Wednesday, 24 May 2017 00:00

Karibu Ramadhani

 

 

سْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Karibu Ramadhani

Kwa jina la Rahmani , Muumba anga na wanda

Na Salamu na Amani, zimfike mziwanda

Bwana wetu Adinani, alotumwa na ajenda

Ramadhani imefika, Shime sote tufungeni.

 

Nawaita Waumini, wa Mbagala na Kitunda

Wa Bara na Visiwani, hadi Kenya Miji Kenda

Hebu haraka n-njoni, kwenye mwezi wa kudanda

Ramadhani imefika,   shime sote tufungeni.

 

 

Umma sote tufungeni,   daraja tutaipanda

Kwenye Pepo ya Rayani,  na Mola Atatupenda

Tuipate burudani,   na shetani kumshinda

Ramadhani imefika,   shime sote tufungeni

 

Haya shime simameni,   tu-uwacheni ununda

Ajizi iwe pembeni, na mambo ya inda inda

Ibada tujipindeni, tuache kurandaranda

Ramadhani imefika, shime sote tufungeni

 

Kalamu nabwaga chini, naitoa kwenye chanda

Ujumbe wangu makini, kwenu nimeshautanda,

Uingizeni moyoni, na mtende ya kutenda

Ramadhani imefika, shime sote tufungeni

 

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut-Tahrir Tanzania

Read 299 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…