Athari Mbaya Itokanayo Na Kunasibishwa Elimu Na Ajira Katika Mfumo Wa Kirasilimali

Ni dhahiri kwa mwenye macho na anayefuatilizia kwa umakinifu kuona kuwa nidhamu ya elimu katika mfumo wa kirasilimali imefeli. Hii ni kutokana na kule kuambatanishwa moja kwa moja na suala la riziki au ajira. Dalili ya haya ni kauli mbiu ambayo husikika mara kwa mara wanafunzi wakihimizwa na walimu au wazazi kutia bidii ya juu masomoni ili kuweza kujipatia kazi nzuri (mfano mzuri ni wimbo maarufu wa ‘someni vijana’). Serikali nazo zimechangia pakubwa tatizo hili katika kuweka mfumo wa alama
(grading system) unaoleta dhana kuwa mwanafunzi atakaye hitimu masomoni na alama za chini ameharibikiwa maishani. Fahamu hii fisidifu imechangia pakubwa kuwepo majanga katika sekta ya elimu
yakiwemo:

Wanafunzi kugeuka kuwa marobot kusoma nadharia kwa ajili ya kupata alama za juu za kutafutia ajira badala ya kuwa mufakkireena (thinkers). Malalamishi haya pia yametolewa na waziri wa elimu bwana Matiangi akisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi huhitimu vyuo vikuu kabla ya kufanya tafiti zozote
kutumia elimu yaokatika kufichua na kuboresha masuala kadha wa kadha katika fani zao.

Kukithiri udanganyifu katika mitihani na utengezaji wa shahada ghushiimekuwe donda sugu ili kufanikiwa kupata ajira. Maafisa wa elimu hupewa hongo na baadhi ya wazazi kuiba mitihani na kuwawezesha
watoto wao kupata alama za juu. Hili linafanyika waziwazi na sio siri. Msongo wa mawazo kwa walimu na
wanafunzi. Wanafunzi wakishinikizwa na wazazi, na walimu wakishinikizwa na idara za shule kupata alama za juu ili kuzitafutia soko shule hizo. Natija yake ni yale tulioshuhudia hivi majuzi ya mashule kuteketezwa. Ambapo yadaiwa baadhi ya walimu pia walihusika.

Ama katika Uislamu, elimu na riziki ni vitu viwili tofauti wala havifai kuchangwa au kimoja kufanywa kuwa sharti ya chengine. Chini ya serikali ya Kiislamu ya khilafah, msingi wa siasa ya elimu ni Aqeeda ya Kiislamu. Nayo ni kumfahamisha mwanafunzi kuwa lengo kuu la kusoma ni kunali radhi za Allah kwa kunufaika nayo na kuwanufaisha wengine. Na riziki kama mojawapo ya masuala ya aqeeda, haiko mikononi mwetu bali iko
katika mzunguko unaomtawala mwanadamu. Kupita au kutopita mtihani sio kipimo kinachoashiria kiwango cha riziki atayokuwa nayo mtu. Ajira hutegemea weledi au ujuzi wa mtu alioubeba akilini mwake katika fani fulani pasi na kuzingatia alama zilizoandikwa katika makaratasi ya mtihani. Mtazamo huu utawashajiisha wanafunzi kusoma kwa ajili ya kuwa wajuzi imara na sio kwa ajili ya kupita mitihani na baada ya hapo kusahau waliosomeshwa.

Ama lengo la siasa ya elimu katika Uislamu chini ya serikali ya Khilafah litakuwa kuwasomesha wanafunzi elimu yenye maana kwao katika mambo ya kimaisha badala ya kuwabebesha mzigo wa masomo mengi
usiowaleteafaidayoyote maishani mwao pindi baada ya kuhitimu masomoni. Hatimaye serikali kubuni fursa muafaka zitakazo wawezesharaia wake kujikimu kimaisha ima kama wafanyikazi wa umma au wa kibinafsi.

Na Masoud Salim Mazrui

Maoni hayajaruhusiwa.