Dola ya Uturuki na uadui wake kwa uislam

0

وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ

“Na wala usidhani kwamba Allah ameghafilika na wanayoyatenda madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao” (14:42)

Utawala wa kisekula wa Uturuki unaoongozwa na Chama AKP (Justice and Development Party) chini ya Recep Tayyip Erdogan unajidhihirisha zaidi kuwa tawi la ukafiri katika mapambano yake dhidi ya Uislamu na walinganizi wa daawa ya Kiislamu. Mamlaka ya kimahkama nchini Uturuki imeridhia maamuzi mawili ya kimahkama yanayoruhusu kuwafunga wanaharakati mpaka miaka 15.

Karibuni ndani ya siku ya  Ijumaa  tarehe 23 Juni 2017 wakati wa maghribi, Jeshi la polisi (Kitengo cha Kupambana na Ugaidi) kilivamia ndani ya nyumba ambamo ndugu yetu Yilmaz alikuwa anajumuika na ndugu zake wengine wa Kiislamu kwa ajili ya futari, kisha kumtia nguvuni kwa mabavu na kwa ushenzi mkubwa, bila ya kujali wakati huo wa futari. Kana kwamba utawala huo unatangaza kuendelea kushikilia msimamo wake wa kuvunja heshima juu ya matukufu ya Allah Taala, tena ndani ya kumi la mwisho la mwezi mtukufu.
Sisi kwa upande wetu katika Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir tunatangaza kwa kinywa kipana kwamba umefuzu upeo wa kufuzu ewe Yilmaz…   umefuzu ewe Yilmaz kwa kubeba daawa ya Kiislamu…… Umefuzu ewe Yilmaz kwa kusimama kidete mbele ya madhalimu…….! Umefuzu kwa kutiwa nguvuni ndani ya usiku wa tarehe 29 Ramadhan ambao ndani yake watu huachwa huru kutokana na moto

(Umefuzu) …. kwa kuwa ulinganizi wetu ni ulinganizi wa Allah Taala, na kwa uwezo wa Allah inshaaAllah utafika kilele chake kwa kurejesha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha tena dola ya Khilafah Rashidah kwa manhaj ya Utume. Dola itakayoleta izza kwa Uislamu na Waislamu, na kuleta idhilali kwa ukafiri na wafuasi wake. Kwa hakika miadi yao (ya kuadhibiwa) ni nyakati za alfajiri, basi jee (wanadhani) alfajiri ipo mbali?

29 Ramadan 1438 AH /   24 Juni 2017 CE

Kufuatia dhulma hiyo ya kutiwa nguvuni ndugu yetu Yilmaz Celik  Hizb ut Tahrir Wilayah  ya Uturuki  imeanzisha  kampeni kabambe kushinikiza kuachiwa huru.  Kauli mbiu ya kampeni:  “Yilmaz Celik  hayuko pekee”.

Kampeni inaendeshwa pia kupitia mitandao ifuatayo ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kiarabu:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/ar/index.php/dawahnews/turkey/44922.html

Kizungu:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/dawah/turkey/13399.html

Kituruki:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/tr/index.php/dava-haberleri/t%C3%BCrkiye/9340.html

Tafadhalini sana  sambazeni kadiri muwezavyo mwito, makala, picha za kampeni hii. Pia tuungeni mkono kwa kuchangia ndani ya mitandao ya Twitter na Facebook.

Barak Allahu Feekum.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.