Hali Ya Mazingira Mitaani Hairidhishi

0

Mazingira ni kila kitu kinacho mzunguka mwanaadamu.Iwapo mwanaadamu atakuwa ni mwenye kupuuza kuhifadhi mazingira yake basi litakuwa ni jambo la kimaumbile kwa mwanaadamu kuwa ni mwenye kuathirika kwa kuwa mgonjwa na hata mwisho kuangamia.Katika maisha tunayoishi leo imedhihirika wazi kuwa upungufu wa usafi kwa mazingira ni njia moja wapo kubwa ya kuleta maradhi duniani.

Miongoni mwa njia moja wapo ya kuchafuwa mazingira ni utupaji wa taka ovyo ovyo mitaani.Pindi taka zitakapo sambazwa ovyo mitaani,ipo hatari ya kusababisha matatizo ya kiafya kwa jamii.Mara nyingi,imekuwa desturi kwa watu mitaani kutupa ovyo winda/binda{diapers} za watoto zilizo ja kinyesi na mikojo kando kando mwa barabara.Kwa watu kukosa haya, maadili mema pamoja na usimamizi bora kutoka serikali,leo utakuta mipira ya uzazi(condom)sodo(pads),maji machafu,mifuko ya lailoni na hata mabaki ya vyakula yamejaa mabara barani na hata katika ploti za watu ambazo hazija jengwa.Katika mtaa wa Bamburi,Kiembeni,Vok,kibarani na katikati mwa jiji la Mombasa yaani marikiti,utakuta taka zimejaa hadi nafasi ya kupita magari hamna na harufu kuwa chafu mno.

Ingawa wakaazi wanayo sehemu yao ya lawama nayo ni wao kutokuwa na ustaarabu wala kuhisi masuliya,lakini sehemu kubwa ya lawama yastahili ipewe wasimamizi wa jiji .Hakika wasimamizi wame feli kutengea wakaazi sehemu za kutupa taka.Ama katika miji walio watengea sehemu hizo,mara kwa mara wamekuwa ni wenye kuchelewa kuja kuzibeba taka hizo. Ilikuwa ya stahili kwa baraza la jiji kuwa ni lenye kutenga masiku maalum ya kubeba taka kwa kila nyumba ili kuwezesha kutopatikana kwa majaa ya taka mijini na vijijini.

Ama kuhusu maji machafu,kutokana na mpango duni wa kupangilia muundo wa jiji,imelazimu kila mmiliki wa nyumba kuchimba mashimo yake binafsi.Ama   kwa wale walio hisi kuwa hii ni gharama kubwa basi wakawa ni wenye kuchimba mitaro ambayo inalekezwa barabarani.Ndio utakuta leo ikawa si ajabu maji ya visima yamejaa harufu chafu na bara bara zetu kugeuka kuwa ni mabomba ya maji machafu.Je ikiwa hali ni kama hii vipi kusiwepo na miripuka ya maradhi?Je yako wapi mabomba ya maji machafu ambayo yamechimbwa na baraza la jiji ili wakaazi waweze kuunganisha majumba yao na mabomba haya?

Kwa kweli mabaraza ya jiji yameshindwa kusimamia na kuweka mazingira kuwa masafi na miaka nenda miaka rudi hayataweza kufaulu kufikia lengo hili.Na hii nikutokamana na kuwa warasilimali ambao ndio wanao ongoza ulimwengu leo hawataki kuona mabaraza ya jiji yana ajibika kutokamana na wao ni wamiliki wa makampuni ya kuzowa taka. Iwapo mabaraza ya jiji yatawajibika,basi huoni kuwa kampuni haya ya warasilimali yatafilisika jambo ambalo warasilimali hawatalikubali litokee.

E nyi watu ,ili mazingira yetu yawe masafi kwa uhakika,hamna budi mwanzo sisi wenyewe tuweni wastaarabu nakuhisi ni masuliya kwa vitendo tunavyofanya.pia lazima tulihisabu baraza la jiji kwa kuto ajibika kwake .mwisho pia lazima tufanyeni haraka kuleta mageuzi kwa mfumo tawala wa leo ambao warasilimali ndio wenye kuusimamia na kuwa naathari kubwa kwa jila jambo.

Na Mwalimu mohamed

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.