Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: “Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia… inafuatiwa na Bishara Njema!”

بسم الله الرحمن الرحيم

Kampeni Pana ya Kiulimwengu kwa Anwani:

   Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia… na Bishara Nyengine Njema Zinafuatia!

          Kwa muongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah,(Allah Sw Amlinde), Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio adhimu la Ukombozi wa Konstantinopoli (mji wa Heraclius) ambao kwa mujibu wa  kalenda ya Hijria  ulizingirwa kuanzia mnamo 26 Rabii’ al-Awwal mpaka 20 Jumada al-Awwal 857 H (5 Aprili- 29 Mei 1453 M) na hivyo bishara njema ya Hadith tukufu ya Nabii (saw) ikatimia

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

 “Mutaifungua Konstantinopoli, mbora wa Amiri, ni amiri wake, na ubora wa jeshi, ni jeshi hilo.”

Sisi Hizb ut Tahrir tumezindua kampeni ya kiulimwengu kwa sababu tatu:

Kwanza: Kurejesha kumbukumbukizi hizi ili kila mwenye macho mawili aone ulivyo utukufu wa Uislamu na Waislamu, unapowekwa Uislamu wao kwenye nafasi ya utabikishaji,  wakati huo ukafiri unakuwa hauwezi kusimama, bali haki huwa juu na kunyanyuka mnyanyuko wa adhana (Allahu Akbar), na hakika ilikua hivyo, Fursi na Bayzantine zikanyenyekea mbele yake na karibu itazifuata hizo ndugu wa Byzantine ambae ni Rome Inshallah, kusadikisha sehemu nyengine ya bishara ya Mtume (SAW) kwa ukombozi wa Rome…

 Pili: Ili nyoyo zenu zipate kutulia kwa kuzihakikisha bishara nyengine tatu za Mtume (SAW), kama ilivyofikiwa bishara ya kwanza, hakika ametubashiria rehema na amani ziwe juu yake ukombozi wa Constantinople , ukombozi wa Rome, kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Utume , kupigwa kwa Mayahudi na kushindwa kwao vibaya mno…  Na Mtume (SAW) hatamki kwa matamanio yake, hayakuwa anayoyatamka ila ni Wahyi. Na zitafikiwa bishara tatu za Mtume (SAW) zilizobakia kwa idhini ya Allah Aliyetakasika. Lakini hazitofikiwa kwa kuteremka Malaika kutoka mbinguni ili watupe sisi, bali hakika ya utaratibu wa Allah SW ni kuwa tumnusuru Yeye naye atupe ushindi sisi, kwa hiyo tusimamishe sharia yake na tunyanyue ukubwa wa Dola yake na tutayarishe nguvu tunazoweza kisha tupigane jihadi katika njia yake. Na wakati huo ardhi itang’aa kwa bishara tatu zilizobakia, na ardhi itang’aa upya kwa Khilafah…

 Tatu: Hakika wamagharibi makafiri wameweza pamoja na makhaini waarabu na waturuki kuivunja Khilafah katika 1342H /1924 AD na kuchukulia kuangusha huku ni sawa na ukombozi wa Constantinople na hapo makafiri wamagharibi wakarejesha nguvu waliyoikosa. Na hima ya wamagharibi imekuwa ni kutumia juhudi katika kutorejea Khilafah upya, ili nguvu waliyoirejesha isijepotea, na hasa kwa kuwa wamekuwa ndio wakoloni wa miji ya Waislamu. Na wamekuwa wanafuatilia harakati katika biladi za  Waislamu. Na wakati kulipotangazwa kuasisiwa kwa Hizb ut Tahrir mwaka 1372H/ 1953AD na ikabainika kwa wamagharibi kuwa lengo la amali ya Hizb na kadhia yake nyeti (mtambuka) ni kurejesha upya Khilafah, na kwamba iko makini hasa (serious) katika amali yake hii, basi wamagharibi wakawaamrisha vibaraka wao ambao ni watawala kuizuiya Hizb na kuwatia ndani na kuwaadhibu wanachama wake hadi kufikia kuuawa katika baadhi ya maeneo, kisha (pia) kwa kuwahukumu vifungo virefu hadi vya maisha katika baadhi ya maeneo… Kisha wakazidisha kwa mbinu za uongo, kuwazulia uongo na kubadilisha mambo bila haya wala aibu

Kwa hivyo, juu ya kwamba mbinu za kupamba uzushi walizozitumia, na ijapokuwa kutengeneza uzuri katika kubadili ukweli wa mambo, mambo yaliwachosha wenyewe katika kuyatengeneza, ila hakika mambo hayo hayakupata usikivu kwa mashababu wa Hizb wala kwa mwenye akili yeyote yule katika Waislamu. Bali yalikuwa:

﴿كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئاً﴾،

“Kama mangati njiani ambayo mwenye kiu huyadhania maji mpaka anapoyafikia hakuti kitu” [Nur: 39].

Na pamoja na vitimbwi vyote walivyovifanya na uovu waliouunda na matendo yao mabaya kwa Hizb na uongozi wake wakidhania miongoni mwao kwamba wataiathiri Hizb, hakika dhana yao imekuwa yenye kuwarejea wenyewe, kisha kwa idhini ya Allah watakuwa wenye kushindwa hawatafikia kheri kwa hali yoyote ile hata ukirefuka uongo wao, mbinu zao na vitimbwi vyao.

﴿وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ﴾،

“Na havimstahikii vitimbwi viovu isipokuwa mwenye” [Fatir: 42].

Na watayakuta mwisho wake hayo mbele ya Allah SW hata uzushi wao na vitimbwi vyao vikiwa vikubwa kiasi gani:

﴿وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ﴾.

Na hakika walifanya vitimbwi vyao, na vitimbwi vyao hivyo mbele ya Allah (ndiko vitamalizia) hata vikiwa vitimbwi vyao vinaondosha milima” [Ibrahim; 46]

Na mwisho wa yote, nanyenyekea kwa Allah (SWT) afuatishe kufikiwa kwa bishara za Mtume (SAW) irejee Khilafah ya ummah huu, kisha ikombolewe Quds yake, na kisha ikombolewe Rome kama ilivyotangulia ndugu yake na ikawa… Kusadikisha ukweli wa Hadithi za Mtume (SAW) … Kama ambavyo tunamuomba Allah (SWT) Atupe msaada kutoka kwake ili tufanye amali ya da’wa vizuri na kwa usafi wake ili tuwe tunastahiki nusra ya Allah Al-Aziz, Al- Rahiym.

﴿وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴾.

“ Na siku hiyo watafurahi  Waumini. Kwa nusra ya Allah humnusuru amtakae naye ni Mwenye kushinda Mwenye kurehemu” [Rum: 4-5]

Ijumaa, 8 Jumada Al-Awwal 1441 AH – 3 Januari 2020 CE

#ﻓﺘﺢ_ﺍﻟﻘﺴﻄﻨﻄﻨﻴﺔ
#ﺍﻟﻘﺴﻄﻨﻄﻴﻨﻴﺔ
#ConquestofIstanbul
#İstanbulunFethi
#istanbul

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!