Friday, 14 April 2017 00:00

Bila ya Khilafah ni Utumwa na Dhulma-3

Khutba ya Ijumaa 17 Rajab 1438 Hijri / 14 Machi 2017 Miladi

Wakati tukiendelea kuikumbuka dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyoangushwa ndani ya mwezi huu wa Rajab, lazima tukiri kuwa kuangushwa kwake kumesababisha kukosekana amani, usalama na utulivu kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii na wanadamu kwa jumla.  Wawe watu wa dini nyengine, wanawake, wafungwa, wakimbizi nk. Khilafah ilisimamia haki za makundi yote kwa uadilifu, insafu na kwa mafanikio ya hali ya juu.

Leo tunashuhudia Waislamu kuteswa na kuuliwa kwa ukatili usioelezeka ndani ya Afrika ya Kati, Burma, India nk. Pia tunaona namna dola ya Misri inavyoshindwa kusimamia usalama wa wakiristo wa madhehebu ya kibti (coptic) kiasi cha karibuni kuripuliwa kwa mabomu na kuuliwa wafuasi wa kanisa hilo karibu 50. Wakati hayo yakijiri ilikuwa ndani ya Rajab (28 Hijria/ 638 miladi) baada ya dola ya Khilafah kuukomboa mji wa Aelia na wakaazi wake kwa ridhaa ya nafsi zao chini ya Askofu wao Mkuu Bwana Sophronius  kuridhia bila ya mapigano, Khalifa Umar ra. binafsi alifunga safari ndefu kuja kushuhudia qadhia ya watu hao, na akaandika waraka mtukufu wa kihistoria unaosomeka:“Kwa jina la Allah, Arrahman, Arrahiym : Huu ni waraka wa mkataba kutoka kwa Umar, mtumwa wa Allah, kiongozi wa Waislamu, kwa watu wa Aelia. Anadhamini usalama wa maisha yao, mali zao, makanisa yao na misalaba yao…Makanisa yao yasivunjwe wala yasiondoshwe, na kisiondoshwe chochote katika vitu vyao. Wasilazimishwe katika mambo ya dini, na asidhuriwe yoyote……”

Pia itakumbukwa katika zama za Khalifa Mu’utasimu bil-llah (750-754 miladia) askari wa kiroma alipomdhalilisha mwanamke wa Kiislamu kwa kumvua hifadhi yake(hijabu), na mama huyu kupiga mayowe kwa kunadi  yaa Mu’utasimu (ewe Mu’utasimu) upo wapi mimi nadhalilishwa ! Kwa haraka Khalifa bila ya ajizi akaandaa jeshi la Waislamu kuwatia adabu waroma na kumkomboa mwanamke huyo.  Khalifah huyu alifariki akiwa mdogo wa umri wa miaka 45 tu, bali tukio hili limekuwa ni kito cha thamani katika tareekh.

Wakati leo wakimbizi wa Kiislamu na wasiokuwa Waislamu wakipewa daraja ya kuliko wanyama katika nchi mbalimbali duniani, ilikuwa ndani ya mwezi Julai 1492, wakati Waislamu na mayahudi walipokuwa wakifukuzwa kwa agizo maalumu la serikali ya Spain (Spanish Inquisition) Khalifah Bayezid II alituma manuari maalumu chini ya Kamanda Kemal Reis kuwaokoa Waislamu na mayahudi, na akawapa hifadhi ya ukimbizi mayahudi zaidi ya 150,000    http://ilmfeed.com/when-the-islamic-state-saved-150000-jews/

Enyi Waislamu na Wanadamu kwa jumla : Sote ni mashahidi kwa matukio ya uovu wa magereza ya kimataifa kama Guntanamo, Abu Ghuraib, Bagram nk. namna wanavyodhalilishwa Waislamu kwa kufanyiwa vitendo viovu visivyoelezeka. Na kwa upande wa kitaifa hali ni hiyo hiyo. Ni Waislamu wangapi hapa Tanzania wamenyakuliwa na hakuna taarifa zao. Kiasi cha hata maiti zilizokutwa zikielea mto Ruvu pia ni za Waislamu. Hali hiyo imekithiri kiasi cha pia kuwahusisha hata wasiokuwa Waislamu akina Ben Sanane na wenzake, hadi uovu wa utekaji kuibuliwa kuwa ni ajenda ndani ya Bunge! Hali ambayo kwa muda mrefu imekuwa ni ya kawaida kwa Waislamu. Ni wangapi wanaouchukuliwa hadharani au kwa kificho, kuteswa, kudhulumiwa, kunyanyaswa bila ya maelezo wala sababu, huku wengine hawarudi tena, na wanaorudi wakiwa hawajiwezi kwa mateso na dhulma

Enyi Waislamu na wanadamu kwa jumla:

Chini ya mfumo batil wa kidemokrasia hakuna atakaesalimika awe Muislamu au mwengineo kwa kuwa ni mfumo uliojengwa juu ya kipimo cha maslahi, kupupia madaraka na kushikilia fikra za Machievelli za “fanya lolote kufikia lengo lako”. Basi ni wajibu kwa Waislamu kushiriki katika mchakato wa kuirejesha Khilafah itakayoanzia katika nchi kubwa ya Waislamu ili kuwakomboa Waislamu na wanadamu kwa jumla. Na kwa wasiokuwa Waislamu waanze kutafiti mfumo mbadala kando na demokrasia.

Tunamalizia kwa kusema ‘Bila ya Khilafah wanadamu watazongwa na Utumwa na Dhulma zisizokwisha.

http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Read 321 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…