Siasa

Siasa (26)

Habari:

Kwa mara nyingine tena vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti taarifa za kuendelea kuteswa kwa vijana wa Kiislamu wanaotuhumiwa na ugaidi. Mbunge wa upinzani jimbo la Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema ambaye naye alikuwa akishikiliwa katika mahabusu ya Kisongo amefichua kwamba vijana 65 wa Kiislamu wa jiji la Arusha watuhumiwa wa ugaidi wanaendelea kushikiliwa katika mahabusu hiyo kwa muda wa miaka minne bila ya kufikishwa mahakamani. Aidha, Mbunge Lema aliweka wazi hadharani kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakitesha kiasi cha mmoja wao kuvunjwa mguu.

Maoni:

Taarifa hizi sio ngeni kwa kuwa ni jambo linalojuulikana na kila mtu kuwa kufanyiwa vitendo vya mateso au hata kuuwawa watuhumiwa wa ugaidi ni suala la muda mrefu hapa Tanzania na kwingineko duniani kote. Mbali na kauli ya mbunge Lema,  watu wengine maarufu wasio Waislamu kama Dr. Slaa, Askofu Gwajima na Tundu Lissu (MP) wamewahi kulisemea hilo hilo.

 Aina mbali mbali za ukatili wa kinyama, udhalilishaji na adhabu ni mwenendo wa kawaida katika sera za kidhalimu za mfumo batili wa kibepari hususan kwa wapinzani au wale waliobeba mfumo mbadala na pinzani na ubepari ambao kwa muktadha huu Waislamu ndio pekee walengwa wakubwa na wanaochukuliwa kuwa ni wahalifu nambari moja.

Mara nyingi vyombo vya dola katika nchi zinazoendelea hutenda matendo ya kikatili kwa Waislamu kwa maagizo kutoka nchi za magharibi. Mathalani, sheria ya Marekani ya kupambana na ugaidi (US Patriot Act) inaviruhusu vyombo vya dola kuzipora mali za watuhumiwa wa ugaidi, kuwatesa au hata kuwaua.

Pamoja na hilo ni ukweli usiopingika kwamba uwepo wa chuki binafsi na uadui mkubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu kutoka kwa maofisa wa polisi wa nchi zinazoendelea si jambo la kupuuzwa hususan nchi kama Tanzania ambapo ubaguzi dhidi ya Waislamu na Uislamu ni suala la kihistoria na lililokita kwa muda mrefu.

Mateso ni suala linalodhihirisha na kufedhehi wazi wazi uwongo wa kile kinachoitwa haki za binadamu, dhana ya uwongo na uchafu unaostahili kutupiliwa mbali jalalani kwa kukosa kabisa uhalisia katika maisha ya kawaida !

Kitu muhimu kwa watawala madhalimu wa kibepari ni kulinda mfumo wao na maslahi yao binafsi.  Kwa hiyo, kwao sheria huwa zina maana pale tu ambapo maslahi yao yatahakikishwa. Suala la uvunjaji wa sheria za kitaifa au kimataifa au vinavyoitwa vipimo vya haki za binadamu kwao halina uzito wowote hususan wanapoamiliana na Waislamu na Uislamu.

Ama kuhusu watuhumiwa wa ugaidi kutopelekwa mahakamani kwa muda wa miaka mine, hii ni dalili ya wazi kwamba hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani kwa tuhuma zinazowakabili. Wanashikiliwa kutokana na uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu. Mara nyingi watuhumiwa wa kinachoitwa mapambano dhidi ya ugaidi (Uislamu) baada ya kuteswa kishenzi huachwa huru kwa kukosekana ushahidi. Makosa yao si mengine bali ni kuulingania Uislamu kama mfumo mbadala dhidi ya ubepari, ubepari ambao ni mfumo batili uliowafikishia wanaadamu maangamizi mabaya katika nyanja zote.

Kama zilivyo nchi nyingine zinazoendelea Tanzania nayo imeburuzwa na Marekani katika vita dhidi ya Uislamu kwa kutaraji thamani duni bila ya kuzingatia mtikisiko wa mshikamano tete wa  jamii yake, hali inayoweza kupelekea mazingira ya mustakbali wa hatari.

Uislamu mfumo wa haki na uadilifu umejengwa juu ya hoja za kukinaisha akili, kamwe hautashindwa kwa mateso wala vurugu la kiwoga la ubepari unaotokana na usekula, kwa udhati mfumo huo (ubepari) unatapatapa katika kujihami kwa mabavu, kwa kuwa umekosa msingi wa kukinaisha na hoja thabiti

 

Imeandikwa na  Ramadhan Said Njera

Mjumbe wa Afisi ya  Habari, Hizb ut-Tahrir Tanzania

Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir

 

 

 

Friday, 03 March 2017 00:00

Majanga Baada ya Kuangushwa Khilafah

Written by

Hatimae mwishoni mwa mwezi kama huu wa Rajab Mwaka 1342 Hijri (Machi 1924 miladi) Serikali ya Khilafah ya mwisho iliyotawala kwa karne 14 mfululizo iliangushwa (Khilafah Uthmania). Hili lilifanikiwa baada ya mapambano makali ya muda mrefu kutoka kwa maadui wa Uislamu kwa msaada wa vibaraka wao wa kiarabu na kituruki.

