Friday, 31 March 2017 00:00

Matukio Munasaba Mwezi Rajab

Written by 
Rate this item
(0 votes)

MATUKIO MUNASABA MWEZI WA RAJAB

1.Hijra ya Uhabeshi.

Mtume SAAW aliwaruhusu  baadhi ya masahaba kuomba hifadhi ndani ya nchi ya Uhabeshi/ Ethiopia kufuatia mateso ya Maqureish. Waliondoka Waislamu 16 wanaume, na wanawake 2. Akiwemo Uthman bin Affan Ra. na mkewe Bi Ruqayah bint Rasullulah SAAW.

2.Kufariki kwa bwana Abuu Twalib

Ami yake Mtume SAAW aliekuwa ngome iliyokuwa ikimkinga na kumuhami dhidi ya maqureish, alifariki akiwa na umri wa miaka 82 (Tukio hili ama lilitokea katika Rajab au Ramadhan Mwaka wa 10 wa Utume)

3.Safari ya Israi na Miiraj.

Hii ilikuwa ni safari ambayo Allah Taala alimpeleka  Mtume SAAW kumliwaza baada ya kuondokewa na watu nyeti na kumpa nguvu kufuatia upinzani wa maqureishi. Pia ilikuwa ni bishara ya ushindi ambapo mara baada ya kurudi alipewa baayah ya kwanza iliyozaa baaya ya pili iliyopelekea kupata nusra.

4.Kutumwa kikosi cha Nakhlah.

Kikosi hiki kilitumwa chini ya uongozi wa Abdallah bin Jahshi Al-Assad na askari 12 wa muhajiriina kwenda katika mji wa Nakhlah ili kukusanya habari na kuitisha misafara ya maqureish. Yalitokea mapigano na kuuwawa Amri bin Hadhram. Tukio hili walilitumia maqureish kueneza  propaganda chafu dhidi ya Uislam. Lakini Allah Taala akavunja uvumi wao. Tukio hili ni miongoni mwa sababu za kutokea vita vya Badr (Mwaka wa 2AH)

5.Kikosi cha Wadil-Quraa

Zaid bin Harithah aliongoza kikosi cha watu 12 kwenda Wadil-Quraa kukusanya taarifa za kijasusi dhidi ya makafiri. Kikosi hicho kikavamiwa na wakaazi wa mji huo, wakauwawa Waislamu 9 na kusalimika  3 akiwemo Zaid mwenyewe. (Mwaka wa 6AH.)

  1. Kutumwa kikosi cha Al-Khabt.

Mtume SAAW alituma kikosi cha watu 300 chini ya Abuu Ubeida Al-Jarrah ili kuwadhoofisha maqureish kiuchumi.(Mwaka wa 8 AH.)

7.Ghazwatu-Tabuuk.

Mtume SAAW alitoka na jeshi la watu 3000 kwenda Tabuuk kupambana na Warumi na vibaraka wao baada ya vita vya Mutah kutofanikiwa vizuri kulipiza kisasi cha balozi wake Al-Harith binUmair Al-Azd aliyeuliwa na Shurhabil Al-Ghassan. Khofu na hali ya hewa iliwatisha makafiri na kukimbia. Uongozi wa dola ulikabidhiwa kwa muda kwa Muhammad bin Maslamah Al-Answari au Sibai bin Arfata Al-Ghifariy (kwa masimulizi mengine) (Mwaka wa 9 AH.)

8.Vita vya Yarmouk.

Vita hivi vilitokea katika zama za Khilafah ya Umar bin Khattwab.

9.Ukombozi wa Al-Quds na Sallahudin Ayoub.

Baada ya Msikiti mtukufu wa Baiutil Muqadas kuwa chini ya Makruseda kwa miaka mingi Waislamu waliweza kuukomboa  na kuurejesha tena katika mamlaka yao  chini ya kamanda Sallahudin Ayoub (Allah Amrehemu) katika Tarehe 27 Rajab.

10.Kuangushwa kwa Khilafah ya mwisho (Khilafah Uthmania)

Serikali ya mwisho ya Kiislamu ya Khilafah Uthmania iliangushwa na makafiri kwa msaada wa vibaraka wa kituruki na kiarabu. Khalifah wa mwisho wa 101 Abdul Majid II alifungiwa virago vyake pamoja na familia yake na kufukuzwa katika makao makuu Istanbul, Uturuki. Na huu ndio ukwa mwisho wa Khilafah  (Tarehe 28 Rajab 1342 AH / Tarehe 3 March 1924 AD)

 

Read 447 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…