Friday, 31 March 2017 00:00

Ijue Kampeni Maalum ya Rajabu 1438/Machi-Aprili 2017 Hizb Ut-Tahrir Tanzania.

IJUE KAMPENI MAALUMU YA RAJAB 1438/MACHI-APRILI 2017

HIZB UT-TAHRIR TANZANIA

 

Nini kampeni maalumu ya Rajab?

Hii ni kampeni maalumu na pana itakayoongozwa na vijana wa Hizb ut Tahrir Tanzania kwa mashirikiano na Umma  mzima ndani ya mwezi huu wote wa Rajab ikibeba kauli mbiu ya“Bila ya Khilafah ni Utumwa na Dhulma”

Kwanini kampeni hii ndani ya Rajab?

Kampeni hii inafanywa zaidi ndania ya mwezi huu wa Rajab kwa sababu mwishoni mwa mwezi huo mwaka 1342 /Machi 1924 ndipo mabakibaki ya dola ya Kiislamu ya mwisho (Khilafah Uthmania)  yalimalizwa rasmi,  baada ya hila, vitimbwi na mikakati kabambe ya makafiri hususan dola ya Uingereza kwa msaada wa khiyana kubwa kutoka kwa vibaraka wao miongoni mwa waturuki na waarabu.

Jee Kampeni hi inalenga nini?

Kampeni hii ina dhamira kama ilivyo kauli mbiu yake. Pamoja na kugusia mambo mengine kama kuwakumbusha Waislamu uwepo wa dola ya Kiislamu ya Khilafah ndani ya fiqhi ya Kiislamu, uwajibu wa kutawaliwa kwa dola hiyo, mambo ambayo makafiri wanafanya kazi usiku na mchana kuwasahaulisha. Bali kubwa zaidi kampeni hii inalenga kujikita zaidi katika kuonesha kwa hoja na mifano hai ya kitareekh na hali ilivyo kwamba tangu kuangushwa dola ya Kiislamu ya Khilafah Waislamu na walimwengu kwa jumla wameendelea kugubikwa na kila aina za utumwa kuanzia wa kiakili, kisiasa, kiuchumi nk. Hali inayoambatana pia na dhulma zisizo na mfano kwa sura zake zote. Hii ikimaanisha kwa Waislamu wafanye kazi kuirejesha dola hiyo ndani ya nchi kubwa za Waislamu ili kuwakombowa Waislamu na wanadamu kwa jumla. Na kwa wasiokuwa Waislamu ambao hawajawa tayari kuwa Waislamu, walau waufahamu ukweli na uadilifu wa dola hiyo kinyume na fikra za kiuadui zinazopigiwa debe na madola maadui wa Uislamu na Waislamu yakiongozwa na Marekani.

Jee Kampeni hii itazinduliwa lini na wapi?

Kampeni hii itazinduliwa rasmi siku ya Ijumaa 03 Rajab/ 31 Machi 2017 Masjid Rahma , Buguruni kwa Madenge mara baada ya Swala ya Ijumaa.

Jee Kampeni hii itahusisha mambo gani mengine?

Kampeni itahusisha mambo kadhaa kama mihadhara, khutba za ijumaa, mijadala ya wazi, utawanyaji vipeperushi, maongezi nje ya misikiti, utawanyaji wa makala katika mitandao ya kijamii, tovuti, utumaji wa makala magezitini nk.

Jee Waislamu wana wajibu gani juu ya kampeni hii?

Kampeni hii licha ya kuongozwa na vijana wa Hizb ut Tahrir Tanzania lakini kimsingi sio kampeni yao bali wao wako mbele tu kuwaonesha Waislamu njia. Kwa kuwa qadhia ya kutawaliwa na Khilafah sio qadhia ya Hizb ut Tahrir bali ni  qadhia ya Umma mzima wa Kiislamu. Pia dola ya Kiislamu sio milki ya Hizb ut-Tahrir bali ni milki ya Umma mzima.

Jee kuna mwito gani kuhusiana na kampeni hii?

Mwito wetu kwa Umma mzima kuanzia masheikh,maustadh, walimu, wasomi na wanafikra jumla kushiriki kikamilifu katika kampeni hii adhimu ambayo inawakumbusha Waislamu juu ya suala zito na nyeti la kurejesha izza/ nguvu yao na kuukomboa ubinadamu. Kuna namna mbalimbali ya kushiriki katika kampeni hii kama kuchangia mawazo na fikra katika kuifanikisha, kushiriki shughuli mbalimbali kama mihadhara, mijadala, kutawanya mitandaoni/share, kuitangaza kwa wengine nk. 

Tunachukua fursa hii kuwakumbusha makhatibu na wahadhiri duniani kote kuifanya mada hii kuwa mada kubwa,  pamoja na kuwa tusiyasahau matukio mengine ndani ya mwezi huu wa Rajab kama Israi na Miiraj, ushindi wa Salahuddiin nk.

Tunawaomba Waislamu wote wawe tayari kushirikiana nasi katika kampeni hii adhimu kwa kutupatia fursa katika misikiti, vyuo, madrassa na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kampeni hii.

Mwisho,  tunawaomba katika mashababu wa Hizb na Umma mzima, kwa wenye uwezo wa kuandika makala mbalimbali waandike kuilenga kauli mbiu ya kampeni hii na kuifafanua ili kuamsha Umma wa Kiislamu na wanadamu jumla juu ya hali ya utumwa na dhulma zilizoenea duniani kote kutokana na kukosekana kwa dola tukufu  ya Khilafah.

Tunaomba sana mashirikiano yenu. Ukipata ujumbe (tawanya/ share) kwa wengine.

 

02 Rajab 1438 Hijri / 30 Machi 2017 Miladi

 

Masoud Msellem

Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania.

 

 

Read 3349 times

Media

Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…