Thursday, 07 June 2018 00:00

WAACHIWE HURU SIO MAGAIDI. 3

Risala Ya Wiki No. 10
Ramadhan 1439 Hijri / Juni 2018 Miladi

 

Ni katika mwezi huu mtukufu wa wa Ramadhani ambapo Mtume wetu SAAW alianza kupewa wahyi kwa ajili ya kuufikisha na kuwakomboa wanadamu wote kutokana na kila aina ya madhila, yawe ya kijamii, kiuchumi, kisiasa nk.
Risala ya Mtume SAAW licha ya kuwa ikitumia njia ya kifikra na kisiasa bila ya kuhusisha nguvu, vurumai wala fujo ilikabiliana na kila upinzani, shutma na uadui mkubwa kutoka kwa makafiri wa kiquraishi wa Makka.

Uadui huo ulianza kwa propaganda chafu za uwongo hadi kudiriki kutumia vitisho na nguvu. Haikumalizia hapo bali Waislamu waliendelea kuhujumiwa katika nyanja mbali mbali kama kuekewa vikwazo, kutengwa, mateso na hadi baadhi ya wafuasi wa Mtume SAAW kuuwawa mashahid. Mfano, hai ni familia ya mzee Yassir.

Mtume SAAW alitambua fika kuwa ujumbe wake ni mzito na sio mzahamzaha, kwa kuwa daima kanuni ya kudumu ya haq lazima ilete mgongano na batil, ndio maana mara alipoaanza kupokea wahyi awali kabisa alitamka wazi kwamba: ‘hakuna tena raha baada ya leo’

Mateso, vikwazo na idhilali dhidi ya Waislamu wa mwanzo na mpaka wa mwisho ni kutokana na ukweli kuwa risala (ujumbe) ya Kiislamu kwa kuwa ni haq kutoka kwa Muumba lazima izae mgongano wa kimaumbile na mifumo amma taratibu zote zilizo kinyume nao. Kwa maneno mengine Uislamu (haq) haviwezi kuwiva chungu kimoja na ukafiri (batil)

Ni kwa sababu ya ukweli huo ndio wakati wote katika historia, vitu viwili hivyo vimekuwa vikigongana migongano ya wazi kwa kuwa vina mielekeo na vipimo tofauti, kamwe haviwezi hata siku moja kuwepo bila ya mgongano.

Mitume (A.S) waliotangulia walikabiliana na upinzani kutokana na ukweli huo, Mtume SAAW alipambana na hali hiyo hiyo, masahaba zake ni vivo hivyo, basi hiyo ni dalili fika kuwa kuwa jambo hilo ni mchakato endelevu kwa kila mwenye kuibeba haq inavyostahiki kubebwa kwa udhati wake, yatamsibu yale yale yaliyowasibu walio kabla yetu.

Leo magereza na mahabusu ulimwengu mzima yamesheheni Waislamu walio kizuizini pasina makosa (hatia) ikiwemo pia hapa Tanzania ambapo ndugu zetu wanachama watatu wa Hizb ut Tahrir, Ustadh Ramadhan Moshi, Omar Salum na Waziri Suleiman, wote wakiwa ni walinganizi wa Uislamu kwa kutumia njia ya Mtume (SAAW) isiyohusisha matumizi ya nguvu wala mabavu. Lakini kinachowasibu wao na wengineo ni kile kile kilichowasibu waliotangulia. Ni natija/matokeo ya mgongano baina ya haq na batil.

Tuchukue fursa hii kuwaarifu kuwa ndugu zetu hao watatu tuliowataja majina yao, yaani Ustadh Ramadhan Moshi, Waziri Suleiman na Omar Salum watafikishwa tena mahkama ya Wilaya, Mtwara Mjini InshaaAllah kesho tarehe 06/06/2018 kwa ajili ya kutajwa tena kesi yao.

Itakumbukwa kuwa ndugu zetu hao wamekuwa mahabusu zaidi ya miezi sita sasa bila ya kesi yao kuendeshwa. Tuchukuwe fursa hii kumuomba kila mpenda haki na uadilifu kusimama kidete kukemea dhulma hii inayombatana na ubaguzi wa wazi wa kidini.

Aidha, tunawataka wasimamizi wa sheria wawachie huru vijana hao mara moja ili waendelee na maisha yao na familia zao, kwa kuwa hawana tembe ya hatia.

Mwisho, tuwaombe Waislamu licha ya wao kukemea dhulma na uonevu huu, pia wayatumie vyema masiku haya kumi matukufu ya kumi la mwisho wa Ramadhani, kumuomba Muumba kwa unyenyekevu ili Awakomboe ndugu zetu hao na Waislamu wote ulimwengu wakiwemo ndugu zetu Waislamu wa Jumuiya ya Uamsho kutokana na wimbi hili zito la dhulma na uonevu.

#WaachiweHurusioMagaidi

Afisi ya Habari - Hizb ut- Tahrir Tanzania

20 Ramadhan 1439 Hijri | 05-06-2018 Miladi

http://hizb.or.tz/

https://www.facebook.com/Hizb-ut-Tahrir-Tanzania

Read 200 times
More in this category: « Waachiwe Huru Sio Magaidi
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…