Tuesday, 11 April 2017 00:00

Uharamu wa Kusheherekea 'PASAKA'

Baadhi ya aya za kutumia 4:156-158   4: 171-172   na aya nyengine zozote utakazoona zinafaa kwa munasaba wa qadhia hii.

Nini Ijumaa Kuu,

Siku hii pia huitwa Ijumaa takatifu ni siku ambayo wakristo wanaitakidi kwamba ndio siku aliyosulubiwa Isa As, baadae akazikwa, na siku ya Jumapili akafufuliwa (Jumapili hiyo ndio huitwa Jumapili ya Pasaka) (Weka neno ‘Good Friday’ katika Goggle utapata ufafanuzi zaidi kuhusu hili)

Matukio haya ya Easter japo kwamba  ni yenye kukubalika katika dini ya kikiristo, katika Uislamu hatuyakubali kwa sababu:

1.Ukiristo si dini ya haki

2.Mtukio haya  yamekanushwa na Quran.

Nini hukmu ya kisheria juu ya kusherehekea, kuadhimisha au kuhuzunika na tukio hili ?

Ni Haramu, kwa sababu:

      1.Aqeeda ya Kiislamu imeweka  wazi zipi sherehe zetu. (Rejea hadithi  juu ya sikukuu zetu)

      2.Kama matukio haya yangetokea tungeelezwa, kwa kuwa tumeambiwa tufunge siku ya Muharram kwa munasaba wa kuangamizwa Firaun na kuokolewa          Mussa As.

Jee inajuzu kujumuika katika sherehe za michezo mbalimbali katika mchakato wa sherehe hii ya Pasaka hata kama huitakidi chochote katika dini ya Ukiristo?

Jambo hili pia ni Haramu. Pamoja na kwamba michezo kwa asili yake ni  ‘mubaha’ lakini kwa vile  hapa linaingiliana na hadhara ya kikiristo, kama vile ilivyo tiba ya Babu wa Loliondo ilivyonasibishwa na hadhara ya kikiristo. Kwa hivyo, ni Haramu isiyo na shaka. (Rejea mada ya Madania na hadhara katika kitabu chetu cha Nidhamu-ul-Islam)

Nini hatari ya Waislamu kujumuika katika wimbi la kusherehekea Pasaka au sherehe nyengine zote za kikafiri kama X-mass na nyenginezo?

1.Kunaimarisha fikra hatari ya dini mseto (Rejea kitabu chetu cha ‘Fikra hatari za kushambulia Uislamu’)

2.Kuwazoesha (normalize) Waislamu na thaqafa ya kikafiri.

3.Kuondosha msukumo wa Waislamu kuwaona makafiri maadu

4.Kupelekea kuzorota au kuacha kabisa jukumu la kuwalingania makafiri. Kwa kuwa watawachukulia kama wenzao wasio na tishio lolote.

Katika hali kama hii nini wajibu wa Umma wa Kiislamu?

  1. Kuweka wazi na kufedhehi uwongo huu. Kwa kuwa Allah Ta’ala katuonesha mfano wa jambo hilo, na kuigonga itikadi ya kikiristo juu ya uovu wao.
  2. Kuwalingania Wakiristo waje katika haki. Lazima tufanye mgongano wa hadhara baina ya Uislamu wetu na kila aina ya ukafiri.  Kwa kuigonga kila dini batil kama hii ya Ukiristo na fikra zake kama hii ya Easter na nyenginezo. Pia kuugonga mfumo wowote na  fikra zozote batil.  Kama ubatil wa  wa mfumo wa Ubepari fikra zake za  uhuru, haki za binaadamu, usawa wa kijinsia nk (Rejea kitabu chetu ‘Kutokuepukika migongano baina ya hadhara’)
  1. Aidha, kufedhehi fikra ya dini mseto na wale wanaoipigia debe ambao hudai  kwamba dini hizi zinatokana na chimbuko moja na msingi mmoja. Katika hilo  lazima tuoneshe  wazi wazi uovu wa fikra hiyo. Pia  tuwakumbushe Waislamu wanaohubiri dini mseto na ukuruba baina ya dini kwa mfano hai wa hali tuliyonayo  namna  wakiristo walivyokuwa hawajali wala hawatambui  fikra hiyo. Hilo linadhihirika wazi wazi katika msimamo wao wa kupinga na kuzuwa uongo mkubwa juu  ya  suala la mahkama ya qadhi. Licha ya kutambua viongozi hao wa makanisa kwamba mahkama hiyo haina athari ya udhati. Lakini kutokana na uadui wao wanaipinga na kueneza propaganda chafu makanisani. Ni kutokana na hilo ndio pia Makanisa  yametoa waraka maalumu kupinga  bila ya kujali  kile kinachoitwa umoja na ukuruba baina ya dini hizi. Kama wanavyolipigia kifua suala hili baadhi ya masheikh maslahi.
  2. Pia lazima tuoneshe namna makanisa yanavyokuwa mstari wa mbele kutetea nidhamu ya  kidemokrasia na katiba zake. Kwa kuwa mambo hayo  yanatokana na ukafiri kama wao. Na kwa kuwa ukafiri ni mila moja.  Wakiristo wanashika misimamo hiyo na kuipigia debe  ilhali wakijuwa wazi kwamba siasa za kidemokrasia, chaguzi zake  na katiba zake  zipo kinyume na Uislamu. Lakini katika hilo kamwe Wakiristo  hawaungani na mtazamo wa Uislamu. Bali kinachotokezea ni  baadhi ya Waislamu  amma kwa  kuanguka kwao kifikra au kwa maslahi ndio huungana na Wakiristo katika kuunga mkono vyama vya kidemokrasia, siasa  zake na katiba zake. Na kamwe wakiristo hawafuati msimamo wa Uislamu ambao ni kupinga  mambo hayo.
  1. Pia tuwakumbushe Waislamu kuwa hata kama baadhi ya Viongozi wa makanisa wakionekana kutofautiana katika  suala la katiba pendekezwa kama inavyoonekana sasa  mvutano uliopo  baina ya Askofu Pengo na  Mchungaji Gwajima. Kimsingi kinachodhihirika hapa ni uadui wa kimaslahi tu baina yao.  Lakini  kimsingi hawapingi katiba kwa udhati wake.  Bali wanachotofautiana ni  mbinu bora zaidi na  uboreshwaji katika  mchakato wa upatikanaji wa katiba hiyo. Kwa hivyo kimsingi viongozi wa makanisa  kamwe huwa hawapingi nidhamu ya kidemokrasia katika msingi wake. Bali daima husimama nayo bega kwa bega. Kwa kuwa ni ukafiri kama wa dini yao, na ambao uko kinyume na Uislamu.

Katika muongozo huu ni muhimu kwa mzungumzaji kuongeza katika ufafanuzi wa aya zaidi, hadithi zaidi za Mtume saaw, matukio katika sira na  mifano hai ya waqia ili kuifanya mada kuwa na mvuto zaidi. Pia mada zifuatazo zitasaidia zaidi:

Read 650 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…