu Ya Uwezo Wake, Au Akamfedhehi, Au Akamnyang’anya Kitu Bila Ya Ridhaa Ya Nafsi Yake, Basi Mimi Nitakuwa Mtetezi Wake Siku Ya Kiyama.” (Mali Katika Dola Ya Khilafah)

Huu Ndiyo Uadilifu Katika Nidhamu Ya Kiuchumi Ya Kiislamu. Khilafah Inashikamana Na Maagizo Ya Mwenyezi Mungu (Swt), Hivyo Basi Hupata Mali Zake Kwa Uadilifu Na Kwa Wingi Bila Ya Kumnyanyasa Hata Mtu Mmoja, Mazingira Au Kiumbe Chochote Chenye Uhai Au Kisicho Kuwa Na Uhai. Hili Ndilo Linalo Hakikisha Kuwa Kila Chenye Uhai Chini Ya Usimamizi Wake Daima Hukidhiwa Mahitaji Yake Yote.

Zehra Malik

Mwanachama Wa Afisi Kuu Ya Habari Ya Hizb Ut Tahrir

Inatoka Jarida La Uqab: 29

Http://Hizb.Or.Tz/2019/07/01/Uqab-30/

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!