Saturday, 27 May 2017 00:00

Enyi Watu wa Sudan: Marekani ni Adui wa Uislamu na Waislamu ! Basi Ondosheni Athari yake ndani ya Ardhi hii ya Waislamu

Kumb: 1438/44 HTS

25 Sha’aban 1438 H                                22 Mei 2017

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu wa Sudan: Marekani ni Adui wa Uislamu na Waislamu ! Basi Ondosheni Athari yake ndani ya Ardhi hii ya Waislamu

Raisi wa Sudan Omar Al-Bashir alijitia kisingizio cha kutohudhuria Mkutano wa Marekani pamoja na Nchi za Kiislamu mjini Riyadh. Na badala yake akamteua Mkurugenzi wa Afisi yake na Waziri wa Nchi kumuwakilisha katika mkutano huo, hayo ni baada ya Marekani kubainisha wazi kwamba Raisi Trump hamtaki Al-Bashir kushiriki mkutano huo, na Saudia ikamsisitiza Al-Bashir kuwa  asishiriki mkutano huo uliofanyika Jumamosi. (Sudan Tribune, 19/5/2017). Kisingizio cha Raisi Al-Bashir kilikuja siku chache baada ya Ubalozi wa Marekani kutoa taarifa yake iliyotangazwa Jumatano 17/05/2017 ambayo ilitamka…..”tunapinga kupewa mwaliko, msaada au kuunga mkono kusafiri (kushiriki mkutano) kwa mtu yoyote ambae kumetolewa nyaraka ya kukamatwa/arrest warrants kwake na Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)”

Kufuatia qadhia hiyo, sisi Hizb ut-Taharir Wilaya ya Sudan tunapenda kusisitiza kwa mara nyengine tena yafuatayo:

Huu ndio uhalisia na ukweli kuhusu Marekani, ni adui wa Uislamu na Waislamu,  na ni nchi iliyopo katika uwanja wa medani ya kivita (kivitendo) na Umma wetu. Haiheshimu rafiki yake wala adui yake. Allah swt amekwisha tudhihirishia namna walivyo makafiri na kufedhehi mtazamo wao kwa Waislamu. Wanaaamiliana na kuwaona Waislamu kwa jicho la  kuwadhalilisha na kuwadharau.  Na uoni wao huo haotobadilika mpaka Waislamu waikatae kabisa imani yao kwa  Sharia ya Allah Taala. Na hili ndilo alilolisema Allah Taala :

وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنْ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنْ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنْ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ (البقرة:

“Hawatakuwa radhi juu yako Mayaudi wala Manasara, mpaka ufuate mila  yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio  yao baada ya ujuzi uliokwishakujia, hutapata mlinzi wala msaidizi mbele ya Mwenyezi Mungu” [ TMQ Al-Baqarah: 120]

Licha ya serikali ya Sudan kujipendekeza na kuifurahisha Marekani kwa kutenda mengi ili kuiridhisha ikiwemo kuimega Sudan vipande kwa mgao wa Sudan ya Kusini na ya Kaskazini, kubadilisha sheria ili kuwafikiana na matakwa ya Marekani na Sheria za Kimataifa na kanuni zake, kushiriki katika vita dhidi ya Uislamu kwa  kwa jina la vita dhidi ya ugaidi na kufungua milango ya Sudan kwa Ujasusi wa Marekani na makachero wake,  kwa yote haya bado Marekani haiko radhi nasi. Sasa Marekani inadiriki kumfedhehi raisi wa nchi Al-Bashir bila ya haya (japo mkutano wenyewe ni batil Kiislamu).

Msimamo thabiti baada ya haya lazima uwe ni kutokana na Sharia ya Kiislamu  nao ni kukata kamba zote za Marekani, kuondoa athari yake ndani ya Sudan, kufunga ubalozi wake – yaani, ngome ya usaliti na ujasusi dhidi ya Sudan, na kung’oa harakati zake za kiulinzi ziondolewe mara moja kutoka katika ardhi yetu badala ya kuzisaidia. Na badala yake Khilafah kwa manhaj ya Utume ishike hatamu mara moja. Haya ndio ambayo daima Hizb ut-Tahrir imekuwa ikiyasema tena na tena kwa Waislamu mara zote, kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa viongozi na wanasiasa ndani ya Sudan wamo katika ndoto na madhania kuwa Marekani italinda viti vyao  vya enzi na vya utawala ambavyo miguu yake imeshateteruka. Lakini wapi! hilo haliwezekani kamwe kwa Marekani !!!! Marekani inachojali ni maslahi yake tu, na ukishakumfanyia malengo yake hukuchoka na hukutupilia mbali!

Enyi watu wa Sudan, kwa kukhitimisha tambueni hakuna tembe ya kheri kutoka kwa dola ya Marekani, kama Allah Tala alivyosema:

مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلاَ الْمُشْرِكِينَ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْكُمْ مِنْ خَيْرٍ مِنْ رَبِّكُمْ

“Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu…..”[TMQ Al-Baqarah: 105].

Tambueni kuwa ni kwa dola ya Kiislamu ya Khilafah pekee kwayo ndio mtarejesha hadhi na izza/nguvu zenu. Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ni utawala ulioahidiwa na Allah Taala na kubashiriwa na Mbora wa wakweli nae ni Mtume SAAW, basi fanyeni kazi kuirejesha.

Allah Taala anasema:

﴿وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لا يَعْلَمُونَ

“…..Na Mwenyezi Mungu ndie Yeye ndie Mwenye utukufu,na Mtume wake na Waumini. Lakini wanafiki hawajui”

 (TMQ Al-Munafiqoun: 8)

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi  wa Hizb ut Tahrir
Wilayah Sudan

Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.      Tovuti &Anuani    Tel: 0912240143- 0912377707           http ://www. Hizb-sudan.org

 

Read 405 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…