Wednesday, 29 March 2017 00:00

Mahkama za Watoto Zanzibar sio ufumbuzi

Written by 
Rate this item
(0 votes)

                    

 

MAHKAMA ZA WATOTO ZANZIBAR SIO UFUMBUZI

Mwanzoni mwa mwezi wa Januari Raisi wa Zanzibar alifungua mahkama maalumu ya watoto ya Mkoa wa Kaskazini. Mahkama hiyo itahusika na kesi za udhalilishaji kwa watoto.

Kuanzishwa kwa mahakama hii maalumu ni dhihirisho jengine la kufeli kwa mfumo wa sheria za kibinadamu, hata waanzilishi wakiwa na lengo zuri, na pia yamaanisha kuwepo uelewa duni wa hali halisi ilivyo, kwani wapi sheria za kibinadamu zimefaulu? si kila siku sheria mama(katiba) zinabadilishwa ili kukidhi hitajio la wakati.

Hili ladhihirisha kuwa mwanadamu ni mdhaifu na mpungufu na ni lazima anyenyekee kwa aliyemkamilifu asiye na ila wala kasoro ambaye si mwengine bali ni Muumba, Allah SW.

Kuanzishwa kwa mahakama hii maalumu ya watoto huko Mahonda ni danganyatoto kwani mahakama zilizokuwa zikiendesha kesi hizo awali hazikuwa na maendeleo mazuri katika kufikia uamuzi kutokana na ucheleweshaji mkubwa mbali maamuzi ya tatanishi.

Kuanzishwa mahakama maalumu haitasaidia chochote kwa kuwa mahakimu na majaji ni walewale ambao kusikiliza kesi hizi ni sehemu ya miradi ya kuwaingizia mapato, hivyo mdhalilishaji akiwa na hela haingii hatiani.

Pia kwa kuwa sheria za mahkama hizo ni za binadamu zisizounganisha  upande wa kiroho, kuhisisha na mambo yote Muumba, hivyo kimaumbile unyenyekevu wao utakosekana au utakuwa dhaifu kwa kuwa waliotunga sheria hizo ni wanadamu  kama wao. Kinyume na Uislamu ambapo watu wote huwa waangalifu kwa matendo wayafanyayo kwa kuwa kila kitendo ni ibada hivyo mtu anayakini akifanya udanganyifu atakwenda kuulizwa siku ya Kiama. Na kamwe matendo hayaishii hapa duniani.

Vilevile kuazshisha mahakama maalumu za watoto si suluhisho kwani kimsingi tatizo la udhalilishaji si la watoto, bali kwa udhati wake ni tatizo la binadamu. Hivyo, ufumbuzi wake lilikuwa likabiliwe kwa upana kwa kumuangalia binadamu kwa upana wake. Aidha, linapaswa kuekewa mikakati ya kinga ili lisitokee. Leo tunaona wakati kunaanzishwa mahakama kama hizi, bado wapo watu maarufu katika jamii ambao ni watendaji na watendwaji wa vitendo vya ngono za jinsia moja ilhali hawachukuliwi hatua yeyote. Matokeo yake wakuwa ni kigezo (role models) kwa watu wengine kuwaigiza.

Ni wajibu majaji,mahakimu na watu jumla kufahamu pasina shaka kuwa  uadilifu pekee unapatikana kwa kufuata muongozo wa Allah SW si vyengine, na ni haramu, pia yaweza kuwa kufru kuamini uadilifu nje ya Uislamu.  

Amesema Allah SW katika Surat Al-hadiid aya 25.

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنْزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ َ

“Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu na ubainifu, tukawateremshia kitabu na mizani (sharia) ili wawasimamie watu kwa uadilifu…”

 

Risala Ya Wiki No.283 

28 Jumada al-thani 1438 Hijri | 27/03/ 2017 Miladi

http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

 

 

 

 

 

Read 1965 times Last modified on Wednesday, 29 March 2017 09:51
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…