Je inajuzu katika Hedhi kusoma Qur’an katika Internet au simu?

Katika kukujibu swali lako kuna mambo matatu yapasa kwanza yawe wazi:

Kusoma Qur’an kwa kinywa (kukariri) sio kutoka katika mas-haf, kuugusa mas-haf na Kusoma Qur’an kutoka katika Mas-haf, na kubeba simu au laptop ambayo ina mambo ya Qur’an na hata kusoma kutoka humo.

1– Kuhusu mwanamke aliyeko katika hedhi kusoma Qur’an kwa kinywa kwa alicho hifadhi.

Ni suala lenye mkanganyiko wa mitazamo baina ya wanazuoni, wapo wanaosema ni haramu wakati wengine wanasema inajuzu. Na hoja yangu nzito ni kwamba katika suala hili ni haramu kwa mwanamke aliye katika hedhi kusoma Qur’an kwa kinywa kwa alicho hifadhi.

Imechukuliwa na Al-Hakim katika Al-Mustadrak kwa masimulizi ya Sulaiman Bin Harb, na Hafs Bin Amr Bin Mara, kutoka kwa Abdullah Bin Salama, amesema: Tulikuja kwa Ali (ra), mimi na wanaume wengine wawili, Ali (ra ) akasema:

«كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقْضِي الْحَاجَةَ، وَيَقْرَأُ الْقُرْآنَ، وَيَأْكُلُ اللَّحْمَ، وَلَمْ يَكُنْ يَحْجُبُهُ عَنْ قِرَاءَتِهِ شَيْءٌ لَيْسَ الْجَنَابَةُ»

“Mtume wa Allah ﷺ alikuwa akijisaidia, na kusoma Qur’an, na akila nyama, na kamwe hakuna kilichomzuia kuisoma (Qur’an) isipokuwa kuwepo katika hali ya kutokuwa twahara (Kuwa na Janaba)”.

Al-Hakim amesema kwamba hii hadith ina Isnad Sahih isnad (mtiririko wa wapokezi), na imethibitishwa na Adh-Dhahabi. Kilicho wazi hapa katika hadith hii ya Mtume ﷺ, nikwamba yeye ﷺ alikuwa akiisoma Qur’an kwa kinywa tu katika nyakati zote isipokuwa alipokuwa hayupo twahara; ikimaanisha kwamba hairuhusiwi kwa mtu asiye twahara kuisoma Qur’an, kinacho maanishwa kwa asiye twahara humaaniswa pia kwa mwanamke aliye katika hedhi katika kipengele cha usomaji Qur’an.

Hivyo hoja yangu ya nguvu ni kwamba Mwanamke aliye katika hedhi asisome Qur’an

2- Kuhusu kugusa Mas-haf (Kitabu) kwa mtu asiyekuwa twahara na mwanamke aliye katika hedhi hairuhusiwi.

Ni Haram kwa mujibu wa kauli ya Allah سبحانه وتعالى:

لَا يَمَسُّهُ إِلَّاالْمُطَهَّرُونَ

 “Hakuna aigusaye ila aliye twaharika”

[Al-Waqi’a: 79].

Na kutokana na hadith tukufu katika kitabu cha Imam Malik in AlMuwatta iliyopokelewa kutoka kwa Abdullah Bin Abi Bakr Bin Hazm, kwamba katika ujumbe ulioandikwa na Mtume ﷺ kwenda kwa Amr Bin Hazm:

«أَنْ لَا يَمَسَّ الْقُرْآنَ إِلَّا طَاهِرٌ»

“Kwamba ni aliye twahara tu anayeweza kugusa Qur’an”.

Katika hadith nyingine iliyosimuliwa na Malik katika  Al-Muwatta, kwa jina kamili la Abdullah, kama ifuatavyo: (kutoka kwa Abdullah Bin Abi Bakr Bin Muhammad Bin Amr Bin Hazm), na kwa kunukuliwa na At-Tabarani katika  Al-Kabeer na As-Sagheer kutoka kwa Salim Bin Abdullah Bin Omar kwa maneno: “kutoka kwa Sulaiman Bin Musa, nimemsikia Salim Bin Abdullah Bin Omar akisimulia kutoka kwa baba yake, alisema: Mtume  ﷺ amesema:

«لَا يَمَسُّ الْقُرْآنَ إِلَّا طَاهِرٌ»

“Mtu aliye twahara tu ndiye huigusa Qur’an”.

Kwahiyo

niwazi kwamba imeharamishwa kwa mwanamke aliye katika hedhi kuigusa Qur’an na hata kusoma kutoka humo (katika Qur’an).

3– Kuhusu kubeba kompyuta mpakato (Laptop) au simu ya kiganjani ambayo ina vitu vitumiavyo Qur’an, tayari wanazuoni wamesha jadili jambo hili ambalo nataka kuanza nalo.

