Siasa

Siasa (29)

Friday, 14 April 2017 00:00

Bila ya Khilafah ni Utumwa na Dhulma-3

Khutba ya Ijumaa 17 Rajab 1438 Hijri / 14 Machi 2017 Miladi

Wakati tukiendelea kuikumbuka dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyoangushwa ndani ya mwezi huu wa Rajab, lazima tukiri kuwa kuangushwa kwake kumesababisha kukosekana amani, usalama na utulivu kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii na wanadamu kwa jumla.  Wawe watu wa dini nyengine, wanawake, wafungwa, wakimbizi nk. Khilafah ilisimamia haki za makundi yote kwa uadilifu, insafu na kwa mafanikio ya hali ya juu.

Leo tunashuhudia Waislamu kuteswa na kuuliwa kwa ukatili usioelezeka ndani ya Afrika ya Kati, Burma, India nk. Pia tunaona namna dola ya Misri inavyoshindwa kusimamia usalama wa wakiristo wa madhehebu ya kibti (coptic) kiasi cha karibuni kuripuliwa kwa mabomu na kuuliwa wafuasi wa kanisa hilo karibu 50. Wakati hayo yakijiri ilikuwa ndani ya Rajab (28 Hijria/ 638 miladi) baada ya dola ya Khilafah kuukomboa mji wa Aelia na wakaazi wake kwa ridhaa ya nafsi zao chini ya Askofu wao Mkuu Bwana Sophronius  kuridhia bila ya mapigano, Khalifa Umar ra. binafsi alifunga safari ndefu kuja kushuhudia qadhia ya watu hao, na akaandika waraka mtukufu wa kihistoria unaosomeka:“Kwa jina la Allah, Arrahman, Arrahiym : Huu ni waraka wa mkataba kutoka kwa Umar, mtumwa wa Allah, kiongozi wa Waislamu, kwa watu wa Aelia. Anadhamini usalama wa maisha yao, mali zao, makanisa yao na misalaba yao…Makanisa yao yasivunjwe wala yasiondoshwe, na kisiondoshwe chochote katika vitu vyao. Wasilazimishwe katika mambo ya dini, na asidhuriwe yoyote……”

Pia itakumbukwa katika zama za Khalifa Mu’utasimu bil-llah (750-754 miladia) askari wa kiroma alipomdhalilisha mwanamke wa Kiislamu kwa kumvua hifadhi yake(hijabu), na mama huyu kupiga mayowe kwa kunadi  yaa Mu’utasimu (ewe Mu’utasimu) upo wapi mimi nadhalilishwa ! Kwa haraka Khalifa bila ya ajizi akaandaa jeshi la Waislamu kuwatia adabu waroma na kumkomboa mwanamke huyo.  Khalifah huyu alifariki akiwa mdogo wa umri wa miaka 45 tu, bali tukio hili limekuwa ni kito cha thamani katika tareekh.

Wakati leo wakimbizi wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu wakipewa daraja ya kuliko wanyama katika nchi mbalimbali duniani, ilikuwa ndani ya mwezi Julai 1492, wakati Waislamu na mayahudi walipokuwa wakifukuzwa kwa agizo maalumu la serikali ya Spain (Spanish Inquisition) Khalifah Bayezid II alituma manuari maalumu chini ya Kamanda Kemal Reis kuwaokoa Waislamu na mayahudi, na akawapa hifadhi ya ukimbizi mayahudi zaidi ya 150,000    http://ilmfeed.com/when-the-islamic-state-saved-150000-jews/

Enyi Waislamu na Wanadamu kwa jumla : Sote ni mashahidi kwa matukio ya uovu wa magereza ya kimataifa kama Guntanamo, Abu Ghuraib, Bagram nk. namna wanavyodhalilishwa Waislamu kwa kufanyiwa vitendo viovu visivyoelezeka. Na kwa upande wa kitaifa hali ni hiyo hiyo. Ni Waislamu wangapi hapa Tanzania wamenyakuliwa na hakuna taarifa zao. Kiasi cha hata maiti zilizokutwa zikielea mto Ruvu pia ni za Waislamu. Hali hiyo imekithiri kiasi cha pia kuwahusisha hata wasiokuwa Waislamu akina Ben Sanane na wenzake, hadi uovu wa utekaji kuibuliwa kuwa ni ajenda ndani ya Bunge! Hali ambayo kwa muda mrefu imekuwa ni ya kawaida kwa Waislamu. Ni wangapi wanaouchukuliwa hadharani au kwa kificho, kuteswa, kudhulumiwa, kunyanyaswa bila ya maelezo wala sababu, huku wengine hawarudi tena, na wanaorudi wakiwa hawajiwezi kwa mateso na dhulma

