Tuesday, 16 May 2017 00:00

Tofauti baina ya ubinafsishaji, utaifishaji na iqta’ (umilikishaji ardhi)

Swali:

Asalamu Alaikum WA Rahmatulah Wa BarakatuhNi ipi tofauti baina ya ubinafsishaji katika mfumo wa kirasilimali (Ubepari) na Iqta’ (umilikishaji ardhi) katika Uislam kama ilivyo elezwa katika kitabu Hazina katika Dola ya Khilafah

 

Jawabu:

Wa Alaikum As-Salam Wa Rahmatulah Wa Barakatuhu,

  • Umiliki upo wa namna tatu. Umiliki wa ummah, umiliki wa dola na umiliki binafsi- ambao ni kila kisichokuwa katika imma umiliki wa dola au umiliki wa ummah.
  • Mali ya ummah ni ile ambayo Muweka sharia ameitaja kuwa umiliki wake ni wa waislam wote, ambao ni umiliki wa pamoja. Mali hii Ameiharamisha kumilikiwa na mtu binafsi. Miongoni mwa mali hizi ni; Vinu vya kufulia umeme, Mitambo ya umeme kama bwawa , viwanda vya kuzalisha gesi, makaa ya mawe, na madini yanayo patikana kwa wingi na yasiyo koma. Yawe ima katika hali ya ugumu kama dhahabu na chuma au kimiminika kama mafuta na gesi. Na vingine vyote mfano wa hivi ni milki ya ummah wa kiislam, umiliki wa shirika, na mali hii ni chanzo pia cha hazina ya dola (Bait-ul maal ya waislam). Khalifah ndiye hugawanya kwa raia mali hii akizingatia hukmu za kisheria.

 

  • Mali milki ya dola. Hii ni kila ardhi au jengo lenye mahusiano na haki za waislam wote; Hii ni tofauti kabisa na Mali milki ya ummah. Mali milki ya Dola ni pamoja na ardhi, mali inayo hamishika ambayo kihukmu za kisheria ina husianishwa moja kwa moja na haki za waislam jumla. Khalifah ana mamlaka ya kusimamia , kuratibu na kutolea maamuzi mali husika.

Japokuwa Dola husimamia mali  ambayo ni milki ya Ummah, na pia husimamia mali ambayo ni milki ya Dola, kuna utofauti wa kisheria katika umiliki huu. Mali milki yote iliyo chini ya Ummah kama vile mafuta, gesi , na madini mengi, bahari, mito, chem chem., mapori, mbuga za malisho na misikiti, sio ruhusa kwa Khalifah kuamua kuipatia umiliki kwa yeyote. , iwe ni mtu mmoja mmoja au kundi; kwa sababu ni milki ya waislam wote kwa jumla.

Kwa ile inayoitwa mali ambayo ni milki ya Dola ikiwemo ardhi na majengo, hii ni ruhsa kwa Khalifah kumpatia umiliki mtu binafsi ambapo humiliki na manufaa, au manufaa pasi na umiliki kimsingi, au aweza kuamuru ifufuliwe na kumilikiwa, au pia anaweza kuitoa katika namna ambayo anaona ni maslahi kwa waislam.  

Khalifah ameruhusiwa kumpatia sehemu ya ardhi milki ya dola muislam yeyote ambaye hana ardhi ya kilimo. Mtuhuyu aweza kuilima na kuimiliki, hivyo mali sio tu kwamba itakuwa kwa matajiri bali hata masikini nao watakuwa nayo, yaani izunguke:

كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ

“ili yasiwe(mali hayo) yakizunguka kati ya matajiri tu miongoni mwenu”

(Al-Hashr: 7)

Aidha Khalifah hana haki ya kuchukua kutoka katika mali ya millki binafsi pasi na sheria na kumpatia mwingine, ila anaweza kuchukua kutoka mali ambayo ni milki ya Dola na kuwagawia masikini na wala sio matajiri; kunakoitwa kumilikisha ardhi.

Iqta’ (umilikishaji wa ardhi) ni ile ruhsa ya Khalifah kuweza kummilikisha sehemu ya ardhi muislam yeyote atakaye ona anahitaji, ardhi hii huchukuliwa kutoka katika mali ambayo ni milki ya Dola wala sio kutoka katika mali ambayo ni milki ya ummah.

Hukmu ya kisheria imefafanua hali za mali hizi, hairuhusiwi kamwe  kubadilisha ufafanuzi huu wa kimgawanyo. Hivyo mali ambayo ni milki ya ummah haiwezi kubadilishwa na kuwa mali ambayo ni  milki ya binafsi, kama vile kubinafsisha uchimbaji mafuta na madini kwa kummilikisha mtu binafsi au kampumi binafsi. Kadhalika haifai katika hukmu za kisheria kutaifisha mali ambayo ni milki binafsi kuwa mali  ambayo ni milki ya Dola, kama kutumia nguvu kuchukua duka la mtu na kulifanya ni mali ya Dola, ambao ndio utaifishaji.

Kutokana na maelezo yaliyo tangulia, imekuwa wazi tofauti baina ya ubinafsishaji, utaifishaji na Iqta (umilikishaji kwa kubadili sifa ya mali milki). Ubinafsishaji ni kitendo cha kuuza mali ambayo ni milki ya ummaha kwa mtu au kampuni binafsi, kama kukabidhi uchimbaji madini, ufuaji umeme au uchimbaji mafuta kwa wamiliki binafsi, jambo hili ni haram. Sheria inataka mali ambayo ni milki ya ummah ibaki kuwa hivyo na isifanywe ni mali ambayo ni milki ya binafsi. Utaifishaji ni hali ya kubadilisha mali ambayo ni milki ya kibinafsi kuwa mali amabyo ni milki ya Dola au mali ambayo ni milki ya ummah. Mfano nikama kubadili duka la mtu binafsi na kulifanya kuwa ni   mali milki ya ummah au mali ambayo ni milki ya Dola, hali hii pia ni haram kwani sheria inataka sifa ya umiliki wa mali iwe  kwa mmiliki wa kiasili, na hakuna ruhusa ya kubadili  haki hii akapewa asiye husika.

Nakuhusu Iqta’ nipale Dola inapo gawa mali ambayo ni milki yake kwa mmiliki binafsi ili kuinua hali zao za kiuchumi na Dola haifai kuacha mali na utajiri ukizunguka tu kwa matajiri hali yakuwa watu walio wengi hawamiliki cha kuwatosha kuendesha maisha yao kwa amani na heshima, hivyo Dola huwapatia wale ambao hawana ardhi ya kulima, pia huwapatia pembejeo wakulima kutoka katika hazina yake na kuwasaidia ukulima.

Kwahiyo, katika ufahamu wa kifiqhi ya kiislam Iqta’ ni tofauti kabisa na Utaifishaji na Ubinafsishaji.

 Ni Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

 

Imewekwa katika Kiswahili na

Hamza Sheshe

Read 477 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…