Kampeni ya Miezi Sita ya Uchumi: Hizb ut-Tahrir Tanzania

Utangulizi.
Tatizo la uchumi ni suala linalogusa kila mahala mashariki na magharibi, iwe katika ulimwengu wa Kiislamu au nchi nyenginezo. Kimsingi ni ukweli usiopingika kwamba sehemu kubwa ya maisha ya wanadamu hujihusisha na masuala ya kiuchumi, iwe ajira, biashara, kukodishana, ushirika wa kampuni nk.

Uislamu umetoa mielekeo mitatu msingi katika kulitupia macho suala la kiuchumi, nayo ni :
a. Kutukuzwa kwa mwanadamu ( kaumbwa kwa ajili ya kunufaika na rasilimali)
b. Kuwepo rasilimali za kutosha
c. Ulazima wa kuwepo muongozo thabiti kutoka kwa Muumba utakaosimamia miamala ya kiuchumi kwa kupitia chombo cha usimamizi nacho ni dola ya Khilafah Rashidah.

Uzinduzi wa Kampeni
Umefanywa rasmi leo tarehe 03 Januari 2020 (baada ya Ijumaa) katika Masjid Rahma , Buguruni Dar es Salaam, ambapo kwa kipindi chote cha miezi sita wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Tanzania watajikita kwa undani na kampeni hii muhimu kuhusu uchumi.

Lengo kuu la Kampeni :
Kujenga ufahamu kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu kuhusu dhana nzima ya uchumi, tatizo msingi la kiuchumi ulimwenguni na suluhisho lake msingi.

Lengo haswa:
Kufafanua kwa kina mada mbalimbali za kiuchumi zinazohusisha miamala binafsi, miamala ya kiwango cha dola, ikiwemo unyonyaji wa kiuchumi unaotendewa nchi changa kupitia taasisi za kinyonyaji za kimataifa.

Mbinu za kampeni
• Semina na Warsha
• Bayan Misikitini
• Ujumbe za wiki na vipeperushi
• Vipindi katika vyombo habari. TV, redio nk.
• Clips za Audio na Video
• Maongezi mubashara ndani ya mitandao ya jamii, kama
facebook nk.
• Matumizi jumla ya mitandao ya kijamii mf. fbook,
twitter, instagram nk.
• Mihadhara
• Darasa za misikitini
• Khutbah za Ijumaa
• Semina nk.

Mwito kwa wote
Kushiriki katika kuchangia, kutoa maoni na kuifanikisha kampeni hii ili ifikie lengo la kukuza upeo wa ufahamu kwa jamii juu ya tatizo msingi la kiuchumi na suluhisho
lake.
#UislamuNdioUfumbuziSahihi

04 Januari 2020 Miladi
09 Jumadu al-awwal 1441 Hijri

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Bonyeza picha kuona uzinduzi kwa video:

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!