Friday, 03 March 2017 00:00

Mikataba iliyoinyonga Khilafah ya Mwisho

Written by

Madola ya Magharibi chini ya Uingereza hayakutosheka kugawana ngawira baada ya Vita vya Kwanza vya dunia. Bali waliendelea na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanaivunjavunja kabisa athari ndogo iliyobakia ya dola ya Khilafah Uthmania.

Katika tarehe 3 Machi 1924 Miladi sawa na mwezi wa  Rajab mnamo mwaka 1342 Hijri/  , dola ya mwisho ya Kiislamu ya Khilafah Uthmania iliyodumu kwa makarne, iliyoziunganisha nchi mbalimbali na iliyofikia kilele cha mafanikio kwa kutisha kila pembe ya ulimwengu iliangushwa na makafiri kwa msaada wa wasaliti wa kiarabu na kituruki.

Febuari 2, 2017 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alianza mfululizo wa kutaja majina ya watu wanaohisiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya “unga”.Tunaunga mkono juhudi za dhati za kupambana na janga hili japo katika demokrasia na ubepari huwa zimeambatana na sababu maalum au kuwalenga watu maalum kwa sababu ya maslahi ya watu maalum na hivyo kukosa tija kwa umma.

 Habari :

Vyombo vya habri vya Tanzania pamoja na vya kimataifa vimeripoti vita vinavyoendelea dhidi ya madawa ya kulevya,ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataja baadhi ya watu maarufu wakiwemo wafanyabiashara wakubwa, viongozi wa kanisa ,wasanii na maofisa wa polisi wakituhumiwa kujihusisha na qadhia ya madawa ya biashara hiyi haramu.Mkuu huyo wa mkoa akawataka watuhumiwa hao kuripoti kituo cha polisi kati kwa ajili ya mahojiano ili kuwabaini wasambazaji wakubwa.

Thursday, 23 February 2017 00:00

MWAKA MPYA WA KIISLAMU UTUKUMBUSHE TUKIO KUBWA LA HIJRA

Written by

‘Na sema Mola wangu niingize muingizo mwema na nitoe kutoka kwema na unipe madaraka kutoka kwako na ushindi’ (TMQ 17:80)

Thursday, 23 February 2017 00:00

Je Mbona Hali Ya Mazingira Mitaani Hairidhishi Jameni?

Written by

Mazingira ni kila kitu kinacho mzunguka mwanaadamu.Iwapo mwanaadamu atakuwa ni mwenye kupuuza kuhifadhi mazingira yake basi litakuwa ni jambo la kimaumbile kwa mwanaadamu kuwa ni mwenye kuathirika kwa kuwa mgonjwa na hata mwisho kuangamia.

بِِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Katika mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2010 miladiya, Tanzania itaingia tena kwa mara ya nne katika chaguzi za kidemokrasia za vyama vingi.Tayari vuguvugu la uchaguzi linafukuta na kuhisika kila mahali katika hatua ya maandalizi yake. Sambamba na hilo, na katika hali ya kusikitisha na kushangaza kuna wanaoendelea kuhamasisha Waislamu kushiriki kikamilifu katika chaguzi hizo za kidemokrasia kiasi cha kunadi kwamba kufanya hivyo sio tu ni muhimu, bali ni miongoni mwa matendo matakatifu ya kidini mbele ya Allah Ta’ala!

Umma wa kiislamu baada ya kusibiwa na uvivu wa kusoma vizuri dini yao na kuifahamu wamekuwa wazito kupambanua baina ya sheikh msomi wa uislamu na mbabaishaji anaye hadaa waislamu wakisikia tu ana soma aya kwa kiarabu bila kukumbuka hata ABUUJAHLI alikuwa na uwezo mzuri wa kusoma quran tena na kuifahamu lakini alikuwa ni pagani.

Tuliyoyashuhudia na tunayoendelea kuyashuhudia ya kutendewa dhulma kwa Sheikh Ponda tangu kuanzia kuekwa korokoroni, kuekewa mipaka katika  ulinganizi, kupigwa risasi na  kusombwa kwa idhilali hospitali ilhali bado akiwa na jeraha la maumivu,  hayo hayakulengwa kwa mtu binafsi tu.  Bali kwa  upana wake  yamelengwa kwa Uislamu wetu na Waislamu jumla.

Page 2 of 2
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…