Thursday, 25 May 2017 00:00

Donald Trump awa nuru ilochomoza Saudia - mpaka lini waislam watavumilia?

Donald Trump awa nuru ilochomoza Saudi -mpaka lini waislam watavumilia?

Viongozi wa Ufalme wa Saudia, tarehe 21,May 2017 wampokea Raisi wa Marekani Donald Trump kama mtu mtukufu wa aina yake mwenye baraka tele na haiba ya kuwakomboa waislamu wapate kazi na kukuza iktisadi zao kupitia miradi iliyosainiwa baina ya nchi mbili hizo. Katika ziara hiyo Marekani na Saudia  zimefanya biashara kubwa mno kuuza na kununua silaha za mabilioni ya Dola kwa kutengenezwa mazingira ya kitisho cha vita/proxy war kutoka Iran kwa vijidola vya Mashariki ya kati ikiwemo Saudia. Viongozi kadhaa wa Mashariki ya kati na Asia Mashariki vibaraka kwa Marekani walihudhuria mapokezi hayo. https://www.washingtonpost.com/politics/trump-gets-elaborate-welcome-in-saudi-arabia-embarking-on-first.

Msimamo wa Donald Trump dhidi ya uislamu na waislamu uko wazi tokea wakati wa  kampeni yake ya uraisi, na katika ziara hii kawaamrisha waziwazi vibaraka wake wa Mashariki ya kati kuwafurusha ndugu zao waislam ambao anawaita magaidi katika ardhi takatifu” barbaric criminals”. Trump alishajuwa kuwa Saudia ni mshirika wao mkubwa katika kuangamiza waislamu kwa kile kinachoitwa ugaidi na uislamu wa siasa kali .Ufalme wa Saudi ulitoa mchango wake mwezi August 2014 kwa UN kitita cha US $ 100 milioni  kwa ajili ya kupambana na ugaidi na uislamu wa siasa kali.

Hakika ziara hiyo ni kulinda maslahi ya Marekani na kuna mambo matano (5) yamejitokeza ambayo ndiyo kiini cha kuhifadhi maslahi hayo:-

Lakwanza ni kuithibitisha Saudia kama ni wakala yenye hadhi ya kwanza  baada ya Israel katika Mashariki ya kati na kuithibitishia kuwa mkataba wa ushirikiano na ulinzi  uliofungwa baina ya nchi mbili hizo na viongozi wa wakati ule Raisi wa Marekani Roosevelt na Mfalme Feisal mwaka 1931 ni wa kupigiwa mfano.

Lapili ni kuthibitisha kuwa viongozi wa Saudia wamekuwa watiifu kwa kila hali inayotaka Marekani  ifanyike Mashariki ya kati, kuanzia kuwaondoa viongozi vibaraka wasiotekeleza yote walio amrishwa na bwana wao Marekani mfano Saddam Hussein ,Gaddafi na wengineo ambao walisababisha kung’olewa madarakani kwa nguvu likitumika jukwaa la UN kiwazi na kwa mlango wa nyuma kuhalalisha vita vilivyoibomoa miji ya Iraq na Libya na kumwaga damu nyingi za waislam kama mito.Itakuwaje UN ikatae kupigwa Iraq lakini baada ya kuvurugwa ihalalishe ujenzi wa miundombinu ya Iraq?  Miji mengine iliyopata athari kama hiyo ni Afghanistan na sasa wanaimaliza miji ya Syria kwa kuunda makundi manyenyekevu kwa Marekani kama ISIS huku wakisaidiwa na Urusi, Iran na Uturuki.

Nchi za Urusi, Iran na Uturuki zimepewa angalizo na Marekani, zizidishe utiifu ili na wao wapate nafasi kama ya Saudia.

Utii wa Saudia kwa Marekani ukaongezeka kwa kuivamia Yemen kijeshi na kuiangamiza miji ya nchi hiyo pamoja na kumwaga damu za waislamu zaidi ya 10,000 na kuwaacha zaidi ya raia milioni 2.5 wakitanga tanga kwa dhiki kubwa ya maisha  baada ya kubomolewa makazi yao. http://foreignpolicy.com/2016/03/25/civilian-casualties-war-crimes-saudi-arabia-yemen-war/

Latatu ni kuipa jukumu Saudia kuwa kinara miongoni mwa nchi za kiislamu katika kutekeleza sera ya nje ya Marekani ya kupambana na “ugaidi na waislamu wenye siasa kali”

Lanne ni kuifyonza Saudia kwa kiwango  kikubwa kwa kiuzia silaha za  Bil $ 110 na katika kipindi cha miaka 10 ijayo mauzo hayo kuongezeka zaidi ya Bil $ 200. Silaha hizo ni dhahiri zitatumika kuipiga nchi yo yote jirani yake kwa maelekezo ya Marekani, kama inavyofanya Israel. Marekani sasa inazidi kurahisishiwa  ukoloni wake wa Mashariki ya kati kupitia Israel na Saudia. Kwa hivyo nchi na makundi yote yaliyokuwa yakisaidiwa silaha na fedha na Saudia kijanja janja kupigana na kutoitambua Israel. Sasa lazima yaache sera hizo kwani mfadhili wao Saudia ameonyesha ile sura yake halisi juu ya Marekani na  Israel.

Latano ni Saudia kumpongeza Trump kukaza kamba katika kutekeleza sera  ya Marekani ya kupambana na ugaidi na waislamu. Kitisho cha Trump kwa uislam na waislam ni faraja kwa viongozi wa Saudia hadi kumtukuza kwa kumvisha mkufu wa dhahabu na qaswida  ya (Twala’a lbadru). Ilhali wanatambua kuwa “Twala’a lbadru” alipokewa Mtume SAW kwa watu kukinai kuwa kuja kwake SAW ameleta taratibu mpya na ustaarabu wa dunia. Sasa fedheha kwa Saudi inampokea Trump kumpongeza kwa kuwachinja waislam?.

Enyi watukufu waislamu, sasa wale walokuwa viongozi wa Saudia ambao wanatulaghai kwa kudhamini/scholarship nyingi za masomo, kuleta misahafu ya bure na kujenga misikiti ya kifakhari pamoja na kujinadi ni wasimamizi wa misikiti mitukufu ya Makka na Madina kumbe sura zao halisi ni kutekeleza sera za Makafiri ya kuangamiza uislamu na waislamu.

Enyi watukufu waislamu, Allah SWT amejaalia ardhi yake itawaliwe na waja wake wema na wala hakuna kisichowezekana mbele Yake  kama anavyosema;

وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِنْ بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ.

إِنَّ فِي هَذَا لَبَلاَغًا لِقَوْمٍ عَابِدِينَ

Na hakika tuliandika katika Zaburi baada ya ufunuo(Allauhilmahfudh)kwamba ardhi hii watairithi waja wangu wema.

Hakika katika haya pana mawaidha kwa watu wafanyao ibada.(21:105-106)

 

Basi enyi Waislamu Viongozi wa Saudia na vibaraka wengine wote wanaonyenyekea Marekani na makafiri wengine hawana haki kamwe kutuongoza sisi wala wasiwe tena mfano kwetu. Tufanyeni daawah tutekeleze yetu na Allah atutekelezee ya kwake kwetu apendavyo tuwaondoe wote hawa viongozi sura mbili. Tuweke viongozi wachamungu, waadilifu na wanyenyekevu kwa Allah SW ili wawasimamie Waislamu chini ya Serikali ya Kiislam/Khilafah.

Na Suleiman Mbarouk-Ticha Sule

Read 1078 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…