Thursday, 22 February 2018 00:00

Kuutukanisha Uislam Kwa Kuitukanisha Dola Ya Kiislam Ya Khilafah Iliyojengwa Katika Njia Ya Utume (Nubuwa) Kwa Kuwatumia Vibaraka Wao

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

Baada ya uamuzi uliotolewa na Tawala ya kidhaalim ya Indonesia ya kuifutia na kuiondolea kibali Hizb ut Tahrir mnamo 19 july 2017, hivyo kupelekea chama kutokubeba ulinganizi wa kiislamu ambalo ni jukumu la chama linalobebwa muda wote la kusimamisha dola ya Kiislamu ya Khilafah,ambayo itatishia mataifa na kuyaondoa kabisa kama hayakuwahi kuwepo.

Na baada ya kushindwa vibaya kwa Tawala dhalimu kuitukanisha Khilafah kama sehemu ya uislamu,kwasababu fikra au wazo kuhusu Khilafah imetagaa (enea)  kwa watu ,na watu hao wanaamini kwamba Khilafah ni msingi na ni sehemu muhimu katika dini yao,Tawala hii dhaalim imejaribu na inaendelea kujaribu kuifuta Khilafah katika mtaala wa kielimu unaotambulika, pia imefuta kabisa matokea ya somo la khilafah mashuleni.

Sio tu hivyo,bali inajaribu kuficha shambulizi lake lililloshindwa kwa kutumia hoja dhaifu za baraza la wasomi wa Indonesia kwa kile kinachoitwa kushikamana na maazimio ya nchi.Tawala hii dhalimu ilijaribu na inaendelea kujaribu kutenganisha kati ya dola ya Khilafah na uislamu kwa kuyatumia  au kuegemea katika maneno ya kibaraka wa kiingereza, Ali Abdel Raziq katika kitabu chake kinachoitwa 'UISLAMU NA MISINGI YA NGUVU ZA KISIASA' ambao mtazamo wake ni kwamba dola ya Khilafah haina misingi katika dini.

Kama azimio la nchi lisemavyo, Waislamu katika sehemu yoyote na muda wowote ni sehemu muhimu sana katika Ummah wa Kiislamu, Ummah wa Muhammad (s.a.w.), ambalo ni Taifa (ummah )bora lilioletwa kwa watu. Ni taifa la muda mrefu ambalo Mtume wa Mungu alilijenga, kiutamaduni na kuliunganisha katika msingi wa Uislamu pekee.

Msingi huu wa kiislamu ni Qur-an na Sunna na ndio kiambatanisho chake. Hili ndilo azimio lake la ulimwengu, tangu Ummah huu ulipokua Ummah Mmoja, uliunganishwa na sera msingi moja ambayo ndo egemezo la Mfumo wake. Taifa hili  sio taifa jipya, sio Taifa lililogawika na lina msingi wake madhubuti, unaoitwa Uislam ambao ni Qur-an na Sunnah, ambao sera yake ndio inayotawala dini. Hivyo basi Ummha huu hauhitajii azimio lolote jipya linaloitwa eti azimio la taifa.

Na kwa kibaraka wa kiingereza, Ali Abdel Raziq katka kitabu chake Uislamu misingi ya nguvu za siasa, mtazamo wake ni kwamba khilafah haina msingi katika dini.

Hili halina mashiko. Kitabu hiki kilichapishwa mnamo April 1925, baada ya Khilafah kuangushwa mnamo march 3,1924 CE/1342 AH, wakati ambao chuo cha Al-azhar nchini Misri kiliongoza juhudi hizi na kuanza shughuli za kisiasa na kidini zenye nguvu zikijadili kuhusiana na Khilafah na kuamua katika hilo.

Na walifikia muafaka kwamba,kunahaja ya kuitisha mkutano wa kimataifa wa Kiislamu ambao utawakilishwa na nchi za kiislamu ambalo litafanyika mjini Cairo chini ya udhamini  na uongozaji wa Al-Azhar.

Kitabu hichi na muandishi wake kimekua kikipingwa vibaya kutokana na kujichanganya kwake na uislamu kwa upande mmoja  na kulenga zaidi kuridhisha sera za kikoloni na tawala za kiislamu kwa upande wa pili.muingereza alihitaji kuifuta kabisa na kuiharibu khilafah na kuharibu kila fikra ya kuirudisha khilafah. Hili ndio lengo la msingi la kitabu kizima. Hivyo ndivyo walivyokua kabla na hivi ndivyo walivyo hivi sasa. Hivi sasa vibaraka wa marekani wanafata nyao zao.