Enyi Waislamu na wanadamu kwa jumla:

Chini ya mfumo batil wa kidemokrasia hakuna atakaesalimika awe Muislamu au mwengineo kwa kuwa ni mfumo uliojengwa juu ya kipimo cha maslahi, kupupia madaraka na kushikilia fikra za Machievelli za “fanya lolote kufikia lengo lako”. Basi ni wajibu kwa Waislamu kushiriki katika mchakato wa kuirejesha Khilafah itakayoanzia katika nchi kubwa ya Waislamu ili kuwakomboa Waislamu na wanadamu kwa jumla. Na kwa wasiokuwa Waislamu waanze kutafiti mfumo mbadala kando na demokrasia.

Tunamalizia kwa kusema ‘Bila ya Khilafah wanadamu watazongwa na Utumwa na Dhulma zisizokwisha.

http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Tuesday, 11 April 2017 00:00

Uharamu wa Kusheherekea 'PASAKA'

Baadhi ya aya za kutumia 4:156-158   4: 171-172   na aya nyengine zozote utakazoona zinafaa kwa munasaba wa qadhia hii.

Nini Ijumaa Kuu,

Siku hii pia huitwa Ijumaa takatifu ni siku ambayo wakristo wanaitakidi kwamba ndio siku aliyosulubiwa Isa As, baadae akazikwa, na siku ya Jumapili akafufuliwa (Jumapili hiyo ndio huitwa Jumapili ya Pasaka) (Weka neno ‘Good Friday’ katika Goggle utapata ufafanuzi zaidi kuhusu hili)

Matukio haya ya Easter japo kwamba  ni yenye kukubalika katika dini ya kikiristo, katika Uislamu hatuyakubali kwa sababu:

1.Ukiristo si dini ya haki

2.Mtukio haya  yamekanushwa na Quran.

Nini hukmu ya kisheria juu ya kusherehekea, kuadhimisha au kuhuzunika na tukio hili ?

Ni Haramu, kwa sababu:

      1.Aqeeda ya Kiislamu imeweka  wazi zipi sherehe zetu. (Rejea hadithi  juu ya sikukuu zetu)

      2.Kama matukio haya yangetokea tungeelezwa, kwa kuwa tumeambiwa tufunge siku ya Muharram kwa munasaba wa kuangamizwa Firaun na kuokolewa          Mussa As.

Jee inajuzu kujumuika katika sherehe za michezo mbalimbali katika mchakato wa sherehe hii ya Pasaka hata kama huitakidi chochote katika dini ya Ukiristo?

Jambo hili pia ni Haramu. Pamoja na kwamba michezo kwa asili yake ni  ‘mubaha’ lakini kwa vile  hapa linaingiliana na hadhara ya kikiristo, kama vile ilivyo tiba ya Babu wa Loliondo ilivyonasibishwa na hadhara ya kikiristo. Kwa hivyo, ni Haramu isiyo na shaka. (Rejea mada ya Madania na hadhara katika kitabu chetu cha Nidhamu-ul-Islam)

Nini hatari ya Waislamu kujumuika katika wimbi la kusherehekea Pasaka au sherehe nyengine zote za kikafiri kama X-mass na nyenginezo?

1.Kunaimarisha fikra hatari ya dini mseto (Rejea kitabu chetu cha ‘Fikra hatari za kushambulia Uislamu’)

2.Kuwazoesha (normalize) Waislamu na thaqafa ya kikafiri.

3.Kuondosha msukumo wa Waislamu kuwaona makafiri maadu

4.Kupelekea kuzorota au kuacha kabisa jukumu la kuwalingania makafiri. Kwa kuwa watawachukulia kama wenzao wasio na tishio lolote.

