Krismas Sio Yetu: Wao Wana Dini Yao, Nasi Tuna Dini Yetu

Siku ya Krismasi imeshawadia. Sikukuu iliyozushwa muda mrefu baada ya Nabii Issa As. Krismas iliasisiwa karne ya 313 AD na Mtawala Constatine wa Roma alipobatizwa kuwa mkiristo. www.history of christmass.net. Hakuna uhakika wa tarehe 25 Disemba kuwa ndio siku aliyozaliwa Issa As. Ndio maana Kanisa la Mashariki (Eastern Church) wao husheherekea Krismasi ndani ya Januari 6 ya kila mwaka badala ya tarehe 25 Disemba.

Krismasi kiasili ni mchanganyiko wa sherehe za kipagani za waroma kutoka sikukuu yao ya Saturnalia iliyochanganywa na ibada ya mafursi kwa mungu wao Mithra.

Waislamu ni haramu moja kwa moja (qatwii) kusherehekea sikukuu ya Krismasi. Iwe amma kumpa mkiristo kadi ya krismasi (Christmass card), mkono wa pongezi, kumtakia sikukuu njema (‘merry christ mass’), kutoa au kupokea zawadi, kuipamba nyumba au mahala pa kazi kwa alama za krismasi (sha’air) kama vile kuweka mti wa krismasi (christmass tree) kuigiza kwa kuvaa au kuwavalisha watoto mavazi ya Father Christmass nk. Kwa sababu, hayo ni kwa mkabala wa sikukuu ya kikafiri. Japo kwamba utaona zawadi ni kitu cha ‘mada’ (kushikika) lakini kwa munasaba huu kina mahusiano na fungamano la kifikra na kiitikadi na dini hiyo.

Ubepari/udemokrasia ambao ni mfumo wa kikafiri na mfumo wa kimaslahi unaipigia debe mno na kuitumia vyema kimaslahi Krismasi kwa kuonesha kwamba mfumo huo hauna ugomvi na dini, kuwapoza raia wao wapunguze joto la mfumo wa dhulma za kiuchumi na kisiasa unaowabana, kwa kuhamasisha ibada ya Krismas. Na pia kubwa zaidi kwa malengo na maslahi ya kibiashara na masoko ya bidhaa zao. Na kwa kuwa ubepari umepandikiza fikra ya hatari ya ‘pupa na uroho’ wa kila kitu (consumerism). Kiasi kwamba raia kama Marekani, nchi nyengine za kimagharibi na nchi zetu changa hujitumbukiza katika matumizi makubwa yasiyomithilika na mzigo wa  madeni yanayochukuwa muda mrefu kuyalipa kwa ajili ya matumizi ya krismasi, mapambo yake nk. Kwa mfano, matumizi ya siku zote za mapumziko (holidays)  nchini Marekani  huingiza kiasi cha $ 750 billioni, kati ya hizo $602.1 billioni hupatikana  katika kipindi  msimu wa Krismas (Novemba na Disemba).

Jambo jengine la hatari makafiri huitumia Krismasi na sherehe nyengine za kikafiri kama ‘Pasaka’ kama mbinu ya kuleta ‘ukuruba baina ya Uislamu na Ukiristo’, pamoja na jamii za wafuasi wa dini mbili hizi. Kwa kusisitiza kauli za ‘kuishi pamoja’, ‘maelewano’ na ‘mashirikiano ya kidugu’ kwa kudai ati dini zote zinatoka kwa Mungu, na zaidi hudai dini zote hizi mbili zinatokana na chimbuko la Ibrahim As.

Fikra hii ni fikra ya kikafiri, hatari na haramu. Na kimsingi inatudhuru Waislamu kwa kuwa dini yetu ndio ya haqi. Tunasema hakuna ukuruba baina ya haqi na batil, wala baina ya Uislamu na ukafiri kwa namna yoyote. Na Waislamu ni wajibu kujiepusha mbali na fikra na mtazamo huu na kuupiga vita kwa nguvu zote za kifikra.

Badala yake  kwa kuwa Waislamu ni Ummah bora wenye mfumo wa haqi  wa kilimwengu unaokubaliana na maumbile, tunapaswa kuijadili krismasi na kuchemsha mjadala kwa ukiristo na wakiristo ili kuwalingania na kuwavuta kuja katika Uislamu kwa kutumia hoja za kiakili. Na lau hawatokubali kusilimu, basi angalau waufahamu Uislamu kwa uadilifiu, kinyume na wanavyooneshwa na makafiri wa magharibi kutokana na uadui wao kuwa ni dini ya uadui na ya kigaidi.

#UislamuNiUfumbuziSahihi

28  Rab’i al Thani 1441 Hijri    | 25 -12- 2019 Miladi

Afisi ya Habari –   Hizb ut- Tahrir Tanzania

http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!