Tuesday, 11 April 2017 00:00

Ukafiri wa Pasaka

HAWAKUMUUWA WALA HAWAKUMSULUBU 

وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَكِنْ شُبِّهَ لَهُمْ

“Na kauli yao ya kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi  Issa , mwana wa Maryam, Mtume wa Mungu” hawakumuuwa wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa mtu mwengine….”

(TMQ 4: 157)

Suala la kuanguka kifikra, kuchanganyikiwa na kutekwa na fikra za kikafiri miongoni mwa Waislamu limepelekea baadhi ya Waislamu kushindwa kutofautisha baina ya fikra ya ‘Madania na Hadhara’ ambayo hufafanua wazi ni mambo gani Waislamu huruhusiwa kuchukuwa kutoka kwa makafiri na mambo gani haturuhusiwi kuchukuwa. (Rejea makala yetu ya hadhara-na-madaniya )

Hali hiyo imewafanya baadhi  ya Waislamu kujitumbukiza katika maadhimisho ya siku kuu za kinaswara na nyenginezo kama hii inayotukabili ya Pasaka. Kwa mfano, Tanzania Bara na Visiwani kwa miaka mingi kumekuwa na ziara za kimichezo kwa munasaba wa Pasaka. Ziara  ambazo kihukmu kwa Muislamu ni haramu kushiriki au kuchangia. Kwa kuwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kinaswara inayonasibishwa na kusulubiwa kwa Issa As. kufa  na kufufuka.

Ajabu inayodhihirika hapa ni badala ya Waislamu kuitumia fursa ya Pasaka kufedhehi waziwazi  na kuugonga udhaifu wa dini ya kikiristo katika misingi yake na kuwalingania wakiristo kuja ndani ya Uislamu kwa hoja za quran na dalili za kiakili, baadhi ya Waislamu kimakosa au makusudi  hujumuika na manasara katika maadhimisho hayo haramu.

Uislamu kwa kuwa ni dini ya haki mapema sana ilianzisha mapambano makali ya kifikra baina ya haki na batil. Na kwa upande wa dhidi ya unaswara unagonga kwa nguvu na makemeo makali misingi yote inayosimamia dini hiyo. Kwa kuonesha waziwazi kwamba ni misingi dhaifu, uwongo na batil. Kamwe Uislamu haukupaka mafuta  katika suala hilo, ili manasara wauone waziwazi udhaifu huo waache dini hiyo batil  na waingie katika dini ya haki ya Kiislamu. Wajibu huu wa kuigonga haki juu ya batil ndio msimamo ambao  Waislamu  daima tuna wajibu kushikamana nao. Amma ikiwa dhidi ya vidini vya kiroho kama ukiristo, uyahudi, uhindu ubudha nk. Au dhidi ya mifumo batil isiyo na haja ya dini kama ukomunisti ulioanguka kimataifa au udemokrasia/ubepari unaoendelea kumtia mashaka mwanaadamu kila uchao.

Quran inatamka wazi kwa kinywa kipana na bila ya lugha ya mzunguuko wala kupaka mafuta juu ya uwongo na upotofu wa fikra zote msingi zilizojengewa dini ya kikiristo. Kuanzia fikra tata  ya utatu, uwongo wao kuhusu uzawa wa Issa As, fikra zao potofu juu  ya  mwanamke mwema bi Maryam As. pia ikagonga kwa ukali upotofu wa madai yao ya kusulubiwa kwa Issa As. ati  kasulubiwa kufidia dhambi zao. Aidha, Quran ikatangaza bayana kwamba  msimamo wao huo wa kusulubiwa Issa As.ni uwongo shahir dhahir.

Uislamu unayafanya mapambano yote haya ya kifikra kwa kujitosheleza kwa hoja waziwazi na kunadi hadharani kwamba  manasara wamekwenda kombo na dini yao ni ukafiri usio na shaka.

Kwa hivyo, ikiwa misingi ya dini na imani ya kikiristo yote imejengwa juu ya msingi mbovu wa  uwongo na batil ina maana pia kwamba  vyanzo inavyovitegemea dini hiyo kuvua na kupata mafunzo yake pia ni batil na si vya kutegemea. Katika hali kama hiyo wakiristo watakuwa na chaguo moja katika mawili. Amma waache dini hiyo mara moja waingie dini nyengine ya haki. Au watafute vyanzo vya kuaminika kuhusiana na imani waliyonayo. Lolote watakaloshika katika mawili hayo watalazimika waingie katika Uislamu.

Tunapoangalia tareekh ya Kiislamu kwa makini  tutaona ndani mwaka wa nne wa Utume  viongozi wa kiutawala na wakinaswara ndani ya Ethiopia/Uhabeshi walikinai kwamba Quran ni chanzo cha kutegemea, wakati  iliposomwa mbele yao na sahaba Jaafar bin Abu Talib Ra. Ndani ya kasri yao kufafanua baadhi ya fikra ambazo manaswara wamezipotosha. Watawala hao na viongozi wa kinaswara walifanya unyenyekevu mkubwa kiasi cha kutiririkwa na machozi na baadhi yao kusilimu. Pia msafara wa wakiristo wa Najran uliokuja kwa Mtume SAAW ndani ya mwaka wa tisa ulikataa kusimama kufanya kiapo cha laana na maapizano (mubahala) baina yao  na Mtume SAAW. Hizi zote ni dalili za manaswara kukinai vyanzo vya kweli vya Uislamu.

Changamoto ya Waislamu leo hususan kwa minasaba ya siku kama hizi za maadhimisho ya kinaswara ni kuwakabili wakiristo hususan ‘wakiristo makini’ kuwaonesha udhaifu katika misingi ya imani yao na udhaifu wa vyanzo vya mafunzo ya imani hiyo ambavyo kamwe haviwezi  kuinusuru imani hiyo. Kwa kuwa kitabu chao hakitokani na Muumba. Na ukweli kuwa kitabu chao si cha Mungu hata wao wanaukiri. Kwa kuwa kitabu cha mungu, lazima kibakie katika lugha yake ya asili kilivyoteremshwa, kisiwe na mabadiliko kwa kuingizwa mikono ya binaadamu na asiweze mwanaadamu kutoa mithili yake kwa lugha na maudhui. Sifa hizo kamwe haziwezi kupatikana katika kitabu chochote duniani isipokuwa Quran. Katika hali hiyo wakiristo wangepaswa kutegemea kupata taarifa sahihi za kidini na mengineyo kwa ukweli, uaminifu na  ukamilifu kutoka ndani ya Quran. Wakiristo wakilikubali hilo ambalo hana budi kila mkiristo makini kulikubali, maana yake pia hawatokuwa na sababu ya kukikataaa kila kilichomo ndani ya kitabu hicho. Kwa kuwa wameshakinai kwamba ni kitabu cha haki. Basi wakati huo hawatokuwa wakiristo tena, bali watakuwa Waislamu. Kwa kuwa wamekinai  ukweli wa kitabu cha Quran.

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلاَّ نَعْبُدَ إِلاَّ اللَّهَ وَلاَ نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلاَ يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ (آل عمران: 64).

“Sema: Enyi watu mliopewa  kitabu (mayahudi na maswara)! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu: ya kwamba tusimwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu. Wakikengeuka , semeni shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu”

(TMQ 3:64)

 

Read 466 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…