Inna Lillah Wainna Illayhi Raajiun

Kwa huzuni na masikitiko tumepokea taarifa za kufariki dunia leo mwanaharakati wa Hizb ut Tahrir Ally Omari Fatehe kutoka Muheza Tanga.
Kifo kimetokea jana Jumanne 4/08/2020 katika Hospitali ya Muhimbili ambapo marehemu alikuja kwa matibabu.
Familia imo mbioni kufanya taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuulekea Tanga, na maziko yanatarajiwa kufanyika leo InshaAllah huko Muheza, kijiji cha Kwemsala, Tanga.
Marehemu aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi King’wangoko huko Kaliua Tabora ameacha mke na watoto wawili.
Marehemu Ally Omari Fatehe atakumbukwa sana kwa jitihada yake kubwa ya kuutumikia Uislamu, amekuwa mwanaharakati wa Hizb ut Tahrir kwa miaka kadhaa sasa, na pia alikuwa katibu wa Masjid Al Hidaya, Konanne huko Kaliua, Tabora.
Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania natoa mkono wa taa’zia kwa familia ya marehemu, jamaa, marafiki na wanaharakati wote hususan wa Tanga kufuatia msiba huu mkubwa, huku tukiwaombea Allah SWT awape ujira mkubwa na kuwamakinisha kwa subra na istiqama katika kipindi hiki kigumu.
Aidha, tunamuomba Allah SWT amsamehe na kumrehemu ndugu yetu Ally Omari Fatehe na amuingize katika Jannah ya darja ya juu.
Amiin
Inna lililahi wainna ilayhi rajiuun
05 Agosti 2020
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Kwa mawasiliano zaidi kuhusu msiba huu :
0718504912 – (kaka wa marehemu)

Maoni hayajaruhusiwa.