Saturday, 27 May 2017 00:00

Tunawapongeza Umma wa kiisalam kwa kuingia Ramadhani

Tunawapongeza Ummah wa kiislam kwa kuingia Ramadhani

Baada ya mwezi kuonekana sehemu mbali mbali ulimwenguni na kuthibitishwa, Alhamdullilah ! tumeanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania Tunawapongeza Waislamu wote kwa kuanza Ramadhani mwezi uliosheheni kila kheri.
Tunawakumbusha Waislamu kujifunga kibwebwe katika ibada mbalimbali kujikurubisha zaidi na Muumba.
Aidha, tunakumbusha kwa wenye uwezo kuwasaidia wanyonge na madhaifu. Kwa kuwa Umma wetu na wanadamu kwa jumla unapita katika kipindi kigumu katika kila hali.

Tunamuomba Allah atupe tawfiq ya kufunga na kufanya ibada mbali mbali na kuzipata fadhila za mwezi huu mtukufu.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Read 310 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…