Monday, 19 June 2017 00:00

Akliya ya Mufti

Ifuatayo ni sehemu iliyochukuliwa kutoka katika tafsiri ya kiarabu ya maswali na majibu ya enzi za Sheikh Taqiuddin an-Nabhani.

 

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali na jawabu

Swali:

Katika baadhi ya maswali na majibu yake Hizb inasema kamwe haitoi fatwa na katu mashababu wake sio mamufti (watu watoao hukmu za kisheria) na iwapo angetakiwa kutowa fatwa basi angejibu kwa uwazi kabisa kwamba sisi sio mamufti. Hoja hii inamaanisha kwamba tunawazuia watu kutuuliza juu ya hukmu za kisheria na hili pia ina maanisha kuficha elimu/maarifa na mambo haya yote hayafai kuwa yanatoka kwetu. Sababu ni kwamba kuwafanya watu wasiirejee Hizb sio sahihi kwa sababu miongoni mwa malengo yetu makuu ni kuwalingania watu hadi Ummah uikubali Hizb na kuzifanya fikra zinazobebwa na Hizb kutawala fikra za watu. Pia kwa kuwa kuficha elimu nijambo lisilo ruhusiwa kwa mujibu wa kauli ya Mtume SAW ….sasa nivipi tutaoanisha baina ya fikra za Hizb na kile tunacholenga kukipata na kile ambacho kilichofanywa wajibu juu yetu kwa mujibu wa Shariah?

Jawabu:

Ifuatayo ni maana ya Hizb kama ilivyo chapishwa katika ukurasa wa mwisho wa kitabu kiitwacho “Mafaaheem”: [Hizb-ut-Tahrir ni chama cha kisiasa na Mabda yake ni Uislam] vilevile imeelezwa katika Mafaaheem: [Ni wajibu kwa kikundi/chama kinacho beba ulinganizi wa kiislam kuwa kikundi/chama cha kisiasa na hairuhusiwi kuwa kikundi/chama cha kiroho, cha kimaadili, cha kiusomi au chama cha kitaaluma au chochote katika namna hii au chakufanana navyo.

Hakika ni muhimu kwa Kutla (kikundi) kuwa cha kisiasa na ndio kwa ufahamu huu imekuwa Hizb-ut-Tahrir. Hizb-ut-Tahrir ni chama cha Kiislam, chama cha kisiasa chenye jukumu la kisiasa na kinafanyakazi kuuthakafisha ummah kwa thakafa ya Kiislam ambapo nyanja ya kisiasa ndio inaojitokeza] nahiki ndicho kilichotajwa katika kitabu ‘At-Takattul: [Na pindi Mabda (mfumo) itakapo zama katika akili za watu kamwe haiwezekani kubakia ndani ila ita wasukuma kubeba ulinganizi ambapo matendo ya kida’awah yatakuwa kwa mujibu wa fikra hiyo na itasongambele kwa kufuata manhaj yake na kufungwa na mipaka yake. Uwepo wao huwa nikwa ajili tu ya mfumo na kubeba ulinganizi kwa hilo, na kutimiza majukumu yake ya kisharia. Na ulinganizi huu unalenga kuufanya ummah ushikamane na mfumo huo pekee na kujiepusha na kingine chochote ilikufikia kujenga ‘wai amma’ (ufaham jumla)]. Kitabu kinandelea: [wai amma juu ya mfumo itapelekea kuunganisha fikra, rai na imani zilizopo katika wengi wa ummah kama sio kwa umma wote na nikwakupitia hii ndio lengo la ummah huunganishwa kama ilivyo kwa Aqeedah yake na mtazamo wake katika maisha].

