Wednesday, 17 May 2017 00:00

Bida'a ni nini na ipi hukmu yake

Swali

Assalaamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakaatuhu,

Namuomba Amir anijibu swali langu ambalo ni muhimu sana. Bid’a ni nini na nni adhabu/ hukmu yake? Na kuna tofauti gani baina ya Bid’a na “anaye anzisha jambo zuri”?

Je katika matendo ya Mtume saw katika masuala yanayo tazamwa kama dalili za Kisheria ambayo ni sahihi na kufaa kurejelewa?. Huwa ninakuwa na mijadala na makundi kadhaa na huwa huyaita baadhi ya masuala kuwa ni bid’a kwakuwa hayakufanywa na Myume saw. Swali hili ni muhimu sana, Baraka za Allah sw ziwe nawe Kutoka kwa: Radhwan Yusuf

 

Jawabu:

Wa Alaikum Assalaam Wa Rahmatullah Wa Barakaatuhu,

Siku za nyuma tulisha toa jawabu juu ya swali linalo husiana na habari za Bid’ah, ilikuwa ni 18/9/2009, na jawabu hilo tulilichapisha kama jawabu la swali la miongoni mwa ndugu zetu wanao patikana katika Facebook, nayo ilikuwa 6/6/2015, hivyo unaweza kurejea. Hatahivyo nita leta jibu japo kwa kufupisha kwa ajili yako katika namna ambayo itakinaisha kujibu swali lako in shaa Allah:

  • Bid’a ni kukengeuka amri ya mteremsha sheria ambayo utekelezaji wake umeshawekwa wazi, maana hii inashabihiana na inayopatikana katika Hadith;

«وَمَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ»

“Yeyote ambaye atatenda kitendo kinyume na maelekezo yangu, kitakataliwa” [Bukhari and Muslim]

Kwahivyo iwapo Mtume saw amefanya kitendo ambacho huonesha ni namna gani jambo hilo lapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa Kitabu na Sunnah na halafu mtu akakitendakitendo hiki kinyume na namna aliyo elezea Mtume saw, basi atakuwa ametenda Bid’a na ni upotevu (Dhalla) unaopelekea katika dhambi kubwa.

Kwa mfano: Allah سبحانه وتعالى anasema: وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ“Na simamisheni swala” [Al-Baqara: 43] Ambayo ipo katika mtindo wa amri, lakini Yeye سبحانه وتعالى hakuiacha amrihii katika uhuru wa binadam kuswali namna atakavyo, ila Mtume saw akaelezea njia ya utekelezaji wake katika matendo yake ya Ihram, qiyyam, Kisomo, ruku’u’, na kusujudu.

Abu Daoud ameipata kutoka kwa Ali Bin Yahya Bin Khalad aliye pokea kutoka kwa mjomba wake:

«فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ إِنَّهُ لَا تَتِمُّ صَلَاةٌ لِأَحَدٍ مِنَ النَّاسِ حَتَّى يَتَوَضَّأَ، فَيَضَعَ الْوُضُوءَ – يَعْنِي مَوَاضِعَهُ – ثُمَّ يُكَبِّرُ، وَيَحْمَدُ اللَّهَ جَلَّ وَعَزَّ، وَيُثْنِي عَلَيْهِ، وَيَقْرَأُ بِمَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ، ثُمَّ يَقُولُ: اللَّهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ يَرْكَعُ حَتَّى تَطْمَئِنَّ مَفَاصِلُهُ، ثُمَّ يَقُولُ: سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَائِمًا، ثُمَّ يَقُولُ: اللَّهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ يَسْجُدُ حَتَّى تَطْمَئِنَّ مَفَاصِلُهُ، ثُمَّ يَقُولُ: اللَّهُ أَكْبَرُ، وَيَرْفَعُ رَأْسَهُ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَاعِدًا، ثُمَّ يَقُولُ: اللَّهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ يَسْجُدُ حَتَّى تَطْمَئِنَّ مَفَاصِلُهُ، ثُمَّ يَرْفَعُ رَأْسَهُ فَيُكَبِّرُ»

“Mtume saw amesema, swala ya mtu haitatimia mpaka apate udhu na kutimiza vipengele vyake vyote, kisha alete takbeer, na amhimid Allah Azza Wa Jal, na amtukuze, na halafu asome kilianachokiweza kutoka katika Qur’an halafu lazima aseme: Allahu Akabar, alafu arukuu mpaka viungo vyake view vimetulia imara, kisha lazima aseme: Sami’a Allahu Liman Hamida, alafu anarejea kusimama wima  na aseme: Allahu Akbar, kisha asujudu mpaka viungo vyake vitulie imara, kisha aseme, Allahu Akbar na kuinua kichwa chake na kukaa kitako, kisha aseme: Allahu Akbar, alafu asujudu mpaka viungo vyake vitulie imara, kisha huinua kichwa chake na kuleta Takbeer”.

