Mzozo wa Amerika na Ulaya ndani ya Sudan

Swali:

Imebainika kuwa maafisa wa Ulaya wamemiminika ndani ya Sudan na kutangaza kuinusuru serikali ya Hamdouk. Mnamo 16/9/2019, Waziri wa Kigeni wa Ufaransa aliwasili Khartoum na kukutana na Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdouk na kutangaza msaada wa Uro milioni 60 kwa Sudan na kwamba itafanyakazi kuiondosha Sudan katika orodha ya Ugaidi. Waziri wa Kigeni wa Ujerumani naye akawasili na kutangaza vivyo hivyo kuhusu orodha ya Ugaidi… Je mawasiliano na misaada hii ni kuuimarisha muungano wa Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko mbele ya jeshi? Au ni kwa malengo mengine? Waziri Mkuu wa Sudan Abdullah Hamdouk alitangaza mnamo  5/9/2019 kuundwa kwa serikali ya kwanza tangu kupinduliwa kwa Bashir mnamo Aprili (serikali itafanyakazi kwa miaka mitatu ya kugawanya madaraka iliyotiwa saini mnamo mwezi uliopita baina ya jeshi na raia… France 24, 5/9/2019) Je makubaliano ya kugawanya madaraka yanatarajiwa kutuliza au vurugu zitarudi tena kwa mara nyingine?

Jibu:

Ili kuweka wazi jibu tunatathmini yafuatayo:

1-Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko kwa msaada wa Uingereza, vyombo vyake vya habari na vibaraka wake wa eneo waliweza kuyateka nyara mapinduzi kutoka kwa watu ambao waliasi dhuluma, njaa, kunyimwa na ufisadi na kurudi nyuma na wala ha- wakuweza kuweka suluhisho msingi kutatua masuala hayo bali ilitoa suluhisho kutoka ndani ya uhalisia uleule ulio na ufisadi. Mazungumzo yalifanyika baina ya baraza la kijeshi lililoegemea mrengo wa Amerika na vibaraka wake na Ulaya ikipigia upatu Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko. Makubaliano sainiwa baina yao juu ya hati ya kikatiba mnamo 17/8/2019… Kwa hivyo waandamanaji walijitoa muhanga pasina mafanikio. Makubaliano hayo yalikuwa ni muendelezo wa uhalisia wa ufisadi kwa misingi ya Umagharibi usekula dhidi ya Uislamu na hukmu zake! Makubaliano baina ya Baraza la Kijeshi na Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko yalijumuisha wanachama 11 Baraza la Ubwana kwa mgao wa 5+5 pamoja na raia huru ambaye atakubaliwa na pande husika wakati wa mpito kwa muda wa miezi 39.

Makubaliano pia yalisema kwamba Baraza la Kijeshi litachukua hatamu ya kwanza kwa muda wa miezi 21 na Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko yatachukua hatamu kwa miezi 18. Muda wa mpito utafuatiwa na uchaguzi mkuu na kubuniwa kwa baraza utungaji sheria. Makubaliano hayo yalisema kwamba uchaguzi wa mawaziri wa ulinzi na usalama wa ndani uwe ni haki ya kitengo cha usalama cha Baraza la Ubwana kwa maana kuwa kitengo hicho kitabakia chini ya jeshi, usalama na ujasusi kando na kusimamiwa na Baraza la Ubwana kwa muhula wa kwanza.

2- Hivyo basi, nguvu za jeshi lililoko uongozini zinajumuisha sehemu asili ya jeshi. Wapo wanachamawatano wa jeshi katika baraza na wawili katika baraza la mawaziri (waziri wa ndani na waziri wa ulinzi). Mmoja ni Jenerali Jamal al-Din Omar, Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Mpito, akiwa ni mmoja wa wanajeshi wakongwe wanaotumikia jeshi hivi sasa. Jenerali Jamal al-Din Omar alikuwa ni rafiki wa karibu wa waziri wa ulinzi, Awad bin Auf aliyefanyakazi kwa muda mrefu ndani ya Huduma ya Kijeshi ya Kijasusi na wenziwe katika Chuo cha Kijeshi walikuwa ni Abdel Fattah al-Burhan na Mkurugenzi Mkuu wa  Kijasusi, Abu Bakr Dumblab na Omar Zain al-Abideen.