Katika hali kama hii nini wajibu wa Umma wa Kiislamu?

  1. Kuweka wazi na kufedhehi uwongo huu. Kwa kuwa Allah Ta’ala katuonesha mfano wa jambo hilo, na kuigonga itikadi ya kikiristo juu ya uovu wao.
  2. Kuwalingania Wakiristo waje katika haki. Lazima tufanye mgongano wa hadhara baina ya Uislamu wetu na kila aina ya ukafiri.  Kwa kuigonga kila dini batil kama hii ya Ukiristo na fikra zake kama hii ya Easter na nyenginezo. Pia kuugonga mfumo wowote na  fikra zozote batil.  Kama ubatil wa  wa mfumo wa Ubepari fikra zake za  uhuru, haki za binaadamu, usawa wa kijinsia nk (Rejea kitabu chetu ‘Kutokuepukika migongano baina ya hadhara’)
  1. Aidha, kufedhehi fikra ya dini mseto na wale wanaoipigia debe ambao hudai  kwamba dini hizi zinatokana na chimbuko moja na msingi mmoja. Katika hilo  lazima tuoneshe  wazi wazi uovu wa fikra hiyo. Pia  tuwakumbushe Waislamu wanaohubiri dini mseto na ukuruba baina ya dini kwa mfano hai wa hali tuliyonayo  namna  wakiristo walivyokuwa hawajali wala hawatambui  fikra hiyo. Hilo linadhihirika wazi wazi katika msimamo wao wa kupinga na kuzuwa uongo mkubwa juu  ya  suala la mahkama ya qadhi. Licha ya kutambua viongozi hao wa makanisa kwamba mahkama hiyo haina athari ya udhati. Lakini kutokana na uadui wao wanaipinga na kueneza propaganda chafu makanisani. Ni kutokana na hilo ndio pia Makanisa  yametoa waraka maalumu kupinga  bila ya kujali  kile kinachoitwa umoja na ukuruba baina ya dini hizi. Kama wanavyolipigia kifua suala hili baadhi ya masheikh maslahi.
  2. Pia lazima tuoneshe namna makanisa yanavyokuwa mstari wa mbele kutetea nidhamu ya  kidemokrasia na katiba zake. Kwa kuwa mambo hayo  yanatokana na ukafiri kama wao. Na kwa kuwa ukafiri ni mila moja.  Wakiristo wanashika misimamo hiyo na kuipigia debe  ilhali wakijuwa wazi kwamba siasa za kidemokrasia, chaguzi zake  na katiba zake  zipo kinyume na Uislamu. Lakini katika hilo kamwe Wakiristo  hawaungani na mtazamo wa Uislamu. Bali kinachotokezea ni  baadhi ya Waislamu  amma kwa  kuanguka kwao kifikra au kwa maslahi ndio huungana na Wakiristo katika kuunga mkono vyama vya kidemokrasia, siasa  zake na katiba zake. Na kamwe wakiristo hawafuati msimamo wa Uislamu ambao ni kupinga  mambo hayo.
  1. Pia tuwakumbushe Waislamu kuwa hata kama baadhi ya Viongozi wa makanisa wakionekana kutofautiana katika  suala la katiba pendekezwa kama inavyoonekana sasa  mvutano uliopo  baina ya Askofu Pengo na  Mchungaji Gwajima. Kimsingi kinachodhihirika hapa ni uadui wa kimaslahi tu baina yao.  Lakini  kimsingi hawapingi katiba kwa udhati wake.  Bali wanachotofautiana ni  mbinu bora zaidi na  uboreshwaji katika  mchakato wa upatikanaji wa katiba hiyo. Kwa hivyo kimsingi viongozi wa makanisa  kamwe huwa hawapingi nidhamu ya kidemokrasia katika msingi wake. Bali daima husimama nayo bega kwa bega. Kwa kuwa ni ukafiri kama wa dini yao, na ambao uko kinyume na Uislamu.