Pia imetajwa katika kitabu ‘At-Takkatul’: [Ni muhimu kuweka kizuizi kizito baina ya akili na nyanja ya taaluma ilikwamba thaqafah ya Hizb isifuate mrengo wa kuwa ni thaqafah ya kitaaluma]. Halafu kinaeleza: [Nimuhimu kuweka kizuizi kizito baina ya wale ambao wamesha thakafika na kuwa sehemu ya Hizb dhidi ya nyanja ya kitaaluma katika thaqafah ya Hizb na kuweka umakini ilikwamba lengo la thaqafah ya Hizb ni kubadilisha ufahamu na kufanyakazi katika uwanja wa mapambano wa maisha na kuchukua uongozi wa kifikra kwa ummah na hairuhusiwi kwa mtu huyu kwendea mbio nyanja ya taaluma]. Kisha kikasema: [Na nihatari kusonga mbele na thaqafah kwa kuendea nyanja ya taaluma kwasababu itapoteza lengo msingi la kazi]. Fikra hizi, ndio umbile la Hizb na huwakilisha picha ya kila shababu katika Hizb, hii ni kwa sababu Hizb inabeba uzinduzi kamili wa kifikra na kwa ajili hiyo kila mwana Hizb ni Hizb na umbile la Hizb ni la kila mwana Hizb. Kwa hali hiyo ilivyo kwa umbile la Hizb na la kila mwana Hizb haiwezekani kwake kuwa Mufti. Naye ni mbeba ulinganizi ambaye anasongambele katika njia ya kisiasa nayo ni siasa wala sio kitu kingine.

Taswira ambayo inajengeka katika mabongo ya watu kuhusu haiba/shakhsiya yoyote miongoni mwa shakhsiya bila kujali ni Shakhsiyah Haqeeqiyah (halisi) kama ilivyo kwa shakhsiya ya kiongozi au ya mtawala, au iwe ni Shakhsiyah Ma’nawiyah (isio halisi) kama shakhsiya ya chama cha kisiasa au ya taasisi ya kihisani. Na hivi ndivyo ambavyo watu hujengeka na kufafanua tabia zao mbele ya shakhsiya hii. Na taswira ya Hizb-ut-Tahrir ambayo ina fanyajuhudi kuiingiza katika mabongo ya watu ni taswira ya kiongozi (Qaa’id) mwenye ufahamu, mwanasiasa mbunifu, taswira ya mufakirina wa hukmu, na taswira ya mtawala muadilifu. Kwa sababu huwa malengo yake ni katika kuuongoza ummah katika mapambano dhidi ya watu na mataifa, na shauku ya kuwa changamsha kwa mwamko sahihi kwa kutumia fikra angavu na anafanyajuhudi ilikuchukua mamlaka kutoka kwao na kusimamia masuala yake. Kwahivyo iwapo taswira ya Ummah iliyojengeka kwa haiba/shakhsiya hii haidhihirishi sifa za uongozi halisi je nivipi ummah huu utamdhaminia utawala/uongozi na kuharakika katika kupata kufa shahidi akiwa katika juhudi za kufanikisha malengo yake?

Hakika maadui wa Uislam wamewafikishia na kuwonesha Waislam taswira iliyo haribiwa ya Mtume (saw), taswira ambayo imevuliwa mbali na fikra za Kiislam jambo lililo wafanya waweze kutumia mbinu hii kuufanya uongozi wa Waislam kwa Uislam kuchukuliwa kama nijambo la matakwa ya fikra tu na kwamba kumfuata Mtume (saw) kama kiigizo chema katika masuala kama ya kisiasa na utawala nikutafuta kushindwa katika nyanja za kimamlaka na siasa. Kwakuwa taswira hii hairejei katika mabongo ya Waislam kamwe hawataongozwa na Uislam na muda wote ambapo taswira ya Abu-l-Qassim (Mtume saw) itaendelea kuwa mabunio yasiyoeleweka katika Ummah, basi katu ummah hautaweza kumakinika na kuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya Ukafir na Makafir. Kwahivyo suala la kuufahamisha ummaha taswira sahihi ya uongozi wake wa-Kiislam ndilo pekee litakalo imarisha uongozi wa ummah nakuufanya uwe nauwezo wa kuingia katika mapambano na mataifa.

