Inna llilahi Wa inna Ilayhi Raajiuun

Kwa masikitiko tumezipokea taarifa za kufariki dunia ndugu yetu Amri Athuman maarufu ‘King Majuto’ aliefariki dunia jana saa 2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. ‘King Majuto’ alifikishwa Hospitalini hapo tangu Julai 31 baada ya afya yake kuzorota kwa muda, na hatimae jana amerudi kwa Muumba Mbingu na ardhi. Yeye ametangulia, na sisi tunafuatia. Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir Tanzania tunatoa mkono wa ta’azia kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu. Tunamuomba Allah Taala Ampe marehemu kauli thabit, Amtakabalie mema yake ikiwemo ibada yake ya Hijja , Amsamehe makosa yake na Amjazie kila penye mapungufu. Amiin 09 Agosti 2018 Masoud Msellem Mwakilishi kwa Vyombo va Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.