Tuesday, 27 February 2018 00:00

Mfumo Muovu wa Kidemokrasia Hauwezi Kutoa Haki.

Habari:

 

Vyombo vya habari vya Tanzania na vya kimataifa karibuni viliripoti maadhimisho ya Mahkama ya Tanzania kwa ‘wiki ya sheria’ yanayofanyika kila mwaka, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni matumizi thidi ya teknolojia ya habari kusukuma zaidi ufanisi,  kuharakisha mchakato wa uendeshaji kesi ili kuondoa mrundikano mkubwa wa kesi mahkamani na maboresho mengine kwa ujumla.

 

Maoni:

Kimaumbile demokrasia kamwe haipo kutoa haki na uadilifu kwa Umma, badala yake ipo kwa lengo la kuwapa nguvu na "haki" wenye nguvu wachache (mabwanyenye) ili wawadhulumu walio wengi na ukandamizaji wa raia jumla hususan Waislamu.

 Sera kandamizi kwa kisingizio cha kusimamia ‘haki’, sheria na taratibu kwa kiasi kikubwa huelekezwa kwa tabaka la wanyonge, wapinzani machoni mwa watawala na wale waliobeba mfumo mbadala tofauti na ubepari, kwa muktadha huu bila ya shaka ni Waislamu pekee,  ambao ndio walengwa wakubwa na huchukuliwa kuwa ndio wahalifu nambari moja.

 Watu wengi hususan Waislamu wamewekwa korokoroni na kufungwa jela kwa dhulma huku wengine wakikaa mahabusu  kwa miaka mingi  kwa kisingizio cha kutokamilika upelelezi.

 Maadamu demokrasia inaitenga dini kando na siasa na kufadhilisha zaidi maslahi na matamanio ya nafsi kwa kuliko jambo lolote, ni wazi haitarajiwi majaji na watawala kusimamia na kutenda haki, na badala yake watafanya ufisadi katika ardhi.

 Uislamu chini ya serikali yake ya Khilafah ndio inayotoa na kusimamia haki kwa raia wote bila ya ubaguzi na wala kuwazingatia dini, asili za wanapotoka, rangi wala kabila zao. Aidha, vipingamizi vyote katika utoaji haki vitaondoshwa, kama rushwa na utesaji wa watuhumiwa, jambo ambalo ni marufuku kabisa.  Bila ya kutaja utaratibu mwanana wa Kiislamu katika kuwasilisha ushahidi. Kama alivyosema Mtume(saaw) :

«البيّنة على المدّعي واليمين على من أنكر»

"Kuwasilisha ushahidi ni juu ya mlalamikaji, na kiapo ni juu ya mlalamikiwa".

(Al-Baihaq)

Mfumo wa kimahkama wa Kiislamu chini ya Khilafah ndio mfumo pekee uliodhihirisha kitareekh kwa ubora na kufaa kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Hii ni kwa sababu Uislamu hutoa wachamungu wanaomuogopa Allah (swt) wanaoishi na kufanya matendo yao wakilenga kupata radhi za Allah swt kwa maisha ya milele ya akhera, na kamwe hawashughulishwi na starehe za kupita za kidunia. Hivyo, maqadhi na watawala hutarajiwa kushikamana ipasavyo na uchamungu katika utoaji haki. Na lau yoyote miongoni mwao atakengeuka, atawajibishwa (kumuhesabu) bila ya khofu na taasisi thabiti ya Mahakama ya juu ya kupambana na dhulma (Mahakmatu Madhaliim) na pia atawajibishwa na raia jumla, watatenda hilo raia bila ya kukhofu wala lawama ya mwenye kulaumu.

 

Imeandikwa na Ramadhan Said Njera

Mjumbe wa Afisi ya Habari

Hizb ut-Tahrir Tanzania

 

Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Read 585 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…