 Kutokana na hichi kitabu, baraza kuu la ulamaa chini ya usimamizi wa Sheikh Muhammad  Abu Al-Fadl, ambae ni Sheikh wa chuo kikuu cha Al azhar alijaribu kwa ushirikiano (jumhuri ulamaa) ya wanachuoni 24 ambao walisema kwamba kitabu hichi na muandishi wake wamechafua dini na dalili zake katika qur-an, sunnah na jamhuri ulamaa. Uchafuzi uliofanywa na kitabu hicho

1. Kimetafsir sharia za kiislamu kama jambo la kiroho pekee halina uhusiano na utawala na mambo mbali mbali ya kimaisha.

2. Eti dini haionyeshi kwamba juhudi za Mtume s.a.w zilikua ni kwa ajili ya kushika Mamlaka (nguvu) tena sio kwa ajili ya dini wala hazikua na lengo la kusambaza ujumbe wake duniani kote.

3  Eti mfumo wa utawala wa Mtume ulikua haupo wazi na sio wenye kueleweka hivyo ukasababisha mtafaruku mkubwa.

4. Lengo kuu la Ujumbe wa Mtumel lilikua ni kutoa ujumbe wa sharia pasi na utawala.

5. Kina pinga jamhuri ya maswahaba ya kuteua kiongozi ambae atasimamia mambo jumla yanayohusu dini katika dunia.

6. Kinapinga vikali kwamba mfumo wa mahkama ni jukumu la kisharia.

7 . Utawala wa Abu Bakr na Khilafah ongofu iliyoendelea baada yake (radhi za allah ziwe juu yao) hazikua ni sehem ya dini. Kulingana na haya,muandishi aliangushwa vibaya na wanachuoni mnao jumatano,22 ya muharram kwa kuchafua uislamu na hakina uhusiano na uislamu.

O enyi watawala na vibaraka,vipi mnajaribu kufuta uongofu wa haki  na kuutenganisha  na uislamu ? Mtume s.a w alisema:

 

«تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلاَفَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

Itakuja nubuwwa kwenu nyinyi pindi Allah akipenda ije, kisha ataiondosha pindi akipenda kuiondosha, kisha itakuja khilafah kupitia njia ya Mtume

(ahmad)

Na yeye Mtume s.a.w ametuamrisha kufata sunnah na Makhalifa wake waongofu waliokuja baada yake:

«عَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِّيْنَ مِنْ بَعْدِي، وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ»

Shikamana na sunnah yangu na njia ya maswahaba wangu waongofu waliokuja baada yangu. Shikilia vitu hivyo kwa meno ya magego (kwa nguvu)."

[Abu Dawood na Tirmidhi]

Sasa unajaribu vipi kuzuia kurejea tena khilafah ? Wakati hiyo ni ahadi ya allah:

 

( وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

Amewaahidi Allah wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda vitendo vizuri kwamba atawapa utawala katika ardhi kama alivyowapa ukhalifa waliopita kabla yao na atawamakinishia dini yao ambayo amewapendelea na atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wananiabudu mimi,hawanishirikishi na chchote, na watakao kufuru baada ya hayo,basi hao ndio wavunjao amri zetu.

[An-Nur:55]

Na ukweli wake Mtume wa Allah (s.a.w):

 

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضًّا فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلاَفَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ»

Kisha ataiondoa pindi akipenda ,kisha utakuja utawala wenye kuumiza pindi Allah akipenda ,kisha atauondoa pindi Allah akipenda ,kisha utakuja utawala wa kidhulma pindi Allah akipenda ,kisha atauondoa pindi akipenda,kisha itakuja khilafah kwa kupitia njia ya Utume"

(Ahmad)

Upingaji wa khilafah ni upingaji wa kitu muhimu sana katika Uislamu,mbali na kwamba ni upingaji wa jukumu muhimu na ambalo ni faradhi kwa uislamu. Hii ni kwa sababu khilafah ni jambo kubwa katika Ummah mzima ambao ni pamoja na watu wa Indonesia, khilafah ndio chanzo cha  uimara wake ,nguvu na urejeshwaji upya wa taifa, na itakua ni taifa moja katika dunia, na halitapingwa ila kwa wale waliokhasirika.

O waislamu,O wasomi wazuri,O wazee mnaoheshimika,na nyote mlio na nguvu na ushawishi,shikamaneni na sunnah ya mtume wenu,mwenendo wa makahalifah wake waongofu waliokuja baada yake,na mzishike kwa magego,haswa masikua haya ya fitna(uasi),isipokua wale waliokatika rehma na huruma ya allah wataongoka.kusikiza allah anavyosema:

( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

  Enyi mlioamini itikieni ,mjibuni Allah na Mtume pindi wanapowaita kwa kile kinachowapa uhai mzuri.

[Al anfal:24]

6 Jumada I 1439 AH

Hizb ut Tahrir/ Indonesia

 

Read 319 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…