Katika muongozo huu ni muhimu kwa mzungumzaji kuongeza katika ufafanuzi wa aya zaidi, hadithi zaidi za Mtume saaw, matukio katika sira na  mifano hai ya waqia ili kuifanya mada kuwa na mvuto zaidi. Pia mada zifuatazo zitasaidia zaidi:

Tuesday, 11 April 2017 00:00

Ukafiri wa Pasaka

HAWAKUMUUWA WALA HAWAKUMSULUBU 

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَكِنْ شُبِّهَ لَهُمْ

“Na kauli yao ya kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi  Issa , mwana wa Maryam, Mtume wa Mungu” hawakumuuwa wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa mtu mwengine….”

(TMQ 4: 157)

Suala la kuanguka kifikra, kuchanganyikiwa na kutekwa na fikra za kikafiri miongoni mwa Waislamu limepelekea baadhi ya Waislamu kushindwa kutofautisha baina ya fikra ya ‘Madania na Hadhara’ ambayo hufafanua wazi ni mambo gani Waislamu huruhusiwa kuchukuwa kutoka kwa makafiri na mambo gani haturuhusiwi kuchukuwa. (Rejea makala yetu ya hadhara-na-madaniya )

Hali hiyo imewafanya baadhi  ya Waislamu kujitumbukiza katika maadhimisho ya siku kuu za kinaswara na nyenginezo kama hii inayotukabili ya Pasaka. Kwa mfano, Tanzania Bara na Visiwani kwa miaka mingi kumekuwa na ziara za kimichezo kwa munasaba wa Pasaka. Ziara  ambazo kihukmu kwa Muislamu ni haramu kushiriki au kuchangia. Kwa kuwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kinaswara inayonasibishwa na kusulubiwa kwa Issa As. kufa  na kufufuka.

Ajabu inayodhihirika hapa ni badala ya Waislamu kuitumia fursa ya Pasaka kufedhehi waziwazi  na kuugonga udhaifu wa dini ya kikiristo katika misingi yake na kuwalingania wakiristo kuja ndani ya Uislamu kwa hoja za quran na dalili za kiakili, baadhi ya Waislamu kimakosa au makusudi  hujumuika na manasara katika maadhimisho hayo haramu.

Uislamu kwa kuwa ni dini ya haki mapema sana ilianzisha mapambano makali ya kifikra baina ya haki na batil. Na kwa upande wa dhidi ya unaswara unagonga kwa nguvu na makemeo makali misingi yote inayosimamia dini hiyo. Kwa kuonesha waziwazi kwamba ni misingi dhaifu, uwongo na batil. Kamwe Uislamu haukupaka mafuta  katika suala hilo, ili manasara wauone waziwazi udhaifu huo waache dini hiyo batil  na waingie katika dini ya haki ya Kiislamu. Wajibu huu wa kuigonga haki juu ya batil ndio msimamo ambao  Waislamu  daima tuna wajibu kushikamana nao. Amma ikiwa dhidi ya vidini vya kiroho kama ukiristo, uyahudi, uhindu ubudha nk. Au dhidi ya mifumo batil isiyo na haja ya dini kama ukomunisti ulioanguka kimataifa au udemokrasia/ubepari unaoendelea kumtia mashaka mwanaadamu kila uchao.

Quran inatamka wazi kwa kinywa kipana na bila ya lugha ya mzunguuko wala kupaka mafuta juu ya uwongo na upotofu wa fikra zote msingi zilizojengewa dini ya kikiristo. Kuanzia fikra tata  ya utatu, uwongo wao kuhusu uzawa wa Issa As, fikra zao potofu juu  ya  mwanamke mwema bi Maryam As. pia ikagonga kwa ukali upotofu wa madai yao ya kusulubiwa kwa Issa As. ati  kasulubiwa kufidia dhambi zao. Aidha, Quran ikatangaza bayana kwamba  msimamo wao huo wa kusulubiwa Issa As.ni uwongo shahir dhahir.

Uislamu unayafanya mapambano yote haya ya kifikra kwa kujitosheleza kwa hoja waziwazi na kunadi hadharani kwamba  manasara wamekwenda kombo na dini yao ni ukafiri usio na shaka.

