Friday, 24 March 2017 00:00

Khilafah ndio mkombozi wa Wanawake- No.4

Written by 
Rate this item
(0 votes)

Tofauti baina  ya Wanawake katika Ubepari na Khilafah

Tunatarajia kuwa Khilafah italeta mageuzi makubwa katika muundo wa kijamii wa kiulimwengu  hususan masuala ya kiuchumi. Kwa kuleta mageuzi katika uchumi wa kidunia na kuanza kushughulikia masuala ya umilikaji mali na ugawanyaji wa rasilimali ipasavyo zinazotokana na uzalishaji ni wazi ufukara utapungua ulimwenguni.  Na hili litachangia pia kwenye mageuzi ya kitabia ya wanadamu hususan wanawake. Hili litatokana na mabadiliko ya kimfumo. Hali hiyo itapelekea kutokea yafuatayo:

  • Punguzo la maradhi ya wanawake. Tunatarajia maradhi mengi yanayowakumbwa wanawake yatapungua kwa kuwa elimu haitabanwa na utafiti wa maradhi mbali mbali utakuwa huru na hata teknlojia haitabanwa kama ilivyobanwa kipindi hiki kwa kigezo cha hakimiliki. Na pia fikra za uhuru zitapigwa marufuku zinazowafanya watu kujitumbukiza katika maovu.
  • Punguzo na hatimaye kukomeshwa kwa unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia ambao wanawake wanaupata ndani ya ubepari utakwisha kabisa kwani unyanyasaji wa kijinsia ni jambo ambalo halipo kwenye Uislamu. Na zaidi Uislamu umempa mwanamke haki zake zote za msimgi ambazo anatakiwawa azipate. Pia umezuiya uvaaji wa nusu uchi na kudhihirisha mapambo. Mambo ambayo hupekeka kushawishi kutukia vitendo vya udhalilishahaji.
  • `Kuwatatulia wanawake matatizo yanayotokana na masuala ya ukosefu wa ajira. Kutokana na ajira kuwa ni tatizo basi wanawake nao wamekuwa wanakumbana na matatizo mengi kutokana na umasikini kukithiri kupita kiasi. Khilafah itasaidia kupunguza tatizo hili kwani watu watapata ajira kutokana na fani walizonazo ila sio kwa ubaguzi wa aina yoyote ile. Wanawake haitokuwa tabu kwenye kupata ajira na hutokumbwa na tatizo la kuombwa rushwa ya ngono.
  • Wanawake ndani ya Khilafah watapata ustawi wa familia. Katika ubepari wanawake wamekosa kupata ustawi wa kifamilia na wengi wao wamejikuta wanalea watoto peke yao. Hili linatokana na mfumo kushindwa kuhakikishia ustawi wa jamii kiujumla

Mwisho, sisi mashababu wa  Hizb ut-Tahrir  tunawaalika wanawake wa Kiislamu kuungana nasi katika kulingania kurudisha maisha ya Kiislamu kupitia kurejeshwa kwa dola ya Kiislamu(khilafah). Khilafah ndio ngao itakayowakinga wanawake na madhila na manyanyaso wanayoyapata  leo kutokana na mfumo dhalimu wa kibepari. Na  ndio itakayobadilisha nafasi ya mwanamke kutoka kuwa kifaa cha starehe na kutangazia biashara  na kumuinua juu ya nafasi na hadhi ya juu kama alivyomuweka Muumba wake.

 

              

 

                 

Read 467 times
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…