Hii inamaanisha kuwa utawala wa mwanzo utawakilishwa kwa nguvu kwa muhula wa mpito na utaweka vikwazo na vizingiti vingi katika kufaulisha malengo ya serikali ya raia ya Ulaya “Uingereza”…  Na hivyo basi upande wa Amerika utabakia wenye nguvu…

3- Abdullah Hamdouk, aliye na mastaz na doktoreti katika uchumi kutoka Chuo cha Uingereza cha Manchester na aliteuliwa na Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko kama Waziri Mkuu mnamo 20/8/2019 napia mamlaka kamilifu yakapewa Baraza la Mawaziri. Mnamo 5/9/2019 kukatangazwa uundwaji wa serikali inayotarajiwa kuongoza muhula wa mpito kwa miezi 39. Hivyo basi Waziri Mkuu atakuwa mtiifu kwa Uingereza na Ulaya na atatenda kwa mujibu wa muongozo wa Ulaya kinyume na Mwenyekiti wa Baraza la Ubwana na Kamanda wa Jeshi Abdel Fattah Al-Burhan na naibu kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka Mohammed bin Hamdan Daglo pamoja na wanajeshi wanaogemea mrengo wa Amerika ambao watafanyakazi kwa muongozo wa Amerika.

4- Utawala ndani ya Sudan kwa mujibu wa hati ya kikatiba inakaribia kujumuisha timu mbili zilizo na nguvu na utiifu wa kigeni tofauti na hili litajidhihirisha katika utendajikazi wao katika kusuluhisha matatizo ya watu na usalama wa maisha yao. Kila mmoja atakuwa na hamu ya kuhudumikia muongozo anaoufuata na kila mmoja atasubiri kupatikane fursa kumuondosha mwenziwe kwa kutumia njia za kindani na kinje. Kubuniwa kwa mabaraza  kama hayo ndani ya Sudan inajulikana kutokana na mahusiano ya mpito na majanga yake…mpaka pale jeshi litakapopangilia mambo ya dola na kuvunja baraza na kumuweka rais wa nchi kutoka katika maafisa wa kijeshi. Hili liko wazi kutoka kwa Baraza la Ubwana mnamo 26/12/1955 ambalo lilichukuwa madaraka baada ya “uhuru” wa Sudan mnamo 1/1/1956. Uliendelea mpaka 17/11/1958, wakati Luteni Jenerali Ibrahim Aboud alipokwenda kinyume dhidi yake…and kutokea kwa mapinduzi ya Nimeiri mnamo 1969 kisha mapinduzi ya Omar Al-Bashir mnamo 30/6/1989… Kisha kupinduliwa kwa Al-Bashir na kuundwa kwa Baraza la Ubwana… Mabaraza haya daima yamehusishwa na mizunguko ya mizozo baina ya Amerika na Muingereza na kila mmoja akiwa makini kuunda serikali pekee lau itakuwa hawezi basi hujiunga na mwengine mpaka pale atakapopata nafasi ya kumuondosha mwengine kama ilivyokuwa hapo zamani wakati Amerika ilikuwa kimya kuhusu uwaziri mkuu wa mrengo wa Muingereza Sadiq al-Mahdi ili kuweza kuzimeza harakati maarufu wakati huo na ilipofaulu ili waagiza wanaume wake jeshini kisha wakaja kumpindua Al-Bashir mnamo 1989.

Na wakati Al-Bashir aliposhindwa kudhibiti harakati maarufu ikamuondosha kama ilivyofanya waliomtangulia, Nimeiri na Mubarak na wengine pasina kuzingatia huduma walizotoa! Baada ya Al-Bashir Amerika ilikuja na Baraza la Kijeshi… Na sasa mchezo unarudiwa tena katika Baraza la Ubwana, kwa hivyo jeshi la mrengo wa Amerika lazima kukubaliana na vibaraka wa Uingereza wa Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko ili kumeza hasira za watu ambao Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko waliweza kuzidandia wimbi lake. Walikubaliana kuwahusisha Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko katika serikali lakini mara hii sio sawa na hapo awali, jeshi halikukabidhi serikali yote kama ilivyofanya wakati wa Sadiq al-Mahdi bali ilibakia kama kichwa chake kwa jina la Baraza la Ubwana na kushikilia vyeo na nafasi muhimu serikalini hata kama nguvu nyingine za ushawishi zilipewa serikali. Baraza la Ubwana ambalo laiongoza nchi nusu yake imejumuisha jeshi na inaongozwa na kamanda wa jeshi Al-Burhan kwa miezi 21 na mawaziri wa ulinzi na usalama wa ndani wamechaguliwa kutoka kwa jeshi ili kuhifadhi uongozi wa kijeshi na usalama wake.

