Fadhila na Ihsani Zisitumike Vibaya

بسم الله الرحمن الرحيم

Fadhila na ihsani lazima ziangaliwe katika sura yake kimakini, kwa sababu zinaweza kutumika na wanasiasa kama kisingizio, guo na kinga yakufunika dhulma na madhila mapana ya walio wengi yaliyotendwa au yanayotendwa na mwenye kutoa fadhila na ihsani hizo ambazo zikilinganishwa na madhila yaliyotendwa au yanayotendwa ni masafa ya mbingu na ardhi.
Firaun (laana ya Allah Sw imshukie) alitaka kuitumia ihsani na fadhila ya kumlea Nabii Mussa As. kuwa kinga yake ya dhulma na kitu cha kuhalalisha kuendelea kuwakandamiza na kuwafanya watumwa Bani Israil, lakini Nabii Mussa As. alipangua hoja za Fir-aun, na mjadala ukawa kama hivi:
قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ (الشعراء: 18
‘Akasema (Firauni) Jee hatukukulea wewe (Mussa) utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi?’
وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنْتَ مِنْ الْكَافِرِينَ (الشعراء: 19
‘Na ukatenda kitendo chako ulichotenda (kumuua mtu) ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?’
قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنْ الضَّالِّين (الشعراء: 20
‘(Mussa) akasema: Niliyatenda hayo hapo nilipokuwa miongoni mwa wale waliopotea.’
وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدْتَ بَنِي إِسْرَائِيلَ (الشعراء: 22
‘(Akasema Mussa) na hiyo ndio neema ya kunisumbulia na kuwatia Bani Israil utumwani ?’
Masoud Msellem
Tuendelee kutetea mahabusu

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!