Nalo ni kubeba Mas-haf (kitabu) katika boksi au pochi, wamekuwa na rai tofati.“Wanazuoni wa Hanafi na wanazuoni wa Hanbali wameshika rai ambayo inamruhusu asiye twahara au asiye na udhu kubeba Mas-haf kwa kutumia kamba/uzi, au kitu kingine ambacho hakikushikana nawo, kwa sababu mtu huyo hatakuwa ni mwenye kuugusa, kwahiyo ataruhusiwa kuubeba sawa na kubeba Mas-haf pamoja na mizigo mingine. Na hii ni kwasababu kilicho katazwa hapa ni kuigusa Mas-haf, na katika hali hii hajaigusa Mas-haf. Rai ya madhahab ya Hanaf inasema: kama ataibeba ikiwa imefunikwa (na kifunikio) ambacho hakikushonewa humo au iko ndani ya pochi, au ya kufanana na hayo, basi haikatazwi kufanya hivyo. Wanazuoni wa Malik na Wanazuoni wa Shafi na kutokana na maelezo ya Ahmad, wote wanafuata kwamba hairuhusiwi. Madhhab ya Malik inasema: Ni aliye twahara tu ndiye mwenye kuibeba (Mas-haf) hata ikiwa katika mto (pillow) au vya kufanana navyo, kama Mas-haf kuwa katika stendi (kiweko, kimeza) au kuwa na kifuniko kilicho shonewa au ambacho hakikushonewa. Na ndivyo wasemavyo Madh-hab ya Shafi, na kwa sahihi kinachofahamika kutoka kwao (wawili hao): “Hairuhusiwi kugusa pochi (mkoba) au boksi ambalo lina ndani yake Mas-haf, yaani mfano kama viliandaliwa kwa ajili ya kubebea Mas-haf, ndio kusema haruhusiwi kugusa wala kubeba boksi kwa lengo la kubeba mzigo uliojumuisha  Mas-haf”.

Ni wazi kwamba kuna utofauti katika rai za kifiqh katika su’ala hili, hoja ipi ninaipa uzito (ninayo kubaliana nayo) ni kwamba inaruhusiwa kubeba simu ya mkononi bila kuwa katika twahara (hata kama simu hiyo) itakuwa na program za Qur’an kwa sababu haibebi hukmu za maandishi, na simu za kiganjani zina program nyingi ikiwemo pia Qur’an na hutumika katika  mambo mengi zaidi ya kusoma Qur’an na haibebi sheria za Mas-haf, isipokuwa katika hali mbili:

Ya kwanza: Pindi program ya Qur’an ikiwa imefunguliwa na matini/maandishi ya Qur’an yapo katika kioo (screen) cha simu:

Katika hali hii, matini yaliyo andikwa (yaliyo katika screen) yanabeba hukmu ya Mas-haf kwa sababu ni matini yaliyo andikwa, na kugusa kioo (screen) chenye matini yaliyo andikwa ni haram isipokuwa kwa aliye twahara, kwa sababu huwa ni kama maandishi katika karatasi, kitambaa au ngozi, ambapo Qur’an imeandikwa humo, kwa hiyo iwapo mmiliki wa simu ya kiganjani anataka kusoma Qur’an katika simu yake kwa kufungua kioo (screen), hairuhusiwi, isipokuwa kama yupo twahara. Hali hii pia ni sawa iwapo kioo kipo wazi kuonesha maandiko ya Qur’an ni haramu kuibeba simu hiyo ila kwa aliye katika twahara.

Iwapo simu ya kiganjani haikufunguliwa kuweka katika kioo (screen) maandiko ya Qur’an:

Katika hali hii (simu) inaweza kubebwa na mtu asiyekuwa twahara japokuwa program za Qur’an zimo katika hifadhi ya simu, kwa sababu kufahamu uhalisia (manat) wa simu ya kiganjani, iwapo maandiko ya Qur’an hayapo katika kioo (screen), basi uhalisia huu ni tofauti na uhalisia wa Mas-haf.

Pili: Simu ya kiganjani haina ila program za Qur’an, ambazo hutokea juu (katika kioo) kwa ajili ya kusoma, kwa maneno mengine simu inatumika tu kwa kusoma Qur’an na haina program nyingine. Kwa hali hii, mtu asiye kuwa twahara ni haramu kuibeba/kuichukua.

Hiki ndicho ambacho mimi nime kikubali kuwa na uzito wa hoja. Allah sw ndiye Mbora wa kujua na Mbora wa busara.

Wassalaam Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatuhu

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Imetafsiriwa: Hamza Sheshe

Kutoka katika Jarida la Khilafah. Toleo 47

Kusambaza ni Kuunusuru Uislamu!