5- Lipi linalotarajiwa? Amerika na Uingereza hawatokaa pamoja kwa utulivu. Maslahi yao ni tofauti na zana zao za mashinani zinafuata hivyo, kwa hiyo kila upande utafanyakazi ili kusitisha harakati za mwengine! Kwa kufuatilia matukio ya sasa, kuyasoma masuala yanayohusiana nayo na kutathmini kauli za kinje na kindani hususan maafisa wa Amerika na Uingereza tunaweza kufahamu njia ambazo kila upande utatumia ili kuhangaisha mpinzani wake na kuweza kumuondosha madarakani kama ifuatavyo:

Ama kuhusu timu ya kijeshi kwa makusudi itaihangaisha serikali kwa upande wa kiuchumi; moja katika sababu muhimu za harakati za watu dhidi ya Al-Bashir ilikuwa ni hali mbaya ya kiuchumi. Serikali ya sasa iliwaahidi watu kuboresha hali ya kiuchumi na lau itafeli basi hili litawafanya watu kuamka tena na itakuwa ni nafasi ya jeshi kuyaondosha Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko kwa maana kuondosha dori ya Ulaya ndani ya Sudan na vigezo vya udhibiti wa uchumi viko mikononi mwa Amerika kama ifuatavyo:

a- Hamdouk alisema katika kongamano la wanahabari pamoja na Waziri wa Kigeni wa Ujerumani:

(“Tatizo la kiuchumi la Sudan ni tatizo kubwa, suala la mfumko na ubadilishanaji wa sarafu ya kitaifa na kurudisha ujasiri kwa nidhamu ya benki,” na kuongeza: “Mpaka kuwepo na makubaliano na Wshington kuhusu kuiondosha Sudan kutoka katika orodha ya Ugaidi, kutakuwepo na uzito,” Anadolu, Reuters 3/9/2019, Hamdouk alisema: (“Kurudisha mawasiliano na Washington ni kipaombele chetu baada ya kuondosha vikwazo kwa kuanguka utawala wa zamani” Anadolu, 8/9/2019 na hivyo basi serikali inahitaji Amerika kuiondoshea vikwazo.

b- Amerika ilianza kwa kuitishia kwa kuwa na msimamo mgumu katika kuiondoshea vikwazo. Baada ya kusaini hati ya kikatiba ambayo vibaraka wake walilazimishwa kuisaini ili kutuliza mabarabara, Amerika ikaanza kurudi nyuma katika kuiunga mkono Sudan. Ubalozi wa Amerika ndani ya Khartoum ambao muhula wake uliisha, uliwajulisha watu maarufu wakuu ndani ya Sudan kwamba suala la kuiondoshea vikwazo Sudan halitosuluhishwa hivi karibuni kwa sababu uamuzi upo katika mikono ya Bunge na sio utawala wa Trump kwa mujibu wa Gazeti la Elaph lililochapishwa mnamo Jumatano  04/09/2019. Kwa maana Marekani ilikuwa na msimamo mgumu katika kutumia vikwazo kama kadi ya kuishinikiza serikali ya Hamdouk, licha ya kwamba Amerika ilimuahidi Al-Burhan tokea mwanzo kwamba ingeondosha vikwazo. Al-Burhan alisema wakati huo, (“Kuna muendelezo wa mikakati kuhusiana na faili ya vikwazo tangu utawala wa zamani, tumetumana wajuzi wa kisheria kujadiliana suala hili na utawala wa Amerika…Amerika imeahidi kuiondosha Sudan kutoka katika orodha ya dola zinazodhamini ugaidi baada ya kukamilika mchakato wa amani na tunaamini kwamba huu ni wakati mzuri. Alisema: “Makubaliano yanaweza kutiwa saini wikendi hii baada ya kuandika mswada wa Muundo wa Serikali ya Mpito”… Middle East 7/7/2019). Ubalozi wa Amerika ndani ya Khartoum Steven Koutsis mnamo 7/7/2019 aliweka wazi kwamba (suala la kuiondosha Sudan kutoka katika orodha ya dola zinazodhamini ugaidi ni lakutarajiwa… Gulf Online on 7/7/2019).

c- Taasisi za Kifedha za Kimataifa (IMF na World Bak) zinaweza kutoa mikopo kwa Sudan kwa idhini ya Amerika. Hii ni kadi nyingine ya shinikizo iliyomo katika mikono ya Amerika na timu yake ya ndani. Pia, kwa sababu Sudan imebakia katika orodha ya Marekani ya ugaidi, hii inainyima kuweza kutumia nidhamu ya malipo ya kimataifa ya Amerika ambayo ni kikwazo kikubwa kwa biashara za kimataifa za Sudan ambapo ufanyaji biashara unategemea dolari.

