Friday, 24 March 2017 00:00

Shujaa si Nape wala Serikali.

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Mfumo wa kidemokrasia na udikteta ni pande mbili za sarafu moja. Mtawala kwa ujanja ujanja hujifanya yuko na watu, mzalendo, anajali katiba na mtumishi wa raia akighilibu wasio na uoni. Lakini matakwa na maslahi yake na ya wapambe wake yanapohatarika hata huo ujanja huweka pembeni na hutumia nguvu, kibri, jeuri na mabavu waziwazi hadharani kulinda matakwa yake.  

Shujaa sio yule alietetereshwa baada ya kufaidika, kujijenga na kudhulumu raia kwa mfumo huo huo hadi kusahau maumbile ya nidhamu ya kisiasa ya mfumo huo kuwa ni nidhamu ya maslahi, husuma na makundi.  Licha ya kuwa na yeye kuwamo humo humo ndani ya makundi hayo, na suluhisho lake ni kubakia kuogelea ndani ya tope hizo hizo chafu.

Bali shujaa wa kweli ni yule anayeupinga mfumo mzima wa kibepari na nidhamu yake batil ya kidemokrasia katika msingi wake, kwa kuwa ni nidhamu ya uwongo (kimaumbile hakuna utawala wa watu), chanzo cha migogoro na haukinaishi kwa hoja za kidini wala  kiakili, na badala yake kutandika au walau kutafiti mfumo mbadala kwa ajili ya ukombozi wa kweli wa wanadamu wote.

24/03/2017

Khilafah ndio Suluhisho

Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Tanzania

Read 2052 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…