Sunday, 14 January 2018 00:00

Trump na Mashimo ya Kinyesi

Mwehu, Donald Trump alipoulizwa kwanini Marekani haiwapi hifadhi wahamiaji wengi kutoka Haiti na Afrika, alijibu kwa matamshi ya kifedhuli na matusi kwamba hakuwa na haja ya wahamiaji kutoka “nchi za mashimo ya kinyesi”. Kisha hakusita kutoa hisia zake kwamba anataka wahamiaji kutoka mahala kama Norway. Akikusudia kuwa angependelea wahamiaji weupe kutoka Ulaya badala ya wahamiaji wa kiafrika.

Marekani na Ulaya zimetengeneza utajiri mkubwa kwa kuwatawala kwa ukoloni na kuwafanya watumwa watu wa Afrika na Haiti. Kutoka mwaka 1824 mpaka 1947 Ufarasa iliitenza nguvu nchi ya Haiti kulipa karibu mara kumi ya kipato cha nchi ya Haiti cha mwaka kwa ajili ya kuulipia kinachodaiwa ‘uhuru’ wake. Deni hilo la kujiua la miaka 125 kulipia kinachoitwa uhuru limekiacha kijinchi hiki cha Carribean katika mangamizi makubwa ya kiuchumi. Makampuni ya kimarekani kama Disney yamekuwa yakiinyonya nchi ya Haiti kupitia kuwalipa wafanyakazi wa nchi hiyo kipato kidogo mno ili  kuzalishia  bidhaa nyingi  kwa ajili ya Marekani. Haiti ni mfano hai wa nchi nyingi ulimwenguni zinavyoendelea kuangamia kwa unyonyaji wa ubepari.

Hali ya kuzingatia rangi ya ngozi, utaifa nk. wa wahamiaji ni kielelezo cha kuonesha  wazi  uovu uliokubuhu wa Ubepari na namna unavyowazingatia  wanadamu.

Wahamiaji waliokwenda Madina walikuwa wamo waarabu, waafrika, maskini na matajiri. Kitu pekee kilichowaunganisha na kuwafunga pamoja ni kushikamana  kwao na mfumo mmoja wa Uislamu ambao haukuwagawa wala kuwatofautisha kwa msingi wa rangi za ngozi  wala  msingi wa kipato cha kiuchumi.

Hali ya ubepari kumzingatia mtu kwa mujibu wa rangi ya ngozi yake na hali yake ya kiuchumi inadhihirisha wazi kwamba fikra za ubepari hazipo kwa kila mtu,  bali ni kwa ajili ya watu maalumu wanye daraja ya  ‘wenye  bahati’.

Uislamu ndio mfumo mbadala wa ubepari, ambao unawazingatia wanadamu wote kuwa sawa, awe mtu rangi yoyote atakayokuwa, na kamwe hauwahesabu wengine kwamba ni “nusu watu” wasiostahiki haki ya kuhifadhiwa na maendeleo.

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ (الحجرات: 13

 “Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa mapote na makabila ili mpate kujuana. Kwa hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni aliye mchaMungu zaidi miongoni mwenu.  Kwa hakika Allah ni Mjuzi na Mwenye khabari   [Quran 49:13]

 Imefasiriwa kutoka Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir America

https://www.facebook.com/HTAmerica/

Read 461 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…