Ama kuhusu Ulaya na hivyo basi Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko, kwa hiyo inatarajiwa itafuata michoro miwili: kwanza, kutegemea kwa Ulaya kupambana na “suala la vikwazo na kuchelewesha kwa Amerika kuiondoshea vikwazo,” na kisha shinikizo la kiuchumi kama natija yake… Pili ni kuwahangaisha wanajeshi na vitengo vya usalama katika migao ya bajeti kifedha.

Kwanza, Ulaya “na hivyo basi Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko wanafahamu uzito wa athari ya vikwazo kwa uchumi wa Sudan, na pia wanazingatia kwamba Amerika itaendelea kuIshinikiza, hivyo basi itafanyakazi kuisadia serikali ya Sudan ndani ya Umoja wa Mataifa na kuipa msaada wa kifedha… Ujerumani imeandaa kuwasaidia; Waziri wa Kigeni Haikou Mas alisema (“nchi yake itazungumzia suala la kuiondosha Sudan kutoka katika orodha ya dola zinazodhamini ugaidi huko Baraza la Umoja wa Mataifa litakalofanyika mwezi huu”…Anadolu 8/9/2019). Waziri wa Kigeni wa Ufaransa (Le Drian) alizuru Khartoum mnamo 16/9/2019 na kukutana na Rais Abdullah Hamdouk na kusema: (“Nilimwambia Waziri wa Kigeni tutafanyakazi na washirika wetu wa Ulaya kuiondosha Sudan kutoka katika orodha ya Amerika ya dola zinazodhamini ugaidi” na kuongeza: “Ufaransa itaipa Sudan msaada wa ki- wango cha Uro milioni 60. Uro milioni 15 zitapeanwa mara moja kwa wakati huu,” ukurasa wa tovuti ya Sudanese Al-Rakouba 16/9/2019). Hii inaonyesha msaada kwa Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko na serikali ya Hamdouk.

La pili linajumuisha vitu viwili: kupunguza mgao wa bajeti kwa jeshi na kuleta mabadiliko katika huduma za usalama. Kauli ya Hamdouk inaashiria wazi hili:

Ama kuhusu bajeti, Hamdouk alitaka kuwepo na “kupunguzwa kukubwa katika matumizi ya jeshi… Akaongeza kwamba “matumizi ya jeshi yanachukua asilimia 80 ya bajeti ya dola” (Arabic Post 26/8/2019) akijadili kwamba kutiwa saini kwa makubaliano ya amani na harakati za kijeshi zilizosambaa nchini lazima “zirudi katika amani” kwa maana kuwa ili kupunguza matumizi ya kijeshi katika bajeti ya Sudan kwa jeshi na usalama.

Ama kuhusu mabadiliko katika huduma za usalama, muundo wa sasa wa huduma za usalama na jeshi ndani ya Sudan hususan hali ya Vikosi vya Msaada wa Haraka ambavyo viliundwa na utawala wa al-Bashir na vilitekeleza unyama mkubwa juu ya waandamanaji wa Sudan. Hivyo basi, kulikuwepo na uhalalishaji wa Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko kudai kubadilishwa kwa muundo wa vitengo hivyo ili kuhakikisha kuwa dola inavidhibiti na kwamba vifuate sheria, (Hamdouk alifichua kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka vitaunganishwa na huduma za usalama katika mchakato wa mageuzi ya muundo na kubuniwa kwa jeshi la kitaifa kwa ajili ya nchi. Aliongezea kwamba serikali yake iko makini kubadilisha muundo wa vitengo vya usalama ikijumuisha Msaada wa Haraka na majeshi ya harakati nyengine za kisilaha ili kuweza kujenga jeshi lenye nguvu la kitaifa. Al Jazeera Net 11/9/2019).

6- Inaonekana kwamba nafasi ya juhudi za Ulaya kutoa msaada kwa Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko yamefaulu kuchache kuliko yale ya Amerika na wafuasi wake kutokana na nukta zifuatazo:

– Ama kuhusu msaada wa Ulaya hausuluhishi tatizo lolote. Lau Amerika haitoiondosha Sudan katika orodha ya dola zinazodhamini ugaidi itaendelea kutaabika, kama alivyosema Waziri Mkuu mwenyewe. Inategemea msaada wa kigeni ambao ni msaada ulio na riba ambao unaendelea kuikandamiza nchi na wawekezaji na hauwezi kuleta mapinduzi ya kiviwanda na hauwezi kuleta maendeleo katika rasilimali za uchumi wake. Ni ya uhalisia ule ule wa ufisadi ambao uko mbali na mfumo na Dini ya kweli ya Ummah ambao nidhamu hupichuza kutoka kwayo, na ambayp itaifufua nchi. Mtazamo wa kiuchumi ndio sababu kubwa uliopelekea mapinduzi dhidi ya utawala wa Al-Bashir kwa kuwa watu wengi wanaangamia katika umasikini, kunyimwa, ukosefu wa ajira na bei za juu.