Na kuwafahamisha Waislam taswira ya Hizb-ut-Tahrir kama Mufti wao inaweza kuwafanya wao kuwa maamuma wa kuswali nyuma yake lakini hilihaliwezi kuwafikisha katika  kuongozwa na Hizb na vilevile suala hili litawafanya waifuate Hizb kwa ajili ya maalumati na elimu tu ni sio kwa ajili ya kuilinda na kuihifadhi matendo yake (ummah). Kwa ajili hiyo kwetu, iwapo kweli sisi tutataka kuchukua uongozi wa ummah, yatupasa ummah uchukue kwetu taswira ya kiongozi, taswira ya siasa na taswira ya mufakirina na mtawala shupavu na hakika hakuna njia ya kuyafikia haya bali tu nikwa kuwapatia ummah taswira ya Hizb-ut-Tahrir. Kwa hivyo nikatika jambo kuu la wajibu la kujifunga nalo, yaani kufanya kwamba taswira ya kila mwana Hizb kuwa taswira ya Hizb mbele ya macho ya Ummah, na zaidi ni kwamba haiba/shakhsya ya kila mwana Hizb iwe ni ya mpambano wa kisiasa katika macho ya watu ambao wanafanya juhudi za kuchukua uongozi wa watu ilikwamba waweze kukabili machungu ya mpambano. Kwa hivyo inapasa tabia ya kila mwana Hizb iwe ni ile tabia ya mtu ambaye yupo katika mpambano uliojengeka katika ufahamu unaolenga kufikia kuinyanyua bendera na kufikia lengo, na hili halimaanishi jambo lingine isipokuwa kuinua neno la Allah SWT, kuvunja vikwazo vya kimaada ili kufungua njia kwa ajili ya Da’awah ya Kiislamu. Ama hakika hii ndio shakhsiyah/ haiba ya Hizb katika uhalisia wake na hii pia ndio taswira yake na dhati yake halisi. Kwa hiyo ni wajibu kwa kila mwana Hizb kuwa fahamisha watu taswira ya Hizb-ut-Tahrir kama ilivyo na wala sio taswira ya Muft au Umuft.

Muft ni mtu ambaye yupo hadhir muda wote kwa kutoa Fatwa na watu humuendea kilamara kwa ajili ya kupatiwa hukmu za kisheria juu ya suala maalum ambalo kila mmoja amekutana nalo au linalo mkabili, na ‘Aalim ni mtu mwenye jukumu la kutafuta maarifa katika vitabu lakini hawazungumzii watu juu ya Fatwa kwa masuala japo kuwa iwapo ataulizwa kuhusu jambo fulani maalum anatoa jawabu kama jawabu la suali lililo ulizwa na wala sio Hukmu maalumu kwa jambo maalum. Mlinganiaji/mhubiri (Waa'idh) ni mtu anaye walingania watu juu ya khofu kwa adhabu za Allah SW, kuhusu pepo na siku ya kiama, ambapo Mwalimu ni mtu ambaye huwafunza watu kibinafsi maarifa jumla yasio na utekelezaji wowote katika mazingira, uhalisia, wala katika kuifanyia kazi. Ama hakika kila mmoja katika wane hawa anayo taswira iliyo tofauti kabisa na nyingine. Kwa hivyo taswira ya Muft ni tofauti na taswira ya ‘Aalim, na ile taswira ya Waa’idh inatofautiana ya taswira ya Mwalimu na hata ikitokea Waa’idh kuwa ni Mwalimu basi kila taswira ya sifa katika sifa hizi huwa ndio yenye kuwakilisha hiyo sifa na wala sio nyingine tofauti. Na hii ndio uhalisia hata kama atakua na sifa zote nne (Mufti, ‘Aalim, Waa’idh na Mwalimu). Kwa ilivyo Hizb-ut-tahrir haina sifa zozote za Muft kwa sababu Hizb haijipeleki mbele kwa ajili ya kutoa Fatwah na wala hashughuliki na mas’ala ya kibinafsi ya mtu katika maelezo yake kama mtu binafsi ilikumpatia Hukmu ya kisheria, bali Hizb ni mwanasiasa ambaye anajali masuala ya watu kwa mujibu wa Hukmu za kisheria. Wala Hizb haina sifa za ‘Aalim kwa sababu jukumu la Hizb sio kushughulika na masuala ya ukusanyaji maarifa katika vitabu na hatakama Hizb itarejea vitabu ilikupata maarifa kwa kuwa kujipenyeza katika maarifa sio katika jukumu lake wala sio katika lengo lake, bali ni njia iliyotumika katika kazi yake ya kisiasa. Wala siye Wa’aidh anaye walingania watu kuhusu Aakhira na kamwe hawaondoi watu katika kubobea kwenye dunia lakini huchunga mambo yao na anawapatia ufahamu juu ya dunia na kuifanya lengo la dunia ni furaha ya baada ya kufa na kupata radhi za Allah. Walapia sio Mwalimu japokuwa Hizb inawalea watu kwa fikra na sheria kwa hiyo kufundisha maarifa tu sio katika kazi yake na wala Hizb haihusiki nayo, lengo lake ni kufanya kazi kwa mujibu wa fikra na hukmu ili iwe inawapatia ummah maarifa yaliyo fungamana na uhalisia katika mazingira ya kisiasa na wala sio kama maarifa kwa ajili ya kupata manufaa yake na wala sio kama elimu.

