Tuesday, 20 March 2018 00:00

Salam Kwa Kuingia Mwezi Mtukufu wa Rajabu

Alhamdullilah tunawapongeza Umma wetu mashariki na magharibi kwa kuingia ndani ya mwezi wa Rajab, mmoja miongoni mwa miezi mitukufu. Ndani ya mwezi huu tukithirishe kufanya ibada mbalimbali, tuwakumbushe Waislamu matukio minasaba yaliyotokea ndani ya mwezi huu likiwemo tukio kubwa la kugonga nyoyo zetu la kuangushwa Khilafah ya mwisho  lililotokea mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijri/ 3 Machi 1924. Aidha, tuwakumbushe Waislamu  ufaradhi wa kuirejesha tena dola hiyo.

Pia, tunawakumbusha Waislamu wanaodaiwa Swaumu ya Ramadhani iliyopita wamalize kulipa kwa haraka. Na zaidi tusisahau kuomba dua ya nusra kwa Umma wetu mtukufu.

01 Rajab 11439 Hijri /  19 Machi 2018 Miladi

Masoud Msellem

Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Read 1076 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…