Yeyote atakaye kwenda kinyume na njia hii katika kuswali atakuwa ameleta Bid’a; mathalan, iwapo mtu ata sujudu mara tatu badala ya mbili, atakuwa ameleta Bid’a ambayo ni upotevu.

Kwa mfano Allah سبحانه وتعالى anasema:

(وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ)

“Na [ni kwa ajili] ya Allah watu kwenda hija katika  Nyumba (tukufu)” [Al-i-Imran: 97]

Hii ni amri ya ibada ya Hija. “inaelezea maana ya hitajio” , na Mtume saw njia (namna) ya kutekeleza ibada hii ya Hija…

Imenukuliwa na Imam Bukhar kutoka kwa Az-Zahri:

«أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ كَانَ إِذَا رَمَى الجَمْرَةَ الَّتِي تَلِي مَسْجِدَ مِنًى يَرْمِيهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ، يُكَبِّرُ كُلَّمَا رَمَى بِحَصَاةٍ، ثُمَّ تَقَدَّمَ أَمَامَهَا، فَوَقَفَ مُسْتَقْبِلَ القِبْلَةِ، رَافِعًا يَدَيْهِ يَدْعُو، وَكَانَ يُطِيلُ الوُقُوفَ، ثُمَّ يَأْتِي الجَمْرَةَ الثَّانِيَةَ، فَيَرْمِيهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ، يُكَبِّرُ كُلَّمَا رَمَى بِحَصَاةٍ، ثُمَّ يَنْحَدِرُ ذَاتَ اليَسَارِ، مِمَّا يَلِي الوَادِيَ، فَيَقِفُ مُسْتَقْبِلَ القِبْلَةِ رَافِعًا يَدَيْهِ يَدْعُو، وَكَانَ يُطِيلُ الوُقُوفَ، ثُمَّ يَأْتِي الجَمْرَةَ الَّتِي عِنْدَ العَقَبَةِ فَيَرْمِيهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ، يُكَبِّرُ عِنْدَ كُلِّ حَصَاةٍ، ثُمَّ يَنْصَرِفُ وَلاَ يَقِفُ عِنْدَهَا»

“Pindi Mtume saw alipo tupa vijiwe (katika Jamra) ambayo ipo jirani baada ya  Mina, alifanya hivyo kwa kutumia vijiwe saba vidogo huku akitamka Takbir kila alipotupa kijiwe, kisha alikwenda mbele yake na na kusimama kuelekea Qibla, akainua mikono yake juu akiomba dua, na alikuwa akisimama kwa muda mrefu , kisha aliendea Jamra ya pili  na akalirushia vijiwe saba huku akitamka Takbeer kwa kila kijiwe anachorusha, kisha akaenda kushoto nyuma ya bonde akasimama kuelekea kibla na kuinua mikono yake juu na kuomba dua, alikuwa akisimama kwa muda mrefu, kisha akaenda katika Jamra ya Aqaba napo akarusha  vijiwe saba vidogo huku akitamka Takbeer kila aliporusha kijiwe, kisha akaondoka bila kusimama pale.”

Yeyote atakayetenda kinyume na utaratibu huu katika hija, kwa mfano akatupa vijiwe nane badala ya vijiwe saba  atakuwa ametenda Bid’a.

Hakika matendo mengi ya ibadat yameleekezwa kwa vitendo vya Mtume saw, hivyo basi yeyote atakaye tenda kinyume na matendo ya Mtume saw atakuwa ametenda Bid’a ambayo hukmu yake ni upotevu na dhambi kubwa.