Kwa hiyo nikatika jambo la dhulma kusema kwamba Hizb ni mufti na niupotofu kama mwana Hizb atakuwa Mufti. Hakika nikweli kwamba hakuna kinacho zuia kumjibu muulizaji katika mas’ala yanayo hitaji hukmu za kisheria juu ya suala maalum lakini zaidi ya hapo ana mjibu kwa namna ambayo pia anamthaqafisha na kumkuza kifikra juu ya Hukmu ya Kiislam kwa lile alilo uliza na kujitahidi kumvuta kimaarifa na mwangaza wa kielimu. Kwa hiyo hulichukulia swali na kulijibu lileambalo linauwezekano wa kumthaqafisha na humpatia jawabu kama thaqafah na wala sio kama Fatwaa. Kwa hivyo hawezi kuwaondoa watu katika muelekeo wa fikra na Hukmu bali hujitahidi kuwaelekeza huko, kwa sababu hiyo hujibu ili kuwavuta kwake na kuyafanya mabongo yao yafungukiwe kwa fikra na mitazamo ya Hizb. Hata hivyo katu hajiweki mbele ili kutoa Fatwaa ila humbadilisha muulizaji kutoka kutafuta Fatwaa na kumuingiza kushiriki katika kujadiliana ambako kutapelekea kuthaqafika kwa muulizaji kwa Hukmu za Kisheria ilikwamba awe anatenda kwa mujibu wa maarifa yake aliyo mpatia na sio kutenda kwa mujibu wa kipi amekipata kutoka katika Fatwaa. Hivyo basi kuna hatari kubwa katika kuwalingania watu ki Fatwaa na kuwapa Hukmu za kisheria kama Fatwaa kutoka miongoni mwa Fatwaa. Na iwapo hili litatokea litaweza kumbadilisha Shabab wa Hizb kuwa kitu kingine ambacho sio Hizb na kukifuata hicho huweza kuchafua na kuharibu taswira ya Hizb. Katu mwana Hizb haifichi elimu/maarifa yake bali pia haitoi elimu yake kama maarifa tu bali huwa anaitoa kama thaqafah iliyo makini, kama fikra angavu na kama fikra miongoni mwa fikra zinazo athiri tabia.

Kwa ajili hiyo, uovu wa kuibadili Hizb kuwa Mufti upo wazi kama ilivyo kwa shabab wa Hizb kuwa Mufti. Jambo hili litapelekea katika maangamivu kamili ambayo hayataishia kwa shabab pekeyake au kwa Hizb pekee bali kwa Ummah mzima ambao unahitajio kubwa la uongozi wa Hizb na fikra (mabda) iliyobebwa na Hizb katika kuubadili Ummah na kutokuifanya kuwa ni mtazamo wa kimaisha bali ni suala la kumtibu mtu binafsi.

