Tabani Katika Hizb na Hukmu Zinazohusiana na Mwanamke

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali

Assalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh, amiri wetu

Kila Muislamu anataka kuwa miongoni mwa wanaofanya matendo yao kwa ajili ya Allah tu na kumtii kwa lengo la kupata radhi zake. Lakini je kumtii Allah na mjumbe wake kunalazimisha kuitii Hizb katika kila jambo na ijtihad ambazo mumezifikia na ambazo zina tofauti na zile nilizozitabani kabla… Natoa mfano utupu wa mwanamke akiwa pamoja na maharim zake na pamoja na wanawake Waislamu, wakati baadhi ya wanavyuoni wamekubaliana kwamba ni kutoka kitovuni mpaka kwenye magoti… Vile vile kusoma Quran kwa mwanamke mwenye hedhi ambae wakati mwengine hurefuka kipindi chake??  Nataraji ufafanuzi, kwani ufahamu mbaya na kukosa ufafanuzi hueneza wasiwasi  mwingi na upuuzi baina yetu na mara nyingi kupoteza wakati. Samahani kwa urefu wa swali na msisitizo na nataraji kwa Allah anawirishe uoni wenu na nyoyo zenu.

Jawabu

Waalykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh,

1.Hakika ya jambo la kutabani katika Hizb liko wazi wazi kama jua, tokea kipindi cha awali ilipoasisiwa wakati huo Hizb. Na hakuna mkanganyiko wowote biidhnillah. Mtu ambae amekubali kufanya kazi pamoja na Hizb huwa ana apa anapokuwa mwanachama katika Hizb juu ya kutabani rai za Hizb Tahrir, fikra zake na katiba yake kwa kauli na vitendo. Na kwa muktadha wa kiapo hiki hujifunga nafsi yake na tabani za Hizb, yaani anajifunga kuacha kila rai inayotofautiana na tabani ya Hizb, na anajifunga katika kauli zake na amali zake kwa rai ya Hizb iliyotabaniwa, ni sawa hayo ikiwa katika mas-ala ya kifikra au ya kisiasa au ya kifiqhi au ya kiidara…

2-Kwahiyo, hakika mwanachama katika Hizb si wajibu kujifunga na rai inayotolewa na Hizb katika kila mas-ala, bali ni juu yake kutofautisha baina ya yale yanayomuwajibikia yeye kisharia na yale yanayomuwajibikia yeye kiidara kujifunga nayo, na baina ya yale yasiyomuwajibikia yeye kisharia na kiidara kujifunga nayo. Ni juu yake aulize ikiwa rai fulani maalum ni yenye kutabaniwa au si yenye kutabaniwa… Ikiwa rai fulani maalumu ni yenye kutabaniwa basi hakika ya mwanachama katika Hizb atatabani rai hiyo kwasababu huwa ni rai yake kwa sifa yake kuwa mwanachama na lazima ajifunge nayo kisharia na kiidara kwasababu amejilazimisha mwenyewe juu ya hilo. Ama ikiwa rai fulani maalumu si yenye kutabaniwa, basi hakika mwanachama wa Hizb haimlazimu kuitabani hiyo na kuifanyia kazi…

2-Na natoa mfano wa hayo kwa yaliyokuja kwenye swali:

a-Utupu wa mwanamke mbele ya maharimu zake na mbele ya wanawake Waislamu ni kama ilivyokuja katika kitabu cha Nidhamu ya Kijamii:

(…na inafaa kwa mwanamume kuwatazama wanawake Waislamu maharimu zake na wasiowaislamu zaidi ya uso na viganja vya mikono katika viungo ambavyo huwa ni sehemu za mapambo, bila ya kuvitaja viungo fulani maalumu kwa kule kupatikana nass katika hilo na kwa kule nass hii kuwa mutalaq. Amesema Allah Mtukufu:

﴿وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاءِ﴾.

“Wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao wa kiume, au watoto wa kiume wa waume zao, au ndugu zao wa kiume, au watoto wa kiume wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa kiume wa ndugu zao wa kike, au wanawake wenzao, au wale waliomilikiwa na mikono yao ya kiume (watumwa wao), au watu wazima wanaume wasio na matamanio, au watoto wa kiume ambao hawajajua tupu za kike”. Hawa wote inafaa wao kumtizama mwanamke nywele zake, shingo yake, sehemu ya mkono wa juu (juu ya mirfaq anamovaa vikuku vya mikono), sehemu ya vikuku vyake (sehemu za miguu anamovaa vikuku), na sehemu za kuvaa kidani chake, na vyenginevyo katika viungo ambavyo inaaminika kuwa ni sehemu za mapambo, kwasababu Allah anasema:

﴿وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ

“Wala wasidhihirishe mapambo yao” yaani sehemu za mapambo yao isipokuwa kwa hawa ambao Quran imewataja, hakika yake inafaa kwa hawa kutazama yale yanayodhihiri kwa huyo mwanamke katika nguo zake anazovaa akiwa ndani (thiyaabul-badhla), yaani katika hali ya kazi za nyumbani. Amepokea Al-Shafi katika musnad wake kutoka kwa Zainab bint Abi Salma:

(أنها ارتَضَعتْ من أسماءَ امرأةِ الزبيرِ، قالت فكنتُ أَراه أباً، وكان يدخلُ عليّ وأنا أَمشُطُ رأسي، فيأخُذُ بَعضَ قرونِ رأسي ويقول: أَقْبلي عليّ)

“Kwamba hakika yeye amenyonyesha na  Asma mke Al-Zubair , akasema nikawa namchukulia kuwa ni baba, na alikuwa akiingia ndani nami nachana nywele zangu akishika baadhi ya nywele zangu na akisema: nielekee mimi”. Na imepokewa kwamba Abu Sufyan aliingia kwa mwanawe Ummu Habiba mke wa Mtume (SAW) wakati alipofika (Mtume) Madina ili kuufanya upya tena mkataba wa Hudaibiyyah, akalikunja godoro la Mtume (SAW) ili asilikalie (Abu Sufyan), wala hakujisitiri kutokana na yeye, akalieleza hili kwa Mtume (SAW) akamkubalia, na wala hakumuamuru ajisitiri kutokana na yeye, juu ya kwamba yeye ni mshirikina lakini ni mahrim). Yamekwisha yaliyokuja katika kitabu cha Nidhamu ya Kijamii.

Na hakika tumeeka wazi rai hii katika jawabu la swali la tarehe 13 Rajab 1434H sawa na 23 May 2013 kuhusu maudhui ya utupu wa mwanamke kwa mwanamke mwenziwe. Tukasema hivi katika jawabu

(…kuhusu utupu wa mwanamke kwa mwanamke mwenziwe, kuna rai mbili za kifiqhi ambazo zina njia kutolea dalili:

Kwanza: Kwamba utupu wa mwanamke kwa mwanamke mwenziwe ni kama utupu wa mwanamume kwa mwanamume mwenziwe, yaani ni baina ya kitovu na magoti, na baadhi ya mafuqaha wanasema hayo.

Pili: Kwamba utupu wa mwanamke kwa mwanamke mwenziwe ni mwili wake wote isipokuwa sehemu zile ambazo kikawaida mwanamke hujipamba, yaani kichwa ambayo ni sehemu ya paji,la uso, sehemu ya wanja, shingo na kifua sehemu za kidani, masikio sehemu za herein, mkono wa juu sehemu ya vikuku vya mkono, mkono wa chini (sehemu ya mkono chini ya mirfaq) sehemu ya bangili, kiganja sehemu ya pete, muundi sehemu ya vikuku vya miguu, na nyayo sehemu ya hina. Na zisizokuwa sehemu hizo, yaani zisizokuwa sehemu za mapambo kikawaida kwa mwanamke hizo ni tupu kwa mwanamke mwenziwe. Yaani sio tu baina ya kitovu na magoti…

Na dalili ya hayo ni kauli yake Allah Mtukufu:

﴿وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاءِ﴾.

“Wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao wa kiume, au watoto wa kiume wa waume zao, au ndugu zao wa kiume, au watoto wa kiume wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa kiume wa ndugu zao wa kike, au wanawake wenzao, au wale waliomilikiwa na mikono yao ya kiume (watumwa wao), au watu wazima wanaume wasio na matamanio, au watoto wa kiume ambao hawajajua tupu za kike”.

Hawa wote inafaa wao kumtizama mwanamke nywele zake, shingo yake, sehemu ya mkono wa juu (juu ya mirfaq anamovaa vikuku vya mikono), sehemu ya vikuku vyake (sehemu za miguu anamovaa vikuku), na sehemu za kuvaa kidani chake, na vyenginevyo katika viungo ambavyo inaaminika kuwa ni sehemu za mapambo, kwasababu Allah anasema

﴿وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ

“Wala wasidhihirishe mapambo yao” yaani sehemu za mapambo yao.

Na katika Aya wametajwa maharimu pia wametajwa wanawake, basi inafaa kutazama kwenye sehemu za mapambo katia ya wanawake wao kwa wao. Ama zisizokuwa sehemu za mapambo zitabakia ni utupu kwa mwanamke mbele ya mwanamke mwengine.

Hii (rai) ndio yenye nguvu (raajih) kwetu kwa mujibu wa dalili hizo. Na tunasema yenye nguvu (raajih), kwasababu wako wanaona kwamba utupu wa mwanamke kwa mwanamke mwengine ni kama utupu wa mwanamume kwa mwanamume mwengine, yaani baina ya kitovu na magoti.) Yamekwisha yaliyokuja katika jawabu la swali.

Na yaliyokuja katika kitabu cha Nidhamu ya Kijamii yametabaniwa kwasababu kitabu cha Nidhamu ya Kijamii kimetabaniwa kama inavyojulikana na kila mwanachama katika Hizb… Na pia yaliyokuja katika jawabu la swali yametabaniwa vilevile kwasababu yanaweka wazi na kusherehesha yaliyotabaniwa… Na ni juu ya kila mwanachama katika Hizb achukue rai hii iliyotabaniwa na awache rai ambayo alikuwa akiisema au akiichukua…

b-Maudhui ya kusoma Quran kwa mwenye hedhi imeelezwa katika jawabu letu la swali lililowekwa kwenye kurasa za mtandao lilotiwa saini kwa jina letu lenye tarehe 01 Rabiu Thani 1436H sawa na 21/01/2015, na yamekuja humo yafuatayo:

(Kusoma Quran kwa mwenye hedhi ni mas-ala yenye maelezo ya tofauti (khilaf) baina ya wanavyuoni, wengi wa wanavyuoni wanasema ni haramu, na wapo wanaojuzisha kwa maelezo na sharuti kadhaa…

Na ninayoitia nguvu (tarjiih) ni kwamba haifai kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma Quran, kwa kauli ya Mjumbe wa Allah (SAW):

«لَا تَقْرَأُ الْحَائِضُ وَلَا الْجُنُبُ شَيْئاً مِنَ الْقُرْآنِ»

“Hasomi mwenye hedhi wala janaba chochote katika Quran”. Imepokewa na Tirmidhi. Na hadithi hii hata kuwa pamepokelewa kwayo kauli kadhaa, ila hakika wengi wa mafuqahaa wanaichukua hadithi hii. Pamoja na hayo imepokelewa hadithi sahihi kuhusu uharamu wa kusoma Quran kwa mwenye janaba, na mwenye hedhi ni kama mwenye janaba katika mas-ala haya. Ametoa Abu Daud na Al-Nasai , na katika riawaya ya Ibn Majah mfano wa hiyo kutoka kwa Ali (RA) amesema:

