Monday, 19 June 2017 00:00

Kushindwa kwa umoja wa Afrika (AU) kufikia malengo


 1. Historia Ya Kuundwa AU Kwa Kifupi:

Mnamo tarehe  25/05/1963  Umoja Wa Nchi Huru Afrika (OAU) ulianzishwa mjini Addis Ababa, Ethiopia, ikiwa ni makubaliano ya Wakoloni yaani Uingereza, Ufaransa, na Amerika kuikusanya pamoja  Afrika ili kurahisisha unyonyaji kisha ukabadilika na kuitwa Umoja Wa Afrika( AU) tarehe 09/07/2002.

Ifahamike kwamba kiasili Ubepari hutumia Ukoloni kama njia( methodology) ya kufika lengo lake la unyonyaji. Kutokana na kukosekana upinzani wa kifikra na kijeshi barani Afrika  pamoja na uwepo wa  rasilimali nyingi za wazi, ukoloni imekuwa  kama ndio lengo lenyewe badala ya kuwa njia ya kufikia lengo.

Hivyo katika karne ya 18AD na 19AD wakoloni  walianza  kuikoloni Afrika, na kuigawanya chini ya mataifa manane (8) ya kikoloni; Uingereza, Ujerumani, Hispania, Ubelgiji, Uholanzi na Ureno. Mataifa haya yaliendelea kushindana  kuikoloni  Afrika mpaka baada ya vita vya pili ambapo Amerika kupitia Umoja Wa Mataifa(UNO) kipindi hicho, sasa UN kuanzisha harakati  za “uhuru wa bendera” kwa Afrika.

Baada ya Uingereza kuona hatari ya Amerika na  Russia ( Soviet Union), ilianza kujihami katika  makoloni yake, ikaanzisha sera ya “kutofungamana na upande wowote”  kupitia kibaraka wake Nehru.  Kupitia sera yake hii ya kutofungamana na upande wowote(neutrality ) au “non alignment  movement” , Uingereza  ikimtumia Nehru ( India) ilishawishi mataifa mengine kama Indonesia,  Yugoslavia, China n.k  na kupelekea mkutano wa Bandug   mwaka 1954. Amerika ilitumia fursa hii kwa kuingiza mada ya ukombozi kutokana na ukolon “mkongwe” ikimtumia Titto, na  Naseer, iliingiza dhana ya uhuru na ikahamishiwa  Afrika mara baada ya mkutano huo.

Kwa kuona hatari hii Uingereza akayapa uhuru makoloni yake kama Zanzibar, Tanganyika, Nigeria, Uganda, n.k  na akayaunganisha na Jumuiya ya Madola(British Commonwealth) ambayo iliasisiwa 1931 na sekretarieti yake kuundwa 1965 jijini London.

Ufaransa naye akaafuata nyayo za Uigereza akazipa uhuru Morocco, Algeria , Tunisia, Senegal, Gabon, n.k na akaziunganisha na Francophone iliyoanzishwa baadaye mwaka 1970

Ama kuhusu Russia (Soviet Union) yenyewe ilishindwa mapema mapambano katika Afrika kutokana na udhaifu wa kindani na kutokuwa na makoloni kabla.

Amerika kwa upande wake hakuwa na makoloni kama Russia, lakini aliibuka taifa lenye nguvu likiendeleza mapambano ya kupigania uhuru kwa lengo la kupata mali za Afrika na kuondoa ushawishi wa Uingereza na Ufaransa na hata Russia.

Mapambano haya dhidi ya wakoloni wakongwe  ndani ya Afika ndiyo yaliyompatia Amerika makoloni kama Uganda, Rwanda na Burundi baadaye kabla ya kufanikiwa kuteka nchi nyingine nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania miaka ya hivi karibuni 

Mapambano haya ya kutafuta makoloni na ushawishi kati ya Amerika,Uingereza, na Ufrarsnsa yalipelekea makubaliano ya kuikusanya pamoja Afrika ili kurahisisha unyonyaji na hapa ndipo ulipobuniwa  Umoja Wa Nchi Huru za Afrika(OAU) 25/05/1963, hata hivyo mapambano ya Wakoloni ndani na nje ya taasisi hii kuhusu Afrika bado ni makubwa kwa sababu ya maslahi makubwa ya rasilimali zinazopatikana Afrika

 

 1. Malengo Ya AU Na Namna Yalivyoshindwa Kufikiwa

Kwa muijibu wa katiba ya AU ibara ya 2 ya Septemba 1963, malengo yafuatayo yalifikiwa:

 

Kufikia maisha mazuri kwa Afrika: Tangu kuanzishwa kwake AU miaka 54 iliyopita, Afrika haijawahi kupata nafuu ya maisha, walau harufu yake bali maisha yamezidi kuwa duni na umasikini kuongezeka maradufu. Mwaka 1990 Waafrika masikni sana walikuwa milioni 280, mpaka mwaka 2012 waliongeeka na kuwa milioni 330.  2/5 ya watu wazima katika Afrika bado hawajui kusoma na kuandika( Poverty in a Rising Africa, World Bank 2016)

 

Kudumisha amani, na umoja katika Arfrika:  Ndoto hii ya mchana kwa Afrika imeshindikana kwani tangu kuanzishwa kwake mpaka leo Afrika imeshuhudia mapigano , mauaji, mapinduzi na umwagaji damu kwa maslahi ya Wakoloni. Afrika imepoteza zaidi ya dolari bilioni 370 ambazo ni zaidi ya 65% ya pato la bara zima kutokana na machafuko haya. Afrika imeshuhudia mapinduzi 175 kati ya hayo 75 yakiwa yamefankiwa, 85% ya nchi za Afrika zimekutwa na mapinduzi walau mara moja katika historia . Vita vimepelekea kuuawa watu zaidi ya milioni 7 na kutengeneza wakimbizi zaidi ya milioni 19.(Understanding African Armies, 2016).Viongozi wa Afrika licha ya kukiri kuonewa na Mahakama Ya Jinai (ICC) bado wameshindwa kuijtoa kupitia AU.

 

Kulinda uhuru na kuondoa aina zote za ukoloni: Afrika bado inakoloniwa kupitia ukoloni mamboleo kwa mbinu kama watawala vibaraka, misaada, mikopo, makubaliano ya kimataifa, wataalamu, n.k. Mapambano ya kuikoloni Afrika leo yamebakia hasa katika nchi tatu yaani Amerika, Uingereza, na Ufaransa yakipelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe kama ilivyoshuhudiwa katika Siera Leone, Liberia, Sudani, Burundi,Kongo, n.k

 

 1. Sababu Za Kushindwa Kufikia Malengo
 • AU haikuanzishwa na Waafrika kwa manufaa ya Waafrika, bali ni makubaliano ya Wakoloni kama tulivyoona hapo juu. Hivyo kufikia malengo hayo iliyojiwekea ni ndoto ya wazi kabisa ambayo Wakoloni hawawezi kuiachia itimie.

 

 • Fungamano lililowakusanya watu katika umoja huo AU ni dhaifu, nalo ni fungamano la kizalendo na kimaslahi. Uzalendo kwa upande wake hauonekani ila katika raha na dhiki na katika hali ya kawaida huwa ni nadra sana, ama maslahi huvunjika pale yanapokosekana au kukiukwa. Kwa AU kuundwa chini ya msingi huu ni wazi haiwezi kufikia malengo hayo mazito.

Hivyo AU inaendelea kutumika na Wakoloni kufikia malengo yao huku Afrika ikiendelea kuzama katika maafa na maangamizi makubawa . Imekua AU ni “talking shop”, “dictators club”, au “puppets trade union” kama ilivyoitwa na baadhi ya wachambuzi ikiakisi uhalisia wake

 1. Hitimisho
 • Kutofikia malengo AU ni suala la kutarajiwa kwa vile haikuundwa na Waafrika kwa lengo la kuwaendeleza bali ni zao la fikra za Wakoloni kwa lengo la kuinyonya Afrika

 

 • Chini ya ubepari, Afrika itaendelea kukoloniwa kwani ukoloni ni njia(method) isiyobadilika ya kufikia lengo (Objective) ambalo ni unyonyaji kwa mataifa machanga.

 

 

 • Amerika kibinafsi imeendelea kuimarisha himaya yake katika Afrika kupitia makubaliano ya kijeshi ikianzisha kambi za kijeshi katika kanda mbali mbali za Afrika ili kuunga mkono vibaraka wake na kupindua viongozi wanaokwenda kinyume na maslahi yake.

 

 • Tutarajie mapambano zaidi katika Afrika na umasikini kwani kila kukicha mali mpya zinazidi kugunduliwa na Wakoloni wanafanya kila ouvu kuzipata mali hizo hata kwa gharama ya damu ya Watu wa Afrika wakiitumia AU

 

 

 • Lau msingi wa umoja kama huu ungekuwa ni fungamao la kimfumo, tena katika mfumo sahihi ambao ni Uislamu bila shaka kufikia malengo haya kupitia serikali ya Kiislamu ni haraka na rahisi kwani Uislamu una uwezo wa kukabiliana na changamoto zote za binadamu na tumeyaeleza haya kwa uwazi na upana katika vitabu vyetu kama “Mali Ya Serikali Ya Khilafah”, “Nidhamu Ya Uchumi Katika Uislamu”, “Nidhamu Ya Kijamii Katika Uislamu”, n.k
Read 385 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…