Thursday, 25 January 2018 00:00

Nabii Tito Na Mahubiri ya Toti

Qadhia ya anayejiita 'Nabii' Tito anayedai kuhubiri biblia kupitia kampeni ya zinaa na ulevi inadhihirisha mambo mawili makubwa ambayo Waislamu na wasiokuwa Waislamu hulazimu kuyazingatia kwa makini:

1. Mgongano wa wazi katika nidhamu ya kidemokrasia, upande mmoja inahubiri fikra za 'uhuru wa kuabudu' na 'uhuru wa maoni'. Fikra ambazo huzalisha utitiri wa dini, madhehebu na wabebaji wa fikra za kimaajabu zinazosheheni maovu na ufuska. Ajabu ! nidhamu hiyo hiyo iliyozalisha hayo hurudi kujidai kupiga marufuku matunda waliyozalisha.

2. Maumbile ya dini yenyewe ya kikiristo ina mgongano sugu na mkanganyiko mkubwa katika mafundisho yake, kiasi kwamba kila siku huleta migongano mipya ndani yake isiyokwisha.

Allah SW anasema:

وَمِنْ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَى أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمْ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمْ اللَّهُ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ (المائدة: 14).

"Na katika wale waliosema : Sisi ni Wakiristo, tulichukua ahadi kwao, lakini wakasahau (wakapuuza) sehemu ya waliyokumbushwa, kwa hivyo tukaweka kati yao uadui na chuki mpaka Siku ya Kiyama. Na hapo Mwenyezi Mungu atawajuza waliyokuwa wakiyatenda"

23/01/2018

Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Tanzani

Read 1099 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…