Kiinua Mgongo Mwisho wa Utumishi

بسم الله الرحمن الرحيم

Swali:

Huenda ikawa kuna jambo limekushungulisheni, Allah Akusaidieni, nimependa nikukumbusheni swali langu kwa haja yangu kubwa ya jibu. Allah akuwafikisheni na apitishe kheri kwa mikono yenu.

Assalamu Alaykum Warahmatullah, maamkizi mema kutoka kwa Allah kwenu,

Sheikh wetu mkarimu,

Ni ipi hukmu ya kisharia ya kutafuta kiinua mgongo mwisho wa utumishi kwa ajili ya mfayanyakazi aliyetumia miaka kadhaa katika kazi  yake kwa uzuri na akadai mshahara wake “waliowafikiana” kutoka kwa mwenye kazi bila ya dhulma au kasoro katika kipindi chote cha kazi yake?

Na kwa maelezo mengine, je huzingatiwa kiinua mgongo mwisho wa utumishi kulikotajwa katika kanuni iliyopo na inayofanyiwa kazi leo ni haki kisharia kwa ajili ya mfanya kazi aliyemaliza muda wake wa kazi? Na je huzingatiwa yule mwenye kazi kukataa kulipa fedha za malipo ya kiinua mgongo ni kula haki (ya mwengine) na kutenda haramu?

Huku tukizingatia kwamba kanuni iliyopo inaeleza kwamba theluthi moja ya kiwango cha mshahara wake wa kila mwezi kwa kila mwaka wa utumishi alipwe mfayakazi aliyetumikia katika kazi yake kwa muda wa chini ya miaka 5, na theluthi mbili ya mshahara kwa kila mwaka wa utumishi kwa mfanyakazi aliyetumikia katika kazi yake kuanzia miaka 5 – 10, na mshahara kamili kwa mwenye kuvuka miaka 10 katika utumishi.

Allah akupeni baraka.

Kwa heshima nataraji mutanijibu kwa haraka kwasababu ya haja na dharura.

Wasalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Jawabu:

Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh,

Ewe ndugu yangu, hakika Waislamu wanafuata masharti yao (waliyowekeana) kama ilivyoelezwa katika hadithi tukufu, ambayo ameitoa Tirmidh katika Sunan yake na akielezea kuwa ni hadithi hasan  na ni sahihi: “Ametueleza Kathir bin Abdillah bin Amr bin Auf Almuzani kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kwamba Mtume (SAAW) amesema: Na Waislamu wanalazimika kufata masharti yako (waliyowekeana) isipokua sharti lililoharamisha halali au lililohalalisha haramu”.

Hivyo basi, ikiwa pameelezwa katika mkataba wa kazi kati ya mfanyakazi na mwenye kazi sharti kwamba mfanyakazi atalipwa kiinua mgongo fulani mwisho wa utumishi, basi itakua ni haki ya mfanyakzi kwa mujibu wa sharti la mkataba.

Vilevile, ikiwa mkataba wa kazi kati ya mfanyakazi na mwenye kazi unafuata kanuni ya masharti ya kanuni ya kazi inayotakiwa kutendwa na mwenye kazi, na ikawa kanuni hii inaeleza kwamba mfanyakazi atalipwa kiinua mgongo fulani mwisho wa utumishi, basi kitakua (kiinua mgongo hicho) ni haki ya mfanyakazi kwa mujibu wa sharti la mkataba.

Ikiwa hakuna lolote lililotajwa katika haya kama ilivyobainishwa hapo juu, basi hupewa mshahara wake tu (huyo mfanyakazi) na hatalipwa kiinua mgongo cha mwisho wa utumishi.

Haya ndiyo ninayoyaona sawa katika mas-ala haya. Na nataraji yamekaa wazi, na Allah ndie mjuzi zaidi na mwenye hekima zaidi.
Ndugu yenu Ata ibn Khalil Abu Rashta

11, Rajab 1440H

13, March 2019.

Maoni hayajaruhusiwa.