Chama hiki kimepitiwa na mitihani ya namna tatu inayojaribu kukitoa katika njia na lengo lake la asili, majaribio ya kuing’oa na kuiweka nje ya siasa na kuelekeza kwa Dini na Fiqh. Kwa hiyo pindi Naibu/mwakilishi alipo toa hutba zenye muelekeo haswa wa kisiasa katika Bunge la Waakilishi la Jordan, hali hii ilileta mshituko na mkanganyiko miongoni mwa baadhi ya mashabab ambao kwa sasa hawapo miongoni mwa wengine, waliouliza swali: Ukowapi Uislam katika hutba hizi?  Na ikowapi Aqaa’id na Ahkaam katika mijadala hii ya Hizb-ut-Tahrir ndani ya bunge/baraza la wawakilishi? Sintofaham hii pia ikaibuka pindi Hizb ilipoanza kutoa kwa kila wiki matamko na maelezo ya kisiasa ambayo yalipelekea mashabab wengi miongoni mwao wakisema: Hizb imechepuka kutoka katika njia yake na kamwe haiwezi kuendelea kuhesabika kama Chama cha Kiislam bali kimekuwa Chama cha Kisiasa kama vilivyo vyama vingine (vya ‘kidemokrasia’). Wakajaribu kuki elekeza chama muelekeo uliotofauti na siasa na kutoka kutoa machapisho ya kisiasa ili irudi katika machapisho yanayohusu hukumu za Kiislam na kuwa na mijadala iliyojikita katika Ahkaam As-Shar’i. Na pindi Hizb ilipoanza kuwakabili watu walio katika utawala na kujifunga katika machapisho juu ya kukosoa matendo yao na ikajifunga katika kitendo cha kushambulia mahusiano baina ya utawala na Ummah basi wengi katika watu wakiwemo baadhi ya mashabab walilifanya ni jambo kubwa sana kwamba Hizb inashambulia utu (watawala wenyewe kibinafsi) na kuchagua kudhihirisha baadhi ya matendo ya baadhi ya watawala, na walisema: Hizb imeamua kutukana na imeamua kubadilisha majukumu yake kuhusiana na fikra na kuanza kuwalenga watu na kutoka katika kuzungumzia Uislam na kuanza kuzungumzia watawala na wakajaribu kuirejesha Hizb katika machapisho ya Kiislam na kuiweka mbali na kazi ya kuwakosoa watawala. Hii ndiyo mitihani mitatu ambayo Hizb iliweza kuivuka na ikafaulu hivyo, na sio kwa kusimama na kuongea dhidi ya hoja hizi na wala sio kwa kukubali mijadala juu yake ila (ilikabiliana nayo) kwa kuendelea kutoa matamko ya kisiasa na kufanya amali za kisiasa na kuendelea kupiga katika mikono ya wale ambao waloshikamana na mamlaka kwa mapigo ya nguvu tena ya mfululizo ili kuushusha upande wao na kuondoa nafasi yao ya utukufu na matumaini ya watu kwao. Na Hizb ikaendelea kuhifadhi taswira yake ya asili ambayo ni Chama cha Siasa na hakina kazi zaidi ya amali za kisiasa na mawazo haya yasiyo ya ukweli (japo yawe yametoka kwa watu waaminifu) hayawezi kuihamisha Hizb japo kwa umbali wa unywele kutoka katika utambulisho wake au wala kuiathiri Hizb hata kwa athari ndogo kutoka katika uhalisia wa shakhsiya yake.

Ama hakika ni Hizb-ut-Tahrir na ni Chama cha Kiislamu kutoka katika muelekeo wa mfumo (mabda) wake na wala sio Chama cha Kiislamu kama ilivyo miundo mingine ya Kiislam….bali ni Chama cha Kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislam. Kwa hivyo Uislam ndiyo mabda (mfumo) yake lakini sio kazi yake na Uislam ndio msingi wake bali sio umbile lake. Kwa hiyo Hizb itachukua mamlaka pindi yatakapo kuwepo kwake ilikuweza kuchukua majukumu ya kuchunga masuala ya watu katika uhalisia wake na Hizb ita uhesabu utawala muda wote iwe ipo katika utawala au nje yake. Kwa kazi zake zote zimejifunga katika amali za kisiasa, ima kimatendo kwa kusimamia masuala au kwa maoni kwa kuwahesabu watawala kwa misingi na vigezo vya Uislam.

