Sunday, 14 May 2017 00:00

Tupatilize fursa ya sha'aban

 

Katika mwezi  kama huu wa Shaaban Mtume SAAW alikuwa akikithirisha sana ibada. Alipoulizwa na Swahaba wake Usama bin Zaid (ra) juu ya sababu ya kufunga sana katika mwezi huu alijibu:


 ((
ذاك شهر تغفل الناس فيه عنه، بين رجب ورمضان، وهو شهر ترفع فيه الأعمال إلى رب العالمين، وأحب أن يرفع عملي وأنا صائم))

“Shaaban ni mwezi ambao watu wameghafilika nao, upo kati ya Rajab na Ramadhan, nao ni mwezi ambao amali hupandishwa kwa Mola wa Ulimwengu na mimi napenda amali zangu zipandishwe na hali ya kuwa nimefunga.   (An-nasai)

Vile vile Mtume saw amesema: Ibada wakati wa matatizo (fitnah) ni kama Hijra.. . (Muslim)

Hadithi kama hizi zinatuonyesha umuhimu wa Waislamu kujifunga katika kutenda amali njema wakati wote bila ya kughafilika katika kipindi au muda fulani

Uislam ni mfumo kamili wa maisha ya mwanaadamu na kwa kipindi chote cha maisha yetu. Hivyo, tunatakiwa tuishi chini ya mfumo aliotuwekea Allah sw,  mfumo  uliokamilika na ulioenea katika maeneo/vipengele v yote vya maisha yetu

Kwa sababu mwanaadamu hutokea kukabiliana na  mazingira tafauti katika mzunguko wa maisha yake ambayo huweza kumpelekea kughafilika na baadhi ya mambo. Katika hali kama hiyo ndipo Mtume SAAW anatuzindua na kutuhimiza kutopunguza kasi ya kutenda matendo mema katika dhurufu/hali ngumu na ambazo aghlabu ya watu hufadhaika,  kuchanganyikiwa au kusahau yaliyo muhimu zaidi katika Uislamu wetu.

Read 296 times
More in this category: Karibu Ramadhani »
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…