Hii inamaanisha kwamba Bid’a ni uzushi katika matendo yaliyo elekezwa na Mtume saw ikiwa pia ni pamoja na kutenda kitendo ambacho hakikuelezwa na Mtume saw na wala hakuna dalili inayo elezea njia utekelezaji wake. Na hili lipo katika kanuni za kisheria kwa kauli ya Ukalifishaji (uwajibu wa kubeba majukumu) au katika kauli za mawaidha ( matukio). Hivyo basi iwapo Mtume saw alifanya sijda mbili na mtu akafanya sijda tatu, mtuhuyu atakuwa amefanya Bid’a kwasababu atakuwa amekiuka kitendo cha Mtume saw. Aidha akama mtu atakuwa ametenda kitendo ambacho hakikutendwa na Mtume saw kamavile kuendesha gari, na hali yakuwa Mtume saw hakuendesha gari, kitendo hiki hakiitwi Bid’a, bali  kitendo kama hiki kinaweza kuzungumziwa kwa misingi ya hukmu za kisheria, ambapo tunakuta kwamba kitendo cha kuendesha gari ni ruhsa (mubah), na mifano mingine kama huu.

2- Kukiuka amri ya Mtunga sheria (Allah sw) ambayo haikuja na utaratibu wa namna ya kuitekeleza, lakini imeelezwa katika hali ya jumla, Mutlaq, haiingii katika yaliyo Bid’a ila huwa katika hukmu za kisheria, ina hesabiwa kama haram (kilicho katazwa) au makrooh (kisicho faa)  iwapo ni kauli ya Kukalifisha, na kuelezewa kama Batil au Ufisad iwapo ni kauli ya waadh (maelezo), hali hii hufafanuliwa na kielelezo (Qareenah) inayo ambatana na kauli rasmi:

Mfano ni kauli ya Mtume saw:

«مَنْ أَسْلَفَ فِي شَيْءٍ فَفِي كَيْلٍ مَعْلُومٍ وَوَزْنٍ مَعْلُومٍ إِلَى أَجَلٍ مَعْلُومٍ»

“Yeyote atakaye lipa pesa kwa kutanguliza (‘advansi’) lazima iwe inafahamika kiwango cha kipimo na uzito kwa muda unaofahamika” [Imeelezwa na Bukhari]

Hapa imeamrishwa “salaf” (kumlipa muuzaji mwanzo) katika masharti ya kimaneno , na kuamrishwa kwamba “salaf” yapasa kuwa katika kipimo na uzito unao fahamika na katika muda unao fahamika. Aidha Mtunga sheria hakuweka wazi njia/namna ya utekelezaji wa hili, kwa mfano pande mbili zinazo husika yapasa kukabiliana na kusoma baadhi aya za Qur’an, kisha wanasonga mbele na kuwapamoja kuanza kulitazama suala la “salaf”, kisha hitajio na ridhio (kuridhika) hutokea na kukamilisha jambo.

Hata hivyo hii si hoja kwani Mtunga sheria hakubainisha namna ya kulitekeleza bali ameliacha jumla kwamujibu wa makubaliano, kwahiyo, Yule ambaye atalipa kwa kutanguliza, kamavile kutekeleza mkataba kinyume na maamrisho ya Mtunga sheria, yaani kwamfano bila kuwepo kipimo maalum, uzito na muda maalum, haitahesabika kwamba amefanya Bid’a bali ni mtu aliye  vunja hukmu ya Mtunga sheria na hukmu yake ni Batil au Ufisadi  kutegemea na aina ya ukengeukaji.

Mfano mwingine, Muslim amechukua kutoka kwa Ubada Ibn As-Samit kwamba alisema:

«إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ ﷺ يَنْهَى عَنْ بَيْعِ الذَّهَبِ بِالذَّهَبِ، وَالْفِضَّةِ بِالْفِضَّةِ، وَالْبُرِّ بِالْبُرِّ، وَالشَّعِيرِ بِالشَّعِيرِ، وَالتَّمْرِ بِالتَّمْرِ، وَالْمِلْحِ بِالْمِلْحِ، إِلَّا سَوَاءً بِسَوَاءٍ، عَيْنًا بِعَيْنٍ، فَمَنْ زَادَ، أَوِ ازْدَادَ، فَقَدْ أَرْبَى»

Nilimsikia Mtume saw akikataza kuuza dhahabu kwa dhahabu, fedha kwa fedha, ngano kwa ngano na mtama kwa mtama, tende kwa tende, chumvi kwa chumvi , isipokuwa kwa kiwango chake kamili na kipimo kamili. Na yeyote atakaye ongeza au kikiongezeka atakuwa ame chukua Riba”

Iwapo muislam atakengeuka Hadith hii akaamua kuuza dhabu kwa dhahabu kwa kuzidisha badala ya kipimo kwa kipimo hahesabiki kama aliye tenda Bid’a ila huhesabiwa ametenda kitendo cha Haram, ambacho ni Riba, kwakuwa hakuna namna maalum iliyowekwa kutekeleza tendo hili kama tulivyokwisha elezea mwanzo, bali imeachwa kama suala jumla kwa mujibu wa makubaliano yao.