Kwa hivyo, ikiwa misingi ya dini na imani ya kikiristo yote imejengwa juu ya msingi mbovu wa  uwongo na batil ina maana pia kwamba  vyanzo inavyovitegemea dini hiyo kuvua na kupata mafunzo yake pia ni batil na si vya kutegemea. Katika hali kama hiyo wakiristo watakuwa na chaguo moja katika mawili. Amma waache dini hiyo mara moja waingie dini nyengine ya haki. Au watafute vyanzo vya kuaminika kuhusiana na imani waliyonayo. Lolote watakaloshika katika mawili hayo watalazimika waingie katika Uislamu.

Tunapoangalia tareekh ya Kiislamu kwa makini  tutaona ndani mwaka wa nne wa Utume  viongozi wa kiutawala na wakinaswara ndani ya Ethiopia/Uhabeshi walikinai kwamba Quran ni chanzo cha kutegemea, wakati  iliposomwa mbele yao na sahaba Jaafar bin Abu Talib Ra. Ndani ya kasri yao kufafanua baadhi ya fikra ambazo manaswara wamezipotosha. Watawala hao na viongozi wa kinaswara walifanya unyenyekevu mkubwa kiasi cha kutiririkwa na machozi na baadhi yao kusilimu. Pia msafara wa wakiristo wa Najran uliokuja kwa Mtume SAAW ndani ya mwaka wa tisa ulikataa kusimama kufanya kiapo cha laana na maapizano (mubahala) baina yao  na Mtume SAAW. Hizi zote ni dalili za manaswara kukinai vyanzo vya kweli vya Uislamu.

Changamoto ya Waislamu leo hususan kwa minasaba ya siku kama hizi za maadhimisho ya kinaswara ni kuwakabili wakiristo hususan ‘wakiristo makini’ kuwaonesha udhaifu katika misingi ya imani yao na udhaifu wa vyanzo vya mafunzo ya imani hiyo ambavyo kamwe haviwezi  kuinusuru imani hiyo. Kwa kuwa kitabu chao hakitokani na Muumba. Na ukweli kuwa kitabu chao si cha Mungu hata wao wanaukiri. Kwa kuwa kitabu cha mungu, lazima kibakie katika lugha yake ya asili kilivyoteremshwa, kisiwe na mabadiliko kwa kuingizwa mikono ya binaadamu na asiweze mwanaadamu kutoa mithili yake kwa lugha na maudhui. Sifa hizo kamwe haziwezi kupatikana katika kitabu chochote duniani isipokuwa Quran. Katika hali hiyo wakiristo wangepaswa kutegemea kupata taarifa sahihi za kidini na mengineyo kwa ukweli, uaminifu na  ukamilifu kutoka ndani ya Quran. Wakiristo wakilikubali hilo ambalo hana budi kila mkiristo makini kulikubali, maana yake pia hawatokuwa na sababu ya kukikataaa kila kilichomo ndani ya kitabu hicho. Kwa kuwa wameshakinai kwamba ni kitabu cha haki. Basi wakati huo hawatokuwa wakiristo tena, bali watakuwa Waislamu. Kwa kuwa wamekinai  ukweli wa kitabu cha Quran.

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلاَّ نَعْبُدَ إِلاَّ اللَّهَ وَلاَ نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلاَ يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ (آل عمران: 64).

“Sema: Enyi watu mliopewa  kitabu (mayahudi na maswara)! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu: ya kwamba tusimwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Wakikengeuka , semeni shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu”

(TMQ 3:64)

 

Friday, 07 April 2017 00:00

Bila ya Khilafah ni Utumwa na Dhulma-2

Written by

 

 Khutba ya Ijumaa 10 Rajab 1438 Hijri / 07 Machi 2017 Miladi

 BILA YA KHILAFAH NI UTUMWA NA DHULMA -2

Alhamdullilah !  tumeingia Ijumaa ya pili ya mwezi mtukufu wa Rajab 1438.  Mwezi ilipoangamizwa kwa uadui dola ya Kiislamu ya Khilafah na kuuwacha Umma wa Kiislamu na wanadamu kwa jumla katika kiza totoro cha utumwa na dhulma.

