Tuesday, 21 February 2017 00:00

Changamoto Za Wanawake Katika Mikusanyiko Ya Kijamii Na Ummu Ammar

Written by 
Rate this item
(0 votes)

 1. Uchukuwaji wa video. Hili hata kama hufanywa na wanawake wenzao lakini inapokuja wakati wa kuhariri kanda, kuitengeza vizuri  na  usambazaji wake hakuna dhamana kabisa ya mambo hayo kutendwa na wanawake. Au pia katika usambazaji hakuna dhamana ya kubakia kanda ile katika mikono ya mahrimu au wanawake wenzao. Matokeo yake husambaa
na kutizamwa na watu jumla jamala. Jambo ambalo ni hatari.
 • Leo tunakabiliwa na wimbi kubwa sana la kushamiri mitandao ya jamii kama watsapp, facebook nk. Na wengi wa wanawake wanamiliki simu zenye uwezo wa kusambaza picha hizo na hata vedio fupi (clip) kwa sekunde chache na kuzisambaza dunia nzima. Wanawake katika mikusanyiko kama hii wengine hucheza madufu kwa kushereheka nk.(Jambo ambalo sio haramu). Matokeo yake vedio yake inasambazwa dunia nzima. Hili nalo ni jambo gumu ambalo inabidi mama na dada zetu wajizatiti vya kutosha katika kukabiliana nalo.   Tangu kuingia hizi simu zenye camera. Suala la kupiga picha kila kitu limekuwa uraibu mkubwa, limeruka mipaka kiasi cha kukera na hata  kupelekea katika uharamu.  Utaona wakati mwengine mtu amepatwa na janga kama ajali au jenginelo badala ya wapitanjia kumpa msaada kuokoa maisha yake wao hushughulika hae hae kupiga picha. Hii ni changamoto ya kutisha sana  katika mikusanyiko ya hususan wanawake. Kushindwa kuikabili changamoto hii kunapelekea kusambaa picha ambazo wahusika walijihisi wako katika faragha lakini kumbe hali ni kinyume na ilivyo. ‘Mambo yako hadharani’
 • Ukiachilia usambazaji wa picha katika mitandao ya kijamii . Wengine hupiga picha za kawaida tu au vedio fupi (clip) bila ya kuzisambaza katika mitandao ya kijamii na hubakisha katika simu zao. Hata  hivyo, simu hizo huangaliwa na watu mbali mbali kama waume zao, jamaa ndani familia kama maharimu zao nk.  Matokeo yake picha zinawafikia watu wasiostahili kumuona mwanamke katika hali aliyonayo.
 • Hilo hudhihirika katika hali za mikusanyiko ya wanawake baina yao. Ni kweli sheria ya Kiislamu inawaruhusu katika mikusanyiko kama hiyo baina yao kujipamba, kudhihirisha mapambo yao, kushereheka kwa namna ya kihalali na kupunguza mavazi ya stara ya maisha jumla(Public). Hilo sio makosa wakiwa ni baina yao. Lakini katika mikusanyiko hiyo hudhihirika changamoto zifuatazo:

  Katika mikusanyiko yetu ya kijamii kama sherehe za ndoa, mama na dada zetu inabidi wawe waangalifu sana.  Si hivyo wanaweza kubeba dhima ya kumuasi Muumba wao, kupoteza heshima zao au hata kuathiri mahusiano  ya ndoa zao.

  Twataraji akina mama katika maharusi na mikusanyiko ya wanawake peke yao itabidi wayaangalie haya kwa jicho la umakini na kwa moyo wa ucha Mungu  kama kweli  wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.

  Read 384 times
  Top
  We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…