Kwa mfano Mtume saw anasema:

«فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاكَ»

 “Chagua aliye na Dini utafanikiwa” [Bukhari]

Yule ambaye hataoa mwenye Dini haisemwi amefanya Bid’a bali hukmu ya kisheria kuhusu kuoa asiye na Dini  yapaswa kusomwa.  Kwasababu sharia haikuweka kipimo maalum cha kivitendo katika kuchagua, kama vile Yule abaye anataka kuingia katika ndoa amkabili mtarajiwa na kusoma Ayat Al-Kursi, kisha amsogelee hatua moja na asome  Ma’oozaatain (Surah al-Falaq and An-Nas), kisha asongembele hatua moja na aseme Bismillah, ndipo anyooshe mkono wake wa kuume na kuomba kuuoa/ kuposa. Bali jambo hili limeacwa huru kwa mujibu wa hali ya usahihi wa mkataba, hivyo kusoma juu ya tukio la ukengeukaji katika hali kama hii huweza kuwa kuhusu Hukmu za kisheria na wala sio kuhusu Bid’a.

Maelezo haya yanathibitisha kilichoelezwa katika Hadith tukufu zinazo elezea ukiukwaji wa namna hii kama suala la Hukmu za kisheria wala sio Bid’a.

Kutoka kwa mama wa waumini, A’isha (ra) amesema kwamba Mtume saw amesema:

«أَيُّمَا امْرَأَةٍ لَمْ يُنْكِحْهَا الْوَلِيُّ فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ»

“Mwanamke yeyote ambaye ataolewa pasi na walii wake, basi ndoa yake ni Batil, ndoa yake ni Batil, ndoa yake ni Batil,” [Ibn Maja]

Hapa tunaona kwamba hukmu ya ndoa pasina walii ni Batil, wala sio Bid’a.

Kutoka kwa Abi Sa’eed Al-Khudri katika Hadith ya Uchinjaji:

«… وَكُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ…»

“…Vyote vyenye kudhuru ni Haram…” [Malik]

Katika hadith hii inaelezwa kwamba vinvyo dhuru ni Haram wala sio Bid’a

Nakutoka kwa Abi Tha’laba Al-Khushani kwamba Mtume saw alisema:

«أَكْلُ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنْ السِّبَاعِ حَرَامٌ»

Kula wanyama wawindao kwa meno ni Haram” [Malik]

Ameeleza hapa kwamba ni Haram  na wala sio Bid’a

Kutoka kwa Abdullah Ibn Zurair kwa maana ya Al-Ghafiqi kwamba alimsikia Ali Ibn Abi Talib (ra) akisema Mtume saw amesema:

«أَخَذَ حَرِيرًا فَجَعَلَهُ فِي يَمِينِهِ وَأَخَذَ ذَهَبًا فَجَعَلَهُ فِي شِمَالِهِ ثُمَّ قَالَ إِنَّ هَذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي»

 “Alichukua Hariri kwa mkono wake wa kuume na akachukua dhahabu kwa mkono wake wa kushoto na akasema hivi viwili vimeharamishwa kwa wanaume wa ummah wangu” [Abu Daoud]

Ukengeukaji huu umeelezwa hapa kuwa ni Hram.

 

Na nyingi kama sio zote katika biashara na mikataba ni ya jumla, Mutlaq kwamujibu wa usahihi wa hali za mikataba zilizo tajwa na Sharia, na hazina njia ya utekelezaji zilizo wekwa rasmi bayana kama zilivyo katika masuala mengi ya ibadat, kwhivyo kukengeuka/kwenda kinyume na taratibu hizi huingia katika Hukmu ya Kisheria na wala sio katika Bid’a.

3- Kwa kuhitimisha:

Kukengeuka/ kwenda kinyume na njia aliyo utendaji wa Mtume saw katika masuala ya Qur’an na Sunnah ni Bid’a na nidhambi kubwa,  kitendo lazima kitekelezwe katika namna ambayo imeelekezwa kivitendo na na Mtume saw.