Miongoni mwa msiba, utumwa na dhulma baada ya kuangushwa Khilafah ni katika upande wa kielimu. Vibaraka waliokabidhiwa kusimamia Waislamu baada ya ardhi za Waislamu kumegwa vipande vipande  walipatiwa sera ya kikoloni ya kielimu isiyomuandaa mwanafunzi kuwa huru kifikra wala kumjengea ubunifu. Sera hiyo inawafanya Muislamu na wanadamu kwa jumla kubakia kuwa watumwa, kuipupia dunia na kuitupa akhera na wasomi kujiona ni watu wa tabaka maalumu.  Ni elimu ya kuwaandaa Waislamu na wanadamu kuwa watumishi na watetezi bila ya hoja mfumo wa kibepari. Ni elimu isiyokuwa na meno ya kuwafanya wanafunzi kuwa  wavumbuzi, kwa kuwa kiasili nchi zao haziko huru, ambayo ndio nyenzo ya kimsingi katika hilo.  Matokeo yake wanafunzi hukaririshwa namna wengine walivyofikiri na sio kufanywa wao wafikiri. Wakoloni katika masomo ya kithaqafa (arts) wanawahifadhisha wanafunzi shehena ya nadharia za wanafikra wao. Matokeo yake wanaoitwa wasomi wa masomo ya kithaqafa (arts) hawana zaidi ya kukariri kama kasuku nadharia za kimagharibi. Na wanaosoma sayansi hubakia kusoma historia ya wavumbuzi badala ya wao kuvumbua. Pamoja na ubovu wa elimu hiyo pia ikageuzwa kuwa biashara ya gharama kubwa. Ripoti ya 2014 ya Shirika la UNESCO imebainisha kuwa zaidi ya watu milioni khamsini katika ulimwengu wa Kiislamu hawajui kusoma na kuandika. Aidha, robo ya watu wote katika nchi zinzazoendelea hawajui kusoma na kundika! Licha ya utajiri na rasilmali zilizomo ndani ya nchi za Kiislamu raia wametumbukizwa utumwani na kudhulumiwa waziwazi kwa kukosa elimu. Hiyo ni hasara kwa Waislamu na wanadamu kwa kuwa elimu leo ni biashara asiyoweza kumudu kamwe mtu mnyonge.

Dola ya Kiislamu ya Khilafah zama zote ilijifunga na mwenendo wa Mtume SAAW kwa kuipa elimu kipaumbele kwa kuwa ni uti wa mgongo, uhai na nyenzo muhimu kuilinda aqeedah ya Uislamu. Kama Mtume SAAW alivyowatuma maswahaba wawili kwenda kuchukua teknologia ya utengezaji wa silaha kwa bingwa  Jurash wa Yemen, Pia ni Khalifah Umar ibn khatwab ndiye aliyeanzisha teknolojia ya kutengeneza manowari. Aidha, makhalifa waliokuja waliwekeza katika elimu kiasi cha ulimwengu wa Kiislamu kumiliki miongoni mwa vyuo vikuu vya mwanzo vyenye hadhi kama Baitul-Hikma ndani ya Iraq na chuo kikuu cha Al-Qarawiyyin ambacho miongoni mwa wanafunzi wake ni Papa Sylvester II wa Kanisa Katoliki. Hali hii iliifanya Khilafah kuwa dola kuu sio tu kifikra na kijeshi bali katika nyanja zote za kielimu kwa zaidi ya karne kumi. Zama ambazo 95% ya watu wa Ulaya hawakujua kusoma wala kuandika! Leo mambo yamegeuka juu chini. Msiba na dhulma unaopaswa kufutiliwa mbali.

 

Enyi Waislamu na wanadamu,

Kama zilivyofanya Khilafah zilizotangulia katika elimu ndio itakavyofanya dola ya Khilafah itakaporudi na kuzidi mafanikio yaliyopita InshaAllah. Itazitumia rasilmali na utajiri mkubwa uliopo kufikia lengo hilo.  Itawekeza katika kuifinyanga haiba ya mwanafunzi na kuzalisha wabunifu na fani mbali ili kuhamasisha uvumbuzi. Utaijenga elimu juu ya utulivu wa nafsi na kuepuka shehena ya nadharia ambazo hazina uhalisia wowote. Kubwa elimu itasimamiwa na dola huru isiyoingiliwa katika mambo yake wala kupangiwa sera na madola ya kikoloni.

http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

 

Page 1 of 2
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…