Tuesday, 18 July 2017 00:00

Kikosi cha Makomandoo Kumuuwa Yahudi Muovu

Mtume (saw)  atuma kikosi cha makomandoo kumuuwa yahudi muovu Salam bin Abil Huqaib

Baada ya kumalizika Vita vya Ahzab katika mwezi wa Shawwal 5AH, dola ya Kiislamu ilichukua hatua kadhaa kuangamiza na kuwatia adabu maadui wengine mbalimbali. Awali lilishughulikiwa kabila la kiyahudi la Bani Quraidha lililoisaliti dola ya Kiislamu kwa kuvunja mkataba wa amani, kwa kula njama ya kushirikiana na makafiri wengine katika Vita vya Ahzab dhidi ya Waislamu. Pia dola ikalipiza kisasi kwa kabila la Bani Lihyan lililowahi kuwauwa masahaba wa Mtume SAAW kwa uadui katika tukio la Biir-maun kwa kutumwa vikosi vidogo vidogo visivyopungua nane hususan katika mwaka wa 6 AH. kwa ajili ya kuzima uadui wa kabila hilo na makabila mbalimbali ya kiarabu. Aidha, ndani ya mwezi dhul-qadah mwaka huo huo Mtume SAAW aliotoa agizo la kukatwa kichwa (kuuliwa) mara moja adui mkubwa wa kiyahudi bwana Salam bin Abil-Alhuqaiq (Abu Rafi’). Yahudi huyu ndie aliyekuwa mfadhili mkubwa kwa kujitolea fedha na utajiri wake kufanikisha Vita vya Ahzab vilivyounganisha makabila mbalimbali ya kiarabu na mayahudi ili kuwapiga Waislamu kwa lengo la kuifuta kabisa dola changa ya Kiislamu. Kadhalika yahudi huyu alikuwa binafsi akimuudhi Mtume SAAW kwa kumkebehi na kumtukana matusi ya nguoni.Kwa hivyo, baada ya kumalizika Vita vya Ahzab na kutiwa adabu mayahudi wa Bani Quraidha, sasa ikawa zamu ya kumshughulikia adui huyu mkubwa.

Mtume SAAW akatangaza haraka jukumu hili na akawataka masahaba wake walibebe na kulitekeleza haraka iwezekanavyo. Waislamu kutoka kabila la Al-Khazraj haraka wakamkabili Mtume SAAW kuwa tayari kulibeba jukumu hilo. Kwa kuwa jukumu la awali la kumuuuwa adui kama huyu Kaab bin Ashraf lilibebwa na kabila Al-Aws. Mtume SAAW akachagua kikosi cha watu watano kutoka katika kabila Bani Salama wa (Khazraj) wakiongozwa na Abullah bin Atiq. Kikosi hiki haraka kiliondoka kuelekea upande wa Khaybar kwenye ngome na makaazi ya adui huyu mkubwa. Jua lilipotua kikosi kile kikawa tayari kimefika katika eneo lile. Walipoyakaribia makaazi ya adui, kiongozi wa kikosi Abdullah bin Atiq akawashauri wenzake wabakie nyuma kidogo ili afanye maarifa na ujanja wa kuingia ndani kwa yahudi huyu. Akanyemelea karibu na lango na kujifunika guo lake, mlinzi alipomuona akamruhusu kwa kudhani ni miongoni mwa wengine wanaoingia. Licha ya kiza kuanza kutanda, Abdallah bin Atiq akafanikiwa kuingia ndani ya ngome hiyo na kujificha na kuanza maarifa ya kumtafuta Abu Rafi’, na akagundua kwamba yumo katika mkutano na baadhi ya washauri wake.

