Thursday, 01 February 2018 00:00

Haiwezekani Kulinda Maadili Kwa Mfumo Usio Na Maadili

Mara kwa mara tumekuwa tukisikia kupazwa sauti juu ya suala la kuendelea kuporomoka kwa maadili kwa kiwango cha kutisha katika mujtamaa/jamii wa Tanzania na ulimwengu mzima. Hapa Tanzania tumesikia zaidi hususan wanasiasa wakilaumiana kwa kutochukuliwa hatua stahiki kwa wanaokiuka maadili yanayoitwa ya mtanzania.

 Kwa bahati mbaya mara nyingi maadili hutizamwa katika ufinyu, kama vile kwa wanaovaa nguo nusu uchi hususan wanamuziki na waigizaji nk. Amma kuhusu ulevi, makasino, uchafu katika fukwe za bahari au hata viguo vinavyovaliwa mitaani, haya yote hayaonekani kama ni ukosefu wa maadili. Bila ya kutaja vituo vya Luninga/Tv kuchezesha miziki yenye kuambatana na picha chafu, lakini huonekana kama kitu cha kawaida. Cha ajabu! hakuna kituo kilichowahi kuadhibiwa kwa maovu hayo, na badala yake huadhibiwa kwa kurusha maudhui yanayokinzana na uoni wa kisiasa. Pia katika kuwazuga raia kwamba maadili yanahifadhiwa  na kulindwa hufungiwa baadhi ya wasanii kujihusisha na sanaa kwa masiku yanayohesabika. Hatimae baadhi yao huomba radhi na kuachiwa kuendelea na shughuli zao!.

 Kwa udhati maadili hayawezi kulindwa na kuhifadhiwa chini ya nidhamu ya kidemokrasia. Kwa sababu jukumu msingi la nidhamu hiyo ni kulinda na kuhifadhi ‘uhuru’ wa raia unaodhaminiwa na sheria zake bila ya kuzingatia maadili, utu, haramu wala ustaarabu.

 Miongoni mwa ‘uhuru’ wa kidemokrasia unaotokamana na kinachoitwa haki za binadamu ni ‘uhuru wa kibinafsi’. Uhuru huu maana yake mtu yupo huru kula, kunywa, ama kuvaa chochote anachotaka kwa utashi wa nafsi yake.  Jukumu la serikali ni kuulinda uhuru huu  na kuhakikisha raia wake wanafaidika nao. Lau watu watamkamata mwizi kisha kumpeleka kituo cha polisi kesi huwa upande wake. Kinyume chake lau watu watamkamata mwenda nusu uchi na kumfikisha kituoni kesi huwa upande wao.!

 Mfumo wa kidemokrasia na miito yake ya ‘uhuru’ inagongana na maumbile ya binadamu (fitra) mathalan mwanadamu na hisia ya kuhifadhi maisha inayomsukuma kutaka heshima ikiwemo stara kwa utupu. Kwa ujanja watawala wa kidemokrasia nao hujinasibu kwamba hawapendi watu kutembea utupu ilhali kwa mlango wa nyuma wakilichochea kwa mbinu na njia mbalimbali.Ndiyo maana tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 maadili yameendelea na yataendelea kuporoka kadiri fikra za kidemokrasia zinapojikita kwa mtu binafsi na kwa jamii kwa jumla. Hali mbaya kwa nchi waasisi wa mfumo huu ndiyo itakavyokuwa kwa Tanzania kadiri demokrasia inavyomakinika.

 Tanzania na kwingineko haiwezekani kulinda maadili kikweli  chini ya mfumo wa kidemokrasia na hususan ukizingatia kuwa nchi changa hazina  hata uhuru wa kutunga sheria kwa matakwa yao. Bali kutunga sheria kwa kufuata maagizo ya mfumo na maazimio ya madola makubwa yanaoitwa a kimataifa.

Uislamu umeyafanya maadili yote mema ni sehemu ya ibada, hivyo, Muislamu binafsi ana msukumo wa ndani wa kulinda na kuhifadhi maadili mema. Na zaidi dola ya Kiislamu ya Khilafah itafanya kazi ya kulinda na kuhifadhi maadili kwa thaqafah na nidhamu ya kuadhibu,  na kamwe watu hawatokuwa huria kama wanyama kama walivyo leo chini ya nidhamu batil ya kidemokrasia.

إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَى وَيَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ (النحل: 90)

 “Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka”

 Afisi ya Habari -   Hizb ut- Tahrir Tanzania

 10 Jumada al-awwal 1439 Hijri   | 27/01/2018 Miladi

                           http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Read 620 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…