: «كَانَ النَّبِيُّ يَخْرُجُ مِنَ الْخَلَاءِ فَيُقْرِئُنَا الْقُرْآنَ وَيَأْكُلُ مَعَنَا اللَّحْمَ، وَلَمْ يَحْجُبْهُ – أَوْ يَحْجُزْهُ – عَنِ الْقُرْآنِ شَيْءٌ لَيْسَ الْجَنَابَةَ».

“Mtume (SAW) alikuwa anatoka chooni anatusomea Quran na anakula nasi nyama na hakijamzuia chochote kutokusoma Quran isipokuwa janaba”

Na ni wazi katika hadithi kwamba janaba huzuia kusoma Quran, yaani haramu kusoma Quran kwa mwenye janaba, na mwenye hedhi ni kama mwenye janaba, basi huwa ni haramu juu yake kusoma Quran kama ilivyo haramu kwa mwenye janaba kusoma Quran). Limekwisha jawabu la swali.

Na majibu ya maswali ambayo yanatolewa na Hizb si yenye kutabaniwa isipokuwa katika hali tatu: Itakapokuwa yametiwa saini kwa jina la Hizb, au likiwa jawabu linatokana na Hizb ni maoni ya chenye kutabaniwa kama kusherehesha, au tafsiri yake na mfano wake, au (hali ya tatu) Hizb ikiyatuma kwa maeneo ili wapewe mashababu wa Hizb… Kama ilivyokuja katika Faili la Kiidara – yaliyotabaniwa.

Na ni wazi kwamba jawabu la swali ambalo tumelitoa kuhusu kusoma Quran kwa mwenye hedhi halipo katika hali yoyote ile miongoni mwa hali tatu zilizooneshwa punde hivi… Kwahiyo, jawabu hili halijatabaniwa na si wajibu kwa wanachama wa Hizb kulitabani na kulifanyia kazi si kisharia wala kiidara. Na juu ya mwanachama wa Hizb kubakia katika mas-ala haya kwenye rai yake ambayo aliyokuwa akienda nayo na kuitabani…

3-Kwahiyo, mas-ala ni mepesi mno na hayatatizi. Yote yaliyomo katika hili jambo ni kuwa mwanachama afahamu ikiwa rai ambayo inatolewa na Hizb ni yenye kutabaniwa au si yenye kutabaniwa. Ikiwa ni yenye kutabaniwa basi ni hakika ajifunge nayo na awache kila rai nyengine isiyokuwa hiyo, na ikiwa si yenye kutabaniwa, basi hakika yeye halazimiki kuitabani na kuifanyia kazi… Na mambo yaliyotabaniwa yanajulikanwa na wazi kwa kila mwanachama katika Hizb… Na yanayohusiana na majibu ya maswali ni kama tulivyotaja punde tu, kwamba majibu ya maswali si yenye kutabaniwa isipokuwa katika hali tatu zilizooneshwa hapo juu…

4-Pamoja ya kwamba kile kinachotolewa na Hizb ambacho si chenye kutabaniwa Hizb haiwalazimishi wanachama wake kukitabani, isipokuwa Hizb inaona uzuri mashababu wake wajifunge na yote yanayotolewa na Hizb, kwasababu yanayotolewa na Hizb yote huwa baada kudurusu (kutafiti), kupata kilichosafi, kuhakiki, na hutumiwa juhudi kubwa kwajili yake kabla ya kuyategemea…

Nataraji suala hili litakuwa limefafanulika hivi sasa na umetulia ukomo wa wasiwasi, upuuzi, na kupoteza wakati ambayo umeyataja katika swali…

Ndugu yenu Atta ibn Khalil Abu Rashtah

18 Dhulqada 1440H

21/07/2019

 

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!