Amali za Kiulimwengu za Hizb ut Tahrir Katika Kukumbuka Kuanguka kwa Khilafah 1441 H – 2020 M

بسم الله الرحمن الرحيم

Katika mwezi wa Rajab al-Muharram wa Mwaka huu 1441 H sawia na 2020M na katika kukumbuka kwa majonzi namna wahalifu walivyoivunja Dola ya Kiislamu na kuuondosha utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo 28 Rajab al-Muharram 1342 H sawia na 3 Machi 1924 M. Hizb ut Tahrir imeandaa amali za wazi ndani ya maeneo inayofanyakazi. Sisi Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tutakuwa na upeperushaji maalumu wa matukio na amali zote na twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kutuharakishia kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya hili. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

)وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ(

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur:55]

Ijumaa, 11 Rajab al-Muharram 1441 H sawia na 06 Machi 2020 M

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!