Lakini iwapo utakuwa unatenda kitendo ambacho hakikutekelezwa na Mtume saw, hukmu yake yapasa kutafutwa katika upande wa Hukmu za Kisheria kwa kuzingatia kauli za ki Takleef, au kauli za Wadh’, na hukmu yake itafahamika iwapo ni faradhi/wajibu, mandoob, Mubah, Makrooh au Haram….au kama ni Batil au Ufisadi.

Kukengeuka jambo ambalo ni jumla/Mutlaq katika Shariah ambalo kwalo Mtunga sharia hakubainisha njia yake ya utekelezaji, ukengeukaji huu utakuwa unatazamwa katika mtazamo wa Hukmu za Kisharia

 “yaani ikiwa ni Takleef – itakuwa Haram, Makrooh,…” or “ ikiwa ni Wadh ’- itakuwa ni Batil, and fasid”.

4- Sasa kwa mujibu wa swali lako kuhusu “mtu ambae huanzisha jambo  nzuri” . Hii ni mada kando, ina maanisha mtu ambaye mwanzoni alikuwa akitekeleza lile ambalo lime amrishwa na shariah na akawalingania wengine katika hilo nao wakamfuata; hupata malipo kwa kila anaye mfuata bila wao kupunguziwa katika malipo yao. Na Yule mtu ambaye mwanzoni alikuwa akitenda jambo ambalo sheria imelikataza na akalingania wengine katika hilo nawo wakamfuata, atabeba madhambi ya wote wanao mfuata na wala haipunguzi chochote katika dhambi za walio mfuata, ushahidi wa hili ni huu:

Katika Sahih yake, Imam Musli amechukua kutoka kwa Jarir Ibn Abdullah kwamba amesema:

جَاءَ نَاسٌ مِنَ الْأَعْرَابِ إِلَى رَسُولِ اللهِ ﷺ عَلَيْهِمِ الصُّوفُ فَرَأَى سُوءَ حَالِهِمْ قَدْ أَصَابَتْهُمْ حَاجَةٌ، فَحَثَّ النَّاسَ عَلَى الصَّدَقَةِ، فَأَبْطَئُوا عَنْهُ حَتَّى رُئِيَ ذَلِكَ فِي وَجْهِهِ. قَالَ: ثُمَّ إِنَّ رَجُلًا مِنَ الْأَنْصَارِ جَاءَ بِصُرَّةٍ مِنْ وَرِقٍ، ثُمَّ جَاءَ آخَرُ، ثُمَّ تَتَابَعُوا حَتَّى عُرِفَ السُّرُورُ فِي وَجْهِهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً، فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ، كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ، وَمَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً سَيِّئَةً، فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ، كُتِبَ عَلَيْهِ مِثْلُ وِزْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أَوْزَارِهِمْ شَيْءٌ»

Kabila la waarabu wa jangwani walifika kwa Mtume saw akawatazama.A clan of desert Arabs arrived to the Prophet ﷺ looked at them. Walikuwa katika mavai ya dhiki. Mtume saw akawaona katika hali ya huzuni na uhitaji mkubwa, basi Mtume saw aka washawishi watu wawape sadaqah lakini walikuwa wakichelewa kuitikia wito, na halihii iliakisiwa katika uso wa Mtume saw, basi mtu mmoja kutoka katika Ansar alifika na mkoba wenye fedha, kisha mwingine akafuatia, na wengine wengi nao wakajitokeza, sura ya Mtume saw ika ng’aa kwa furaha. Kwahali hiyo Mtume saw akasema: “ yeyote Yule atakye anzisha kitendo chema katika uislam na akaigwa na wengine katika kukitenda atapata malipo kwa hilo na malipo ya wale walio mfuata bila wao kupunguziwa chochote katika malipo yao. Na yeyote anakaye anzisha kitendo kiove katika Uislam kisha akafuatwa na wengine atapata dhambi za hilo na dhambi za wale wote waliomfuata bila wao kupunguziwa dhambi zao hata kidogo”

Kilicho wazi katika Hadith hii ni kwamba walichelewa katika kuitikia wito wa kutoa Sadaqah kisha mtu mmoja kutoka katika Ansar akasongambele haraka akiwa na Sadaqah na waliobaki wakamfuatia mpaka furaha ikadhihiri katika uso wa Mtume saw.

Namuomba Allah sw jawabu hili liwe nilenye kutosheleza kwa idhini ya Allah سبحانه وتعالى.

Wa Assalaam Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu

 Ndugu yako,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

 

Read 656 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…