– Ama kuhusu kupunguza bajeti ya jeshi, jeshi kwa miongo mingi limekuwa likichukua mgao mkubwa wa bajeti ya Sudan na inatarajiwa kupinga vikali upunguzaji huo kwa njia tofauti tofauti ili kuhalalisha kuwepo kwa matumizi makubwa… Ama kuhusu ufisadi wa kifedha pande zote mbili hazijanusurika kwa hivyo nani kati yao atatatua suala hilo?! Ufisadi wa kifedha unasuluhishwa tu na wanaume wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kuongozwa na Uislamu katika hukmu zake zote sio chini ya nidhamu iliyowekwa na mwanadamu.

– Ama kuhusu huduma za usalama, Amerika imejifunga na mtu mmoja naye ni Mohammad Hamdan Dagalo (Himaidti), kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka ambaye amezidisha kauli zake na ziara zake hususan kuelekea Misri na Saudi Arabia. Inaonekana kwamba ndiye chaguo la Amerika la siku zijazo kwa Sudan, Himaidti, naibu mwenyekiti wa Baraza la Ubwana, atakuwa kipingamizi kwa mabadiliko katika Vikosi vya Msaada wa Haraka ambavyo kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vinajumuisha takribani asilimia 25 ya bajeti ya jeshi. Hivyo basi juhudi za serikali ya Hamdouk kuunda upya huduma za usalama ndani ya Sudan moja kwa moja zitagongana na mwanamume anayeungwa mkono na Amerika ndani ya Sudan, Himaidti!

7- Hivyo basi, hali ya kisiasa na kiuchumi ndani ya Sudan haitarajiwi kumakinika wakati wa muhula wa mpito:

– Ama utulivu wa kisiasa haupatikani ndani ya nchi kwa sharti kuna mzozo wa kimataifa ambao unachochewa na zana za kindani. Hili liko wazi kwa mabalozi wa harakati za kimataifa ndani ya Sudan na kutoka kwa kauli zao, vitendo vyao na mikutano yao na maafisa wa kindani kama ilivyo onyeshwa hapo juu. Hivyo basi utulivu hautopatikana na inawezekana ukosefu wa amani kupelekea mapinduzi ya kijeshi ndani ya muhula wa mpito kwa msaada wa Amerika labda watu wa Sudan watambue uhalisia huu na wampe nusra Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuondosha makafiri waliokoloniwa kutoka katika mizizi popote walipo na washirika wao… Na wasimamishe utawala wa Kiislamu, Khilafah Rashida (Khilafah iliyoongoka) kwa njia ya Utume. Watakuwa washindi na wataweza kuishi kwa usalama katika nyumba zao na kurudi kwa Mwenyezi Mungu kama walivyotarajiwa wawe:

خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ) ) “Umma bora walio tolewa watu” [Al-i-Imran: 110].

– Ama kuhusu ukosefu wa utulivu wa kiuchumi ni natija ya uingiliaji wa kikoloni ndani ya nchi, hauwezi kuvuna zabibu kutoka katika miba! Sudan Kusini imetenganishwa na utajiri wa mafuta umepotezwa kwa maagizo ya Amerika kwa mtawala aliyeusaliti Ummah katika hilo. Sudan, kama ilivyoelezewa kuwa ni kapu la chakula cha Afrika, watu wake wamekuwa masikini wa kupindukia kwa sababu ya kutegemea mikopo ya riba na ardhi zao zimekosa misaada kwa wakulima na kuwatafutia soko bidhaa zao kwa hivyo wakaachana nazo. Utajiri wa madini ukawachiwa uwekezaji wa kigeni na kuendelea hivyo… Na kisha la muhimu zaidi, Uislamu ukaondoshwa madarakani na nidhamu ya kiuchumi ndani ya Uislamu ikatelekezwa ambayo imewekwa na Mwenyezi Mungu (swt) na nidhamu fisadi ya wanadamu ikatelekezwa, itawezekanaje kupatikane utulivu wa kiuchumi? Bali kutakuwepo na maisha ya dhiki na Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al-Hakim, ndiye Msema kweli anayesema:

فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ ﴿١٢٣﴾ وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala  hatataabika* Na atakayejiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” [Ta-Ha: 123-124].

24 Muharram Al-Haram 1441 H

23/9/2019 M

Inatoka Jarida la Uqab: 34   http://hizb.or.tz/2019/11/01/uqab-34/

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!