Na ilivyo Hizb na mjumuiko wake wa mashabab na uongozi nikwamba iwapo itatokea watu wakasema kwamba Hizb imesema kadha wakadha au imefanya hili nalile hakika wanamaanisha mashabab wa Hizb na machapisho yake kwa sababu Hizb ni hisia ya kifikra katika jumla yake kiasi kwamba kila mwana Hizb ni Hizb. Kwa hiyo iwapo taswira ya mmoja wa wana Hizb au mmoja wao akavaa taswira ya Mufti basi Hizb itakuwa imechakachulika na kuwa Mufti. Hili nikatika nyongeza ya yanayo changia katika kupondoka (kwenda kombo) kutoka katika amali za Hizb na kupondoka kutoka katika utambulisho wake kwa kuwa mambo haya baada ya muda fulani yata bomoa taswira ya Hizb na pia kuwa badili mashabab wa Hizb kutoka kuwa wanasiasa na kuwa mamuft. Kutokana na athari hizi inakuwa hatari kwa mashabab kuanza kufanyakazi ya kutoa fatwa kwa kuwa wataanza kutambulika kwa watu kwamba wao ni mafuqahaa badala ya kuonekana kuwa ni viongozi, kuwa ni watafuta maarifa/elimu badala ya kuwa mada’ai na hatimaye Hizb itakuwa nikama taasisi ya elimu badala ya chama cha kisiasa. Katika haya yote kuna madhara makubwa tena ya wazi kwa mashabab wenyewe binafsi na pia kwa Hizb.

Bila kujali kwamba utoaji wa fatwa nikatika amali ndogo sana za Fiqh na bila kujali kwamba nikitendo cha kauli ya muft ambayo hudhihirisha udororaji wa mujtama, na bila kujali kwamba jambo hili nikushajiisha watu kuulizia fatwa ambazo huziweka Ahkam Shari’ah kwa wajinga kuzitumia kutoa hukmu, na bila kujali kwamba kutoa jibu la haraka au kutoa majibu ya kukariri (yaliyokwisha hifadhiwa katika mabongo) ni kujikurubisha zaidi katika kukosea katika mas’ala yaliomengi. Hakika kuwa shauri mashabab kwamba wasijiweke katika majukumu ya kutoa fatwa na kuwafahamisha hatari ya wao kuwa kama mamuft sio kwa sababu ya kutatuwa swala la fatwa katika mujitama na wala sio kupinga watu kufahamu Ahkam Shar’iah bali kwa ajili ya kuhifadhi taswira halisi ya Hizb katika macho ya watu kwani lazima ionekane na kufahamika kwamba ni chaa cha kisiasa wala sio aina nyingine ya chama. Pia ni kuchunga mashabab wasiende nje ya misingi ya Hizb na hatimaye kuwa watu wengine kabisa kama ma Mufti au ma Ulamaa au wa Hadhir au Walimu.

Katika kuhitimisha ni kwamba sio sahihi kwa shabab kujitanguliza kutoa fatwa kiasi kwamba watu watamuendea ili awatolee fatwa. Hata hivyo iwapo ataulizwa kuhusu namna ya du’aa ya Qunuut atapokea nafasi hii kwa haraka na kuitumia kama wasaa wa kuelezea maana kamili ya Du’aa na iwapo ataulizwa kuhusu mjongeo/haraka katika swala atapokea ujibuji wake kama nafasi kuelezea kuhusu maana kamili ya Taqliid, na iwapo ataulizwa kuhusu uwakala katika kumiliki atalipokea swali hili na kuuelekeza mjadala katika ufaradhi wa kujifunga na Ahkaam Sha’riiah.

Kwa hivyo kamwe hataficha kile anacho kifahamu na wala hatafanya juhudi za kujifunza ili tu awe nimwenye kutoa fatwa badala yake katika muda huu na muda wote anakuwa katika hali ya mlinganiaji (Mbeba da’awah) katika manhaji ya kisiasa, yaani yeye ni mwanasiasa ambae mfumo (mabda) wake ni Uislam.

 

Mwezi 22, Rabee’ul Awwal 1390

26/06/1970

 

Read 346 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…