Kwa hivyo, akawa hana namna ila kumsuburi kumaliza mazungumzo yao. Akajibanza kumsubiri. Baada ya kumalizika mazungumzo yao na kutawanyika, Abu Rafii akaelekea kwa familia yake. Hapo Abdulla bin Atiq akamfuata nyuma nyuma mpaka Abu Rafi’ alipoingia chumbani mwake kilichokuwa giza, akiwa katikati ya familia yake, akamwita kwa jina lake: ‘Yaa Aba Rafii uko wapi’? Nae akauliza: ‘nani wewe’? Abdullah bin Atiq alimuuliza ili ajue Abu Rafi’ yuko upande gani kwani giza lilikuwa limeanza kushtadi. Abullah bin Atiq alipogundua sehemu alipo akampiga dhoruba moja tu ya upanga lakini hakufa, akaanza kupiga kelele, hapo akamuuliza tena: ‘umepatwa na nini’? akajibu: ‘humu ndani mna balaa, mna mtu amenipiga upanga kwa nyuma’. Hapo Abdullah bin Atiq akamuongeza dhoruba nyengine lakini bado hakufa, akamuongezea kumchoma upanga wa tumbo hadi mgongoni mpaka akafariki. Akafungua mlango na kutoka nje, kwa bahati mbaya katika purukushani za kutoka nje ya ngome aliumia goti, akaamua kulifunga kilemba na haraka akenda mpaka walipo wenzake. Hapo akawashauri kwamba wasiondoke mpaka watakapohakikisha kwamba kweli Abu Rafii amefariki dunia.

Kulipokucha na alipowika jogoo asubuhi mapema mtangazaji wa eneo lile akatangaza kwamba Abu Rafi, mfanya biashara mkubwa wa Hijaz ameuwawa. Hapo haraka kikosi kikaondoka na kurudi Madina kwa Mtume SAAW. Akaelezwa Mtume SAAW ripoti ya tukio lote la kuuliwa kafiri Abu Rafi’ na kuumia goti kwa Abdullah bin Atiq. Hapo Mtume SAAW kwa miujiza akalishika goti la komandoo Abdullah bin Atiq, na likapoa kana kwamba halikuumia. Baada ya tukio hili mayahaudi walihangaika kwa jitihada kubwa kukitafuta kikosi hiki lakini hawakufanikiwa, kwa kuwa kilijificha na wakashindwa kuwaona, na kikaweza kurejea Madina salama usalimini.Miongoni mwa mafunzo katika kisa hiki, ni namna Mtume SAAW akiwa kiongozi alivyokuwa akishughulika kuwaondolea Waislamu na dola yake kwa ujumla kila aina ya fitna iliyowakabili na kukata mizizi yake ili kuondoa kila kizuizi mbele ya daawa/ulinganizi na maisha ya Waislamu kwa ujumla.

Pili, ushujaa wa masahaba wa Mtume SAAW, kiasi cha kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya Uislamu bila ya kukhofu chochote zaidi ya kutawakal kwao kwa Allah Ta’ala na kuamini kwao Qadhaa: kwamba halitowafika ila lililoandikwa na hatokufa mtu ila kwa ajal yake.
Na mwisho na muhimu zaidi, tunaona ulazima wa kuwa na dola. Kwa kuwa ni nguvu ya dola pekee na sio mtu binafsi au vikundi ndio yenye uwezo mkubwa wa kukabilina na kila aina ya vitisho na kutatua matatizo mbalimbali. Mtume SAAW alitoa agizo la kuuliwa yahudi adui akiwa yeye Mtume SAAW ni mtawala kamili na dola yake ya Kiislamu. Leo Waislamu tunakabiliwa na kila aina ya vitisho, mashaka na matatizo mbalimbali kuanzia kukashifiwa dini yetu, kutukanwa Mtume SAAW, Quran nk. Aidha, tunakabiliwa na unyama na uovu wa kijidola cha kiyahudi, (Israel), uovu wa vibaraka wanaouwa na kuchinja Waislamu kwa kulinda tawala zao kama yanayoendelea ndani ya Yemen, Syria, Saudia Uzbekistan, Libya nk. Bila ya kusahau uvamizi wa makafiri katika nchi zetu kuchukuwa rasilmali zetu, kuchafua thaqafa yetu na kueneza mfumo wao muovu wa kibepari ndani ya Iraq, Afghanistan, Somali nk.

Yote haya ni fitna ambazo zinahitaji kushughulikiwa kwa kiwango cha dola ya Kiislamu, ambayo leo kwa bahati mbaya hatunayo.Kwa hivyo ni wajibu kwetu kufanya kazi ya kuirejesha tena Khilafah Rashidah ambayo kurudi kwake hakuna shaka kama alivyobashiria Mtume wetu SAAW aliposema:


‘’Kisha itarudi tena Khilafah juu ya